Wachumba Admin

Wachumba Admin Ili kuunganishwa na mchumba, uwe tu na ada ya kuunganishwa Tsh.10,000 ya Kitanzania(sawa na 600 hela ya KENYA).

Bonyeza hapo chini ya Profile yangu button imeandikwa "WhatsApp" uje Inbox kwangu. Tunatengeneza tabasamu kwa mioyo iliyoumizwa kimahusiano😊

Hisia za kuumiza zaidi katika dunia hii, ni kujua ulifanya yote kadri ulivyoweza; lakini kwao bado haikutosha.
10/09/2023

Hisia za kuumiza zaidi katika dunia hii, ni kujua ulifanya yote kadri ulivyoweza; lakini kwao bado haikutosha.

Kuna nyakati katik maisha, kitu bora zaidi unachoweza kufanya, ni kufunga mdomo wako, kisha kuacha macho wazi yatazame m...
24/05/2023

Kuna nyakati katik maisha, kitu bora zaidi unachoweza kufanya, ni kufunga mdomo wako, kisha kuacha macho wazi yatazame mambo yanavyoenda. Kukiwa na mchanganyiko wa Mafuta na Maji, hata vichanganywaje, mafuta yataonekana tu.

Usiumie saaana kwa kitu ambacho hapo mwanzo kiliwahi kukupa furaha. Ni mapito tu ya dunia; vumilia, yatakwisha. Ili siku...
23/03/2023

Usiumie saaana kwa kitu ambacho hapo mwanzo kiliwahi kukupa furaha. Ni mapito tu ya dunia; vumilia, yatakwisha. Ili siku ikamilike, lazima iwe na mchana, iwe na usiku pia. Na hakuna usiku usiokuwa na asubuhi yake. K**a unaumia sasa, saa yaja utatabasamu tena. Kwa sababu maumivu yapo pale kutuimairisha, na furaha ipo pale kutunenepesha; hivyo furahia kila sekunde ya maisha yako.

Kadri unavyoendelea kukua, kuna kipindi kutakuwa na nyakati za maumivu makali sana kuwahi kutokea katika maisha yako. La...
07/02/2023

Kadri unavyoendelea kukua, kuna kipindi kutakuwa na nyakati za maumivu makali sana kuwahi kutokea katika maisha yako. Lakini nyakati ngumu k**a hizo zijapo, ebu zikakufanye uwe imara zaidi, ukawe shupavu zaidi. Lia kadri unavyoweza, omboleza kadri unavyoweza, lakini baada ya hayo jitie nguvu, simama upya kisha endelea kusonga mbele. Usikubali kukata tamaa kirahisi; wacha kizazi chako kijacho nyuma yako kije kijifunze kuwa kuliwahi kuishi mtu shujaa katika ukoo wao.

Anapokuwa katika mahusiano mazuri, mwanamke sikuzote huonekana mwenye afya njema, asiye na stress, mwenye furaha muda wo...
31/01/2023

Anapokuwa katika mahusiano mazuri, mwanamke sikuzote huonekana mwenye afya njema, asiye na stress, mwenye furaha muda wote; na uwezekano wa kuishi miaka mingi zaidi huongezeka.

Sijui ni nani anataka kusikia hili. Lakini nikwambie tu mammy, ni kweli umeumizwa kimapenzi, lakini wewe ni wa thamani s...
06/01/2023

Sijui ni nani anataka kusikia hili. Lakini nikwambie tu mammy, ni kweli umeumizwa kimapenzi, lakini wewe ni wa thamani sana, unajidhalilisha kumlilia mtu asiyejua thamani yako. Mpenzi ebu tabasamu katikati ya majonzi yako, kisha chukua kioo, mtazame mwanamke mzuri anayeonekana mbele yako, tabasamu, pia mwanamke huyo nae atatabasamu. Kisha jiulize hivi yule kibushuti anastahili kweli kuliliwa machozi yako?😊

Mwanamke anapokuwa na jambo lililomuumiza moyoni, mara nyingi hupendelea kulisema kwa mtu wake wa karibu aneyemwamini; n...
25/12/2022

Mwanamke anapokuwa na jambo lililomuumiza moyoni, mara nyingi hupendelea kulisema kwa mtu wake wa karibu aneyemwamini; na k**a atasikilizwa kwa kujali wakati anasimulia yaloyomuumiza, taratibu hujisikia k**a ametua mzigo fulani moyoni.

Hakuna kitu kinavutia zaidi k**a kujitambua na kujiamini. Pindi tu unatakapojitambua na kuiona thamani yako, kila mtu at...
24/12/2022

Hakuna kitu kinavutia zaidi k**a kujitambua na kujiamini. Pindi tu unatakapojitambua na kuiona thamani yako, kila mtu ataiona na kuitambua pia.

Usimlaani wala kumlaumu Mwenyezi MUNGU kwanini ni wewe tu ndie unayepitia maisha ya, taabu, mateso, na njia ya miiba; wa...
18/12/2022

Usimlaani wala kumlaumu Mwenyezi MUNGU kwanini ni wewe tu ndie unayepitia maisha ya, taabu, mateso, na njia ya miiba; wakati huko maisha ya wengine ni raha na mtelezo. Usimlaumu Mungu, bali mshukuru kwa yote unayoyapitia, kwa sababu huwezi jua kuna tunu gani umewekewa mbeleni baada ya mateso hayo.

Machozi ya uchungu huwa sio yale yanayotoka machoni na kutililika mashavuni; bali ni yale yanayotoka moyoni na kutililik...
15/12/2022

Machozi ya uchungu huwa sio yale yanayotoka machoni na kutililika mashavuni; bali ni yale yanayotoka moyoni na kutililika nafsini. Kila mtu ana historia yake ya kuumiza iliyoacha makovu makubwa moyoni.

Address

Dodoma

Telephone

+255672427474

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wachumba Admin posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category