08/04/2024
*UMUHIMU WA KUTUMIA VIRUTUBISHO LISHE*
Viumbe wote hai huhitaji chakula ili kuishi. Chakula huwapa binadamu nguvu ili waweze kufanya shughuli zao za kila siku, huwawezesha kujenga na kuikarabati miili yao, na huwawezesha kupambana na maradhi mbalimbali. Ili mwili uweze kuyafanya yote hayo na kuwa na afya nzuri, inabidi upate chakula cha aina mbalimbali. Mada ya leo inahusu umuhimu wa virutubishi katika mwili wa binadamu ambapo tutavitaja virutubishi hivyo na kuelezea umuhimu wa kila kimoja.
Kirutubishi Cha Mwili Ni Nini?
Chakula tunachokula ndicho kinachoupatia mwili virutubishi au vitu vinavyotoa nguvu mwilini, kuusaidia mwili kukua, kupambana na maradhi n.k. Kusudi mwili upate virutubishi hivyo kutoka kwenye chakula tunachokula, chakula hicho lazima kivunjwevunjwe kwanza. Zoezi hilo linaanza kwa kukitafuna chakula mdomoni, kukimeza na kwisha kufika tumboni. Kikifika tumboni, chakula hicho huchanganyika na maji na vimimina vingine zikiwemo tindikali na kisha kitaelekea kwenye utumbo mdogo. Virutubishi hufyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu kupitia kuta za utumbo mdogo na kusambazwa mwilini. Mabaki yasiyofaa mwilini huelekea kwenye utumbo mpana na kisha kutoka nje ya mwili.
Kuna virutububishi muhimu sita ambavyo mwili unahitaji kupata tutoka kwenye chakula ili kuwa ana afya nzuri. Virutubishi hivi muhimu hugawanywa katika makundi makubwa mawili: micronutrients na macronutrients.
Micronutrients ni virutubishi ambavyo mwili wa mtu unahitaji kwa kiasi kidogo. Micronutrients ni pamoja na vitamini na madini.
Pamoja na ukweli kwamba mwili unahitaji virutubishi hivi kwa kiasi kidogo, ukosefu unaweza kusababisha maradhi.
Macronutrients ni virutubishi ambavyo mwili wa mtu unahitaji kwa kiasi kikubwa. Macronutrients ni pamoja na maji, protini, wanga na mafuta.
Kwa hiyo, kuna virutubishi sita ambavyo ni muhimu kwa afya ya mwili wa binadamu, navyo ni:
1. Protini
2. Wanga
3. Mafuta (fats)
4. Madini
5. Vitamini
6. Maji
Protini: Protini ni moja ya virutubishi vitatu vinavyohitajika kwa wingi katika mwili (macronutrients ), vingine vikiwa ni wanga na mafuta. Unapokula chakula chenye protini, huvunjwavunjwa na kuwa amino acids. Amino acids hutumika katika kujenga na kukarabati misuli ya mwili. Hii ni muhimu kwa watu wale ambao huwa na shughuli nzito au wanaofanya mazoezi. Sehemu zote za mwili zina misuli hivyo ni vizuri kupata chakula chenye protini ili kuirudishia kwenye hali yake. Protini vile vile husaidia katika kujenga kinga za mwili na afya ya ubongo. Vyanzo vikuu vya protini ni nyama, samaki, maziwa, siagi na mayai. Protini pia hupatikana kutokana na mimea; maharage, njegere zilizokaushwa, mbegu n.k.
Protini ni kirutubishi kinachotakiwa kwa wingi na mwili ambacho kinatakiwa na kila seli ya mwili ili kufanya kazi vizuri.
