
25/08/2025
Wengi Wanatembea Na Kisukari bila kujua na huenda ni wewe, au mtu wa karibu yako.
Na mbaya zaidi, kila kona ya dunia, Vijijini hadi mijini watu wanazidi kuathirika na ugonjwa huu kimya kimya k**a moto unaotafuna ndani bila moshi.
Leo nakupa ukweli mzito kuhusu ugonjwa huu wa kimya kimya lakini ni hatari.
Unakunywa Maji Lakini Kiu Haiishi?
Au unakula kila saa lakini bado una njaa isiyoisha?
Unachoka sana, hata bila kufanya kazi ngumu?
K**a jibu ni "NDIYO" Sikiliza kwa makini, Hizi ni dalili za awali kabisa za Kisukari, USIPUUZE
Ugonjwa unaohusiana na kushindwa kwa mwili kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
Sasa hebu twende polepole Kisukari Huanzia Wapi?
Kuna aina kuu mbili 2 (Na nusu ½) za kisukari, na zote zina tabia Tofauti Tofauti.
Tuzione hapa...
1. Type 1– Kisukari cha kurithi au cha utotoni
Hiki hutokea pale ambapo kongosho lako linashambuliwa na kinga ya mwili wako...
Matokeo yake?
Mwili kukosa kabisa uwezo wa kutengeneza Insulin, homoni inayosaidia kiwangi sahihi cha sukari kuingia ndani ya seli zako.
Kwa kifupi Sukari inazunguka kwenye damu, Lakini haiingii sehemu inayotakiwa.
2. Type 2 – Kisukari cha mtindo wa maisha.
Aina hii ya kisukari kuhua kwa kasi na kuongoza duniani kwasasa husababishwa na
Kula ovyo (vyakula vya haraka, sukari, mafuta...)
Kukosa mazoezi
Uzito kupita kiasi
Msongo wa mawazo
Na hata watoto siku hizi wanakipata kwa sababu ya kula chipsi, kunywa soda, Mitindo mibovu na malezi mabovu
3. Gestational Diabetes (Kisukari cha Mimba)
Kinatokea wakati wa ujauzito, mara nyingi hutoweka baada ya kujifungua Lakini kuna uwezekano wa kupata Type 2 baadaye.
Unataka kujua k**a kisukari kimeanza kukutembelea?
Basi chunguza mwili wako kwa makini kupitia dalili hizi.
Kukojoa mara kwa mara, hasa usiku
Kiu ya ajabu, unakunywa maji lakini haikati..
Njaa isiyoeleweka
Uchovu wa mara kwa mara
Kupungua uzito bila sababu
Vidonda visivyopona..
Miwasho isiyoisha sehemu za siri au ngozi
Ukipuuza dalili hizi, unakipa kisukari nafasi ya kujenga makazi mwilini mwako.
Sasa Swali Ni Hili, UNAWEZA KUJIKINGA na Kisukari?
Ndiyo unaweza kujikinga, hataka k**a kwenye familia yako kuna mgonjwa wa kisukari.
Kisukari Type 2 kinaweza kuzuilika, na hata kudhibitiwa kikamilifu.Lakini ni lazima ubadili maisha, Sio kwa magumashi, bali kwa maarifa sahihi.
Hebu fuata haya...
Kula kwa akili, sio kwa njaa, Mboga za majani kila siku, Matunda kwa kiasi, si ya sukari nyingi, Nafaka zisizokobolewa, Punguza mafuta mabaya na sukari ya viwandani
Anza kujutuma, mwili wako haukuzaliwa ubweteke, Tembea dakika 30 kila siku, Panda ngazi badala ya lifti, Fanya mazoezi unayoyapenda k**a jogging, hata kazi ngumu k**a kulima...
Punguza uzito, Mzigo mkubwa wa mwili ni mzigo wa kongosho pia...
Tuliza akili yako, Msongo wa mawazo ni mwuaji wa kisasa Unaharibu homoni zako...
Pima sukari mara kwa mara, Huwezi kutibu kile usichokijua, Tumia glucometer nyumbani au pima hospitali...
Ukizembea...Madhara Yake Hayana Huruma.. Kisukari hakisamehi, na hakijali una miaka mingapi.
Madhara yake ni k**a mlango wa majanga, Ukiingia utakumbana na....
Kiharusi na Presha kali
Upofu
Figo kushindwa kufanya kazi (ESRF)
Vidonda visivyopona hadi kukatwa mguu..
Kukosa nguvu za kiume au matatizo ya uzazi
Swali ni je Kisukari Kinatibika?
Wengi wanaona jibu la kwamba Hakiponi lakini wanasahau kuwa kutibu Kisukari kunaanza na Kudhibiti chanzo Na chanzo kinadhibitika vizuri, Na hilo linaweza kuleta maisha marefu, yenye afya na furaha...
Kwa Type 1:
Sindano za insulin kila siku, bila kuruka dozi
Kwa Type 2:
Badili maisha k**a nilivyoeleza
Dawa za kisukari kwa ushauri wa daktari
Ufuatiliaji wa sukari mara kwa mara..
Usikubali Kuishi Bila Kujua hali yako ya kiafya, Wengine wanakufa kwa ugonjwa, wengine kwa kutojua...
Nimekuambia yote haya kwa sababu nakujali, Na najua unaweza kubadili hali yako leo au kusaidia ndugu, rafiki, au mzazi aliyeko hatarini..