
17/08/2025
MAFUA NA DAWA ZAKE; FAIDA NA MADHARA YAKE
Mafua ni tatizo lenye kasi kubwa katika jamii na huambatana na dalili nyingi.
Kawaida mafua ni tatizo linalokuja ghafla, lenye kutokana na maambukizi ya virusi maeneo ya mfumo wa hewa wa juu.
AINA ZA MAFUA
1. Mafua yatokanayo na virusi aina ya rhinoviruses (Common cold)
2. Mafua yatokanayo na virusi aina Influenza virus (Flu)
1. COMMON COLD (MAFUA)
Mafua haya huambatana na dalili zifuatazo ambazo ni kukohoa, pua kujaa maji maji mithili ya k**asi na huweza kuziba, homa ya kawaida na uchovu ambapo dalili hujitokeza kati ya siku 1 hadi 2 mara baada ya kukumbwa na virusi. Dalili nyingi hutoweka kati ya siku 7 hadi 10, ingawa dalili nyingine huchukua karibia wiki tatu kutoweka
Uwezekano wa kuugua mafua ya aina hii hupungua kadri umri unavozidi kuwa mkubwa. Baadhi ya tafiti zimeweza kutambua kuwa watoto huugua mara sita hadi nane kwa mwaka ikilinganishwa na wazee wenye umri chini ya miaka 60 ambao hupatwa mara tatu hadi nne kwa mwaka, wakati watu wenye umri zaidi ya 60 hupatwa mara moja kwa mwaka.
Ukiachana na sababu ya umri, sababu nyingine zinazopelekea kupatwa mafua ni kutopata muda wa kulala vya kutosha na mawazo.
Mafua ya aina hii kawaida hayawezi kusababisha madhara makubwa ila mgonjwa mwenye pumu, pneumonia na magonjwa mengine yupo hatarini zaidi
NB: Common cold (mafua) watu wengi huchanganya na aina hii nyingine ya mafua (influenza virus)
2. FLU (MAFUA)
Mafua ya aina hii husababishwa na virusi aina ya influenza, influenza virus vimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Influenza A, B au C. Influenza A na B huathiri zaidi wanadamu lakini Influenza A hupelekea dalili kuwa mbaya zaidi. Influenza virusi inaweza kuwa hatari zaidi kwa wazee na wenye kinga ya mwili pungufu. Kawaida wagonjwa wenye mafua yatokanayo na influenza virus huugua zaidi ya wale wenye mafua aina ya common cold. Mara nyingi dalili za mafua aina flu ni k**a zifuatazo joto la mwili kupanda, hali ya kujisikia baridi sana, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, na hali ya kujisikia uchovu
MAKUNDI YA DAWA AMBAYO HUTUMIKA KATIKA MATIBABU YA DALILI ZA MAFUA (PHARMACOLOGIC AGENTS)
1. Kundi la dawa la decongestants
K**a mgonjwa ana shida ya pua kujaa maji maji na k**asi, dawa zilizopo katika kundi la decongestants husaidia zaidi kupunguza hali hio.
Decongestants ni dawa ambazo huongeza msukumo wa damu puani hivyo kupelekea kupungua kwa ujazo wa maji maji na k**asi puani
Dawa zilizopo katika kundi hili la decongestants ambazo hutumika sana ni phenylephrine na pseudoephedrine
Kundi hili la decongestant kuna dawa zipo katika mfumo wa sprei hasa zile zinazofanya kazi haraka na kwa muda mfupi dawa hizo ni ephedrine, na-phazoline, na phenylephrine, pia zipo dawa ambayo hufanya kazi kwa muda mrefu oxymetazoline.
Muunganiko wa dawa hizi za kundi la decongestants husaidia zaidi kupunguza hali hii ya tatizo la mafua.
Vidonge vya pseudoephedrine hutibu kwa haraka zaidi kuliko phenylephrine.
Dawa za kundi hili la decongestant ni salama zaidi endapo zikatumika kwa usahihi lakini matumizi yake hupelekea madhara zaidi kwa kuamsha mfumo mkuu wa fahamu. Baadhi ya madhara ni k**a yafuatayo kukosa usingizi, ongezeko la presha mwilini, kukosa utulivu, wasi wasi au hofu, mapigo ya moyo kuongezeka, na pia tatizo katika mfumo wa mkojo
Dawa hizi zinapaswa kuepukika kwa watu wenye matatizo ya moyo, shinikizo la damu, kisukari na kuvimba kwa tezi dume.
Pia dawa za kundi hili hazipaswi kutumiwa kwa pamoja na dawa za kundi la monoamine oxidase inhibitors ambazo ni rasagiline (Azilect), selegiline (Eldepryl, Zelapar), isocarboxazid (Marplan), phenelzine (Nardil), na tranylcypromine (Parnate).
2. Kundi la dawa la Antihistamines
Kundi hili la dawa linaweza kutumika Ili kupunguza hali ya pua kutokwa na maji maji au k**asi kwa wingi, macho yenye kuwasha na yenye kutoa maji maji na chafya inayoambatana na mafua aina ya common cold
Kundi la antihistamine zimegawanyika katika makundi mawili
Kundi la kwanza la dawa hizi ni brompheniramine, chlorpheniramine, na clemastine hupendelewa kutumiwa kuliko dawa za kundi la pili
Kundi la pili la dawa hizi ni cetirizine, fexofenadine, na loratadine. Dawa za kundi hili haziwezi kupenya na kuingia ndani ya ubongo
Ubora wa dawa kundi la kwanza umetokana na uwezo wa hizi dawa kufanya kazi maeneo ya histaminic na muscarinic katika ubongo (medulla).