Protini hufanya kazi nyingi mwilini, ikiwa ni pamoja na:
kuhakikisha ukuaji wa misuli, mifupa, nywele, na ngozi kutengeneza kingamwili (antibodies), homoni, na vitu vingine vya muhimu kufanya kazi k**a chanzo cha fueli cha seli na tishu inapohitajika
Binadamu anaweza kuapata protini kupitia chakula. Chakula kifuatacho ni chanzo kizuri cha protini:
nyama nyekundu (tumia kwa kiasi kidogo na chagua nyama isiyo na mafuata) nyama ya kuku na batamzinga samaki na chakula kingine cha bahari maharage mayai bidhaa zitokanazo na wanyama soya njugu baadhi ya nafaka, pamoja na quinoa
Ingawa nyama na samaki ndicho chakula chenye protini kwa wingi zaidi, watu wasiokula nyama wanaweza kupata protini kutokana na bidhaa za mimea.
Wanga: Chakula cha wanga hukupa nguvu ili mwili uweze kufanya shughuli zake za kila siku vizuri. Glycogen ndani ya misuli ndicho kitu muhimu katika kukusaidia kuweka sawa kiwango cha nishati siku nzima. Chakula chenye wanga kikiliwa kongosho hutoa homoni iitwayo insulin. Insulin husaidia wanga uweze kuhifadhiwa kwenye misuli au k**a mafuta. Wanga uliohifadhiwa ndani ya mwili huitwa glycogen. Glycogen iliyohifadhiwa ndicho chanzo cha nishati katika mwili wako. Wanga hutokana na mahindi, ngano, shayiri, mchele na pia kutoka kwenye matunda na mboga.
Wanga hugawanywa katika makundi mawili: simple na complex. Wanga kutoka kwenye sukari ni simple carbohydrates na wanga kutoka kwenye nafaka ni complex carbohydrates. Wanga hutoa karibu kalori 4 kwa gramu na ndicho chanzo cha mwanzo cha nishati kwa misuli na ubongo.
Kabohaidreti ni ya lazima kwa mwili. Kabohaidreti ni sukari au wanga vinanavyotoa nishati kwa seli na tishu zote katika mwili.
Kuna aina mbili za kabohaidreti: simple na complex. Watu wanatakiwa kuwa waangalifu na matumizi ya simple carbohydrates, k**a mikate myeupe, pasta, na wali. Lakini , mwili unahitaji complex carbohydrates kwa ajili ya kusaidia katika shughuli zifuatazo:
mfumo wa kinga za mwili ufanyaji kazi wa ubongo mfumo wa neva nishati ili kufanya kazi mfumo wa mmengβenyo wa chakula
The Dietary Guilines for America wanashauri mtu apate asilimia 45-65 ya kalori zake kutokana na complex carbohydrates.
Chakula kifuatacho kina complex carbohydrates kwa wingi:
quinoa brown rice mboga za majani nafaka nzima (pasta, mkate, na vinginevyo vya kuokwa) oatmeal matunda shayiri.
Mafuta: Mafuta ni moja ya virutubishi vitatu vinavyohitajika kwa wingi na mwili, bila mafuta mwili hauwezi kuishi. Pamoja na kutoa kalori 9 kwa kila gramu, mafuta husaidia kuupa mwili joto wakati wa baridi. Mafuta pia hulainisha maungio ya mifupa. Mafuta hutunza baadhi ya vitamini k**a A, D, E na K. Chakula cha aina ya nyama na maziwa kina uwingi wa saturated fats na mboga zina kiwango kikubwa cha unsaturated fats. Mafuta hutoa kalori mara mbili ya protini. Mafuta hutunza afya ya ngozi na nywele.
Watu wengi wanahusisha chakula chenye mafuta mengi na afya mbaya. Ukweli ni kwamba mtu anahitaji aina fulani za mafuta ili kuwa na afya njema.
Mafuta huupa mwili nishati na kuasaidia baadhi ya shughuli. Lakini, inatakiwa kula mafuta yenye afya, k**a monounsaturated na polyunsaturated fats na kupunuguza au kukwepa kabisa saturated na trans fats.
