10/10/2025
Wewe mwenye kisukari ni Tabibu wa kwanza wa tatizo lako.
Kuna taarifa nyingi mitaani na kwenye mtandao ila ni jukumu lako wewe kujua ni taarifa gani sahihi na inayokufaa.
Unaweza kuambiwa kula aina hii ya chakula, usile aina ile ya chakula,acha kabisa kula aina hii ya chakula,kula sana aina ile ya chakula, mara kula sana aina hii ya matunda,usile aina ile ya matunda.
Kwa mfano, wengi wanaambiwa wale ndizi changa kwa wingi,labda na ugali wa uwele,dona au ulezi kwa wingi.
Sasa vipi k**a umeenda sehemu ambapo hakuna ndizi changa,hakuna dona,ulezi au uwele, unataka kusema hautakula chakula?
Utashinda na njaa? La Hasha, utakula tu, mwenye kisukari anakula aina zote za chakula, iwe wali,ndizi za kupika,pilau,biryani,viazi vya aina yote, maboga,sembe,dona n.k, cha msingi ni kujua ni jinsi gani au kwa utaratibu gani unaweza kula vyakula hivyo.
Tusipikiwe au tusitengewe chakula tofauti na cha familia, hapana, tunakosea sana, chakula cha familia ndio na wewe mwenye ugonjwa wa kisukari unaweza kula chakula hicho hicho, hakuna chakula maalum cha mtu mwenye kisukari,isipokuwa tu wewe mwenyewe ni lazima ufahamu ni jinsi gani unatakiwa ule au ni kwa utaratibu gani unatakiwa ule, ndio maana ninasema wewe mwenye kisukari ndiyo tabibu wa kwanza wa kisukari.
Mimi nitakushauri,mpishi atapika tu na chakula kitawekwa mizani, ila wewe ndiyo utajua jinsi ya kula.
Wewe ni Tabibu wa kwanza wa kisukari chako.
Leo nina package maalum kwa ajili yako wewe mwenye changamoto ya Kisukari,tuma neno INSULIN kwenda 0746 334 963