23/07/2025
WATANZANIA wengi wana uzito uliopitiliza (mabonge) kutokana na kutozingatia ulaji unaofaa huku takwimu zikionyesha ni watu saba pekee nchini katika 100 wanaozingatia mlo kamili.
Takwimu Aidha, Mtanzania mmoja katika watatu, ana uzito uliokithiri na watu wenye elimu na uhakika wa kipato ndio waathirika zaidi.
Katika maeneo machache ambayo tunafanya vizuri ni kwenye mazoezi kwa sababu kumekuwa kwa mfano na marathoni nyingi.
Hatufanyi vizuri kabisa katika masuala ya ulaji bado ni watu saba katika 100 ambao wanazingatia ulaji unaofaa.
Suala la uzito na unene kupita kiasi pia hali imezidi kuwa mbaya, zamani ilikuwa ni katika kila watu wanne, mmoja ana uzito uliokithiri, sasa hivi ni mtu mmoja katika kila watu watatu ana uzito au unene uliokithiri, kwa hiyo hatufanyi vizuri katika eneo hili.
Bahati mbaya kuliko zote vijana ndio wanaathirika zaidi kuliko rika lingine lolote na wanawake wanaathirika zaidi kuliko wanaume na watu wenye umri mdogo na wanawake ndio wako kwenye hatari zaidi.
Utafiti unaonesha kwamba magonjwa yasiyoambukiza k**a saratani, kisukari, figo na shinikizo la juu la damu, yanaathiri zaidi watu wenye kipato cha chini, lakini ni kinyume chake katika baadhi ya nchi k**a Tanzania ambako waathirika wakubwa ni wasomi na wenye uhakika wa kipato.
Katika jamii mfano za wafanyakazi ndio wanaotumia vyakula vya viwandani zaidi, pombe zaidi, ndio watu wenye fursa ya kununua soda na vitu vingine ambavyo vinaathiri afya,wanaathirika zaidi kutokana na mtindo wa maisha kwa kuwa hawana nafasi ya kupata chakula bora kwa kuwa wananunua vyakula wasivyojua namna vilivyoandaliwa na pia hawapati nafasi ya kufanya mazoezi.
Hali hii hupelekea ghrama kubwa kwenye vitu vikubwa vinavyouelemea mwili ikiwemo kutibu magonjwa k**a saratani, matatizo ya figo, shinikizo la juu la damu, kiharusi na kisukari.
Jitahidi upate muda wa kufanya mazoezi na upate mlo kamili unaopaswa kuzingatiwa kila siku na aina yake kwenye mabano ni wanga (ugali, wali au ndizi), mboga (kabichi, spinachi, mchicha au figiri) protini (nyama, samaki, kunde, njegere na maharage), matunda (embe, chungwa, papai au tikiti), vitamini (karanga au korosho) na maji ya kutosha