Mafuta yenye afya yanasaidia katika kazi zifuatazo:
ukuaji wa seli kuganga kwa damu ujenzi wa seli mpya kuondoa hatari ya magonjwa ya moyo na kisukari miondoko ya misuli kuweka vizuri sukari katika damu tendaji kazi wa ubongo ufyonzaji wa vitamini na madini utengenezaji wa homoni utendaji kazi wa kinga za mwili
Mtu anaweza kupata mafuta yenye afya kutokana na:
njugu samaki, k**a samoni na tuna mboga za majani mbegu.
Vitamini
Vitamini ni virutubishi vinavyohitajika kwa kiwango kidogo na mwili na hutoa faida nyingi za kiafya, ikiwa ni pamoja na:
kuimarisha kinga za mwili kusaidia kuzuia au kupunguza kansa za aina fulani, k**a saratani ya tezi dume kuimarisha mifupa na meno kusaidia ufyonzwaji wa calcium kutunza afya ya ngozi kusidia mwili kuvunja na kujenga protini na wanga kutunza afya ya damu kusaidia utendaji wa ubongo na neva.
Kuna vitamini muhimu 13 ambazo wataalamu wa lishe huzigawanya katika makundi mawili: zinazoyeyuka katika mafuta na zile zinazoyeyuka katika maji.
Vitamini Zinazoyeyuka Katika mafuta ni :
Vitamini A Vitamini D Vitamini E Vitamini K.
Vitamini Zinazoyeyuka Katika Maji ni:
Vitamini B-1 (thiamine) Vitamini B-12 (cyanocobalamin) Vitamini B-6 Vitamini B-2 (riboflavin) Vitamini B-5 (pantothenic acid) Vitamini B-3 (niacin) Vitamini B-9 (folate, folic acid) Vitamini B-7 (biotin) Vitamini C
Kwa kawaida, mtu anayekula chaukula chenye uwingi wa mboga za majani, matunda, na minofu isiyokuwa na mafuta, anaweza kuapata vitamini zote anazozihitaji kutoa kwenye chakula chake. Lakini wale wanaokula matunda na mboga za majani kidogo, na wale wenye matatizo ya kiufyonzaji kwenye matumbo yao, wanahitaji kupata supplements za vitamini ili wasipatwe na tatizo la upungufu wa vitamini.
Madini
Madini ni kirutubishi kingine cha mwili kinachotakiwa kwa kiwango kidogo (micronutrient). Kuna makundi mawili ya madini: major na trace minerals. Mwili unahitaji madini kutoka makundi yote ili kuwa na afya nzuri.
Major minerals ni pamoja na:
magnesium calcium phosphorus sulfur sodium potassium chloride
Major minerals husaidia mwili katika:
kuweka vizuri viwango vya maji kutunza afya ya ngozi, nywele, na kucha kuboresha afya ya mifupa
Trace minerals ni pamoja na:
chuma selenium zinc manganese chromium copper iodine fluoride molybdenum
Trace minerals husaidia katika:
kuimarisha mifupa kuzuia kuoza kwa meno kusaidia kuganda kwa damu kusaidia kusafirisha oksijeni kusiadia kinga za mwili kusaidia kuweka sawa pressure ya mwili
Mtu anaweza kujihakikishia kupata madini ya kutosha kwa kula chakula cha aina ifuatayo:
nyama nyekundu (kula kiasi na chagua nyama isiyo na mafuta) chakula cha bahari chumvi (iodized table salt) maziwa na bidhaa nyingine za maziwa njugu na mbegu mboga za majani matunda kuku mkate na nafaka kiini cha yai nafaka nzima maharage na njegere.
Vitamini Na Madini: Vitamini na madini ni muhimu kwa miili yetu kwani huusaidia mwili kufanya kazi zake vizuri na kuongeza kasi ya ufanyaji kazi wa kemikali ndani ya mwili. Madini ya calcium na magnesium ni muhimu kwa mifupa yetu na chuma (iron) kinahitajika katika chembechembe nyekundu za damu ili kusafirisha oksijeni.