Dawa hizi za husaidia kupunguza athari za mafua kwa haraka hata ikitumiwa aina moja ya dawa lakini imeonekana kusaidia zaidi endapo dawa za kundi hili zikatumiwa kwa pamoja na kundi la dawa la decongestant na dawa za maumivu
Kundi la kwanza la dawa za antihistamines huambatana na madhara tofauti tofauti kwasababu ya uwezo wake wa kuingilia mfumo mzima wa mfumo wa fahamu.
Dawa hizi zinapelekea kupatwa na usingizi mzito, hulevya, mwili kuchoka na pia zinapaswa kutumiwa kwa uangalifu kwa wagonjwa wenye matatizo la akili kwasababu zinaweza kupelekea upotevu wa kumbu kumbu na matatizo ya kutembea
Pia, dawa hizi za kundi la kwanza huambatana na madhara yafuatayo hupelekea macho kuwa makavu, mkojo kubaki kwenye kibofu, choo kigumu
Onyo; dawa za kundi la antihistamine zisitumike kwa wagonjwa wenye glaucoma na kuvimba kwa tezi dume
3. Kundi la dawa la Antitussives
Dawa nyingi utazozikuta kwenye maduka ya madawa kwaajili ya kutibu mafua utagundua dawa ya kundi hili ipo ndani hass dextromethorphan
Dextromethorphan ni dawa iliopo kundi la antitussive ambapo hupunguza zaidi hali ya kukohoa ambayo huambatana na mafua au magonjwa mengine ya koo.
Dextromethorphan hupatikana k**a dawa moja lakini pia unaweza kuipata katika muunganiko na dawa nyingine katika kutibu dalili zaidi ya moja ya mafua.
Endapo ikatumiwa kwa kiwango kikubwa dextromethorphan husababisha dalili za magonjwa ya akili kujitokeza ambazo hufanana na zile zitokanazo na dawa za phencyclidine na ketamine;
Pia kiwango kikubwa cha dextromethorphan hupelekea mapigo ya moyo kuongezeka, mabadiliko ya mfumo wa akili, shinikizo la damu, kifafa, coma na mapafu na moyo kufeli kufanya kazi
4. Kundi la dawa la Expectorants
Kundi hili la dawa hufanya kazi kwa kupunguza uzito na ujazo wa maji maji mithili ya k**asi puani kwa mgonjwa yeyote yule mwenye matatizo ya mfumo wa hewa.
Guaifenesin ni dawa pekee ambayo mara nyingi ndio hutumika katika kundi hili. Ijapokuwa guaifenesin imekuwepo katika muunganiko na dawa nyingine
Licha ya kukosekana kwa baadhi ya taarifa zinazohusu ubora wa dawa hii, lakini guaifenesin imeendelea kutumika k**a dawa bora katika kundi hili
Dawa hii ni salama na haijahusishwa na mwingliano na dawa nyingine. Endapo ikitumika katika kiwango sahihi, dawa hii inavumilika kwasababu mara nyingi imehusishwa kuwa na madhara katika mfumo wa tumbo
5. Dawa za kutuliza maumivu na homa (Analgesic & antipyretic)
Dawa k**a aspirin, paracetamol, ibuprofen na naproxen mara nyingi hutumika katika kupubguza maumivu mwilini, maumivu ya kichwa na homa ambayo huambatana na mafua
Dawa zote hutoa matokeo sawa kulingana na dalili za mafua, ila inabidi zitumike kwa uangalifu kwasababu zimeambatana na madhara makubwa
Mgonjwa ambae ana aleji na aspirin na yule mwenye vidonda vya tumbo hawapaswi kutumia aspirin au dawa ya maumivu
NAMNA YA KUJIKINGA MWENYEWE
Virusi wanaosababisha baridi na mafua wanaweza kuenezwa kutoka kwa mtu alieathirika kwenda kwa wengine kupitia hewa na migusano.
Pia, unaweza kupata maambukizi kupitia migusano ya kinyesi. Hii hutokea pindi unapogusana mikono na mtu mwenye maambukizi au kugusa uso wake alaf uguse tena macho, mdomo au pua yako.
Unaweza saidia kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huu kwa kufanya yafuatayo:
* Osha mikono yako kwa sabuni na maji. Osha kwa muda wa sekunde 20, na kuwaosha watoto wadogo vivo hivo.
* Epuka kugusa macho, pua na mdomo kwa mikono kabla hujanawa baada ya kugusana na alie na mafua
* Kaa mbali na mtu alieugua ugonjwa huu. Watu waliougua ugonjwa huu wanaweza kueneza kutokana mgusano au ukaribiano
*
NINI CHA KUFANYA ILI UJISIKIE VIZURI
Hakuna matibabu sahihi ya baridi. Ili ujisikie vizuri unapaswa kupata muda mwingi wa kupumzika na unywe maji mengi.
Antibaotiki haziwezi kukupa nafuu kwasababu baridi na mafua husababishwa na virusi, hazifanyi kazi dhidi ya virusi wa koo la hewa.
-Epuka kutumia antibaotiki mara kwa mara km tiba ya baridi na mafua kwasababu antibaotiki hazifanyi kazi dhidi ya virusi bali hupelekea bakteria waliopo mwilini kuwa sugu