Kuna vitamini 13, ikiwa ni pamoja na vitamin A,B complex, C, D, E na F. Kwa sababu vitamini nyingi hazitengenezwi na miili yetu, zinatakiwa zipatikane kutoka kwenye chakula.
Pamoja na kwamba ni vitu muhimu, vitamini na madini huhitajika kwa kiwango kidogo. Vitamini na madini hupatikana katika chakula tunachokula, lakini kwa kawaida mahitaji ya mwili ya vitamini na madini ili uwe na afya huwa ni makubwa kuliko kiwango kinachopatikana kwa kula chakula.
Maji
Maji hujenga asilimia 65 ya mwili wa binadamu. Ni lazima mwili uwe na maji ili mwanadamu aweze kuishi. Maji yana kazi ya kusafirisha virutubishi kwenda kwenye seli na kutoa vitu visivyohitajika kutoka kwenye seli. Inashauriwa mtu anywe glasi 8 za vimiminika kwa siku. Wakati wa kufanya mazoezi, maji hufanya kazi ya kuupoza mwili.
Maji ni dhahiri ndicho kirutubishi muhimu zaidi kinachohitajika na binadamu. Mtu anaweza kuishi siku chache sana bila maji. Hata upungufu wa maji kidogo tu unaweza kuleta maumivu ya kichwa na kuzorota kwa utendaji kazi wa mwili na akili.
Mwili wa binadamu unajengwa kwa kiasi kikubwa na maji, na kila seli inahitaji maji ili kufanya kazi. Maji yanasaidia katika shughuli kadhaa za mwili, zikiwa ni pamoja na:
kutoa sumu nje ya mwili kuzuia mishtuko (shock absorption) kusafirisha virutubishi kuzuia kufunga choo kulainisha kuupa mwili maji
Chanzo kizuri cha maji ni kunywa maji asilia, ambayo hayajaongezewa utamu kutoka kwenye bomba au yaliyosindikwa kwenye chupa. Watu wasiopenda ladha ya maji wanaweza kukamulia limau au tunda lo lote la aina ya machungwa (citrus fruit).
Mtu anaweza kupata maji ya ziada kwa kula matunda yenye maji mengi.
Inashauriwa kukwepa kupata maji kutoka kwenye vinywaji vyenye sukari. Vinywaji vyenye sukari ni k**a chai iliyoungwa sukari, kahawa, soda, lemonade na juisi za matunda.
Mlo Kamili (Balanced Diet)
Mlo kamili (balanced diet) ni mlo ulio na virutubishi vinavyohitajika na mwili ili uweze kufanya kazi ipasavyo. Ili kupata virutubishi vinavyotakiwa kutoka kwenye mlo, unahitaji upate kalori nyingi kutoka:
kwenye matunda mboga nafaka nzima jamii ya kunde njugu nyama isiyo na mafuta
Kalori Ni Nini?
Kiwango cha kalori katika chakula ni kipimo cha nishati iliyohifadhiwa ndani yake. Mwili hutumia kalori kutoka katika chakula ili kukuwezesha kutembea, kufikiri, kupumua, na kufanya shughuli nyingine muhimu. Mtu wa kawaida anahitaji kiasi cha kalori 2,000 kila siku ili kuwa na uzito wa kawaida.
Lakini kiwango cha kalori kwa siku kwa mtu kinatofautiana kulingana na umri, jinsia, na uzito wa kazi zake. Kwa kawaida, wanaume huhitaji kalori nyingi kuliko wanawake, na watu wa mazoezi huhitaji kalori nyingi kuliko wale wasiofanya mazoezi.
Chanzo cha kalori katika mlo wako ni muhimu k**a kilivyo kiwango cha kalaori. Inashauriwa kupunguza matumizi ya kalori tupu (empty calories), au zile ambazo hazina au zenye thamani ndogo ndogo ya lishe. Kalori tupu ni zile zinazotokana na sukari na mafuta ya kuganda, k**a siagi.