Good Samaritan Cancer Hospital - Ifakara

  • Home
  • Good Samaritan Cancer Hospital - Ifakara

Good Samaritan Cancer Hospital - Ifakara Good Samaritan Cancer Hospital is a non-profit private health care institution owned by Missionaries of Compassion under Catholic Diocese of Ifakara.

We provide comprehensive investigations and treatment of all pre-malignant lesions and solid cancers.

Kambi ya Madaktari Bingwa wa Samia Outreach kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kushirikiana na Good Samaritan ...
14/07/2025

Kambi ya Madaktari Bingwa wa Samia Outreach kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kushirikiana na Good Samaritan Cancer Hospital (GSCH) watafanya kampeni ya utoaji wa elimu ya saratani pamoja na uchunguzi wa saratani ya Mlango wa kizazi, saratani ya Tezi dume na saratani ya Matiti bila malipo.

Walengwa:
👉🏼Wanaume wote wa miaka zaidi ya 40.

👉🏼Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 25.

Zoezi hili litafanyika Hospitali ya Good Samaritan Cancer Hospital iliyopo Mashimoni-Ifakara Tarehe 17/07/2025 hadi tarehe 19/07/2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Wote mnakaribishwa

Good Samaritan Cancer Hospital-Ifakara tunawatakia watu wote Sabasaba njema yenye Heri na Fanaka.
07/07/2025

Good Samaritan Cancer Hospital-Ifakara tunawatakia watu wote Sabasaba njema yenye Heri na Fanaka.

Naibu Katibu Mkuu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia (Prof. Daniel E.Mushi) Atembelea Good Samaritan Cancer Hospital...
28/06/2025

Naibu Katibu Mkuu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia
(Prof. Daniel E.Mushi) Atembelea Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA na kujionea uwekezaji mkubwa wa Machine za Kisasa za Kutibu Saratani kwa Teknolojia ya hali ya juu ya IMRT

Mwakilishi wa Good Samaritan Cancer Hospital (GSCH)-IFAKARA MOROGORO katika Kongamano la Kitaifa la Madaktari , AICC ARU...
25/06/2025

Mwakilishi wa Good Samaritan Cancer Hospital (GSCH)-IFAKARA MOROGORO katika Kongamano la Kitaifa la Madaktari , AICC ARUSHA TANZANIA lililoandaliwa na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kuadhimisha Miaka 60, wakati wa UWASILISHAJI WA BANGO JUU ATHARI ZA MPANGO WA FEDHA WA HUDUMA ZA AFYA NA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA SARATANI KATIKA HOSPITAL YA GSCH, JUNI 19 2025

Mtaalamu wa Mionzi Tiba(Mr. Egdi Mlwilo) kutoka Good Samaritan Cancer Hospital IFAKARA, ahudhuria IAEA,Nchini Kongo Braz...
19/06/2025

Mtaalamu wa Mionzi Tiba(Mr. Egdi Mlwilo) kutoka Good Samaritan Cancer Hospital IFAKARA, ahudhuria IAEA,Nchini Kongo Brazzavile, kwenye mafunzo ya Kanda ya Afrika ya kuimarisha utamaduni wa usalama wa Mionzi katika Tiba, kuanzia tarehe 9 hadi 14 Juni 2025.

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA tumeshiriki siku ya Wachangia Damu Duniani kwa kufanya kampeni ya uchangiaji damu...
18/06/2025

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA tumeshiriki siku ya Wachangia Damu Duniani kwa kufanya kampeni ya uchangiaji damu katika eneo la Sokoni Ifakara. Tunatoa shukrani kwa wote waliojitokeza kuchangia Damu kuokoa maisha .Ni ukweli usiopingika kuwa uhitaji wa Damu ni mkubwa hivyo tunazidi kuwakaribisha Hospitalini watu wote wenye mapenzi mema ya kuchangia Damu kwa ajili ya ndugu na jamaa wanaopatwa na uhitaji huo

Good Samaritan Cancer Hospital kuelekea kilele cha Wachangia Damu Duniani ,tunapenda kuwakaribisha watu wote wanaopenda ...
13/06/2025

Good Samaritan Cancer Hospital kuelekea kilele cha Wachangia Damu Duniani ,tunapenda kuwakaribisha watu wote wanaopenda kuchangia damu ili kuokoa Maisha ya ndugu na jamaa wanaopatwa na uhitaji wa damu wawapo Hospitalini.
Tutapatikana Ifakara Sokoni kwa siku ya Jumamosi Juni 14,2025.

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA tunawatakia Waislamu wote Duniani Eid Al-Adha Njema ,ikawe ya furaha ,amani  na m...
07/06/2025

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA tunawatakia Waislamu wote Duniani Eid Al-Adha Njema ,ikawe ya furaha ,amani na mafanikio.

Good Samaritan Cancer Hospital yafanya Warsha(Workshop) ya Kuandaa Mpango Mkakati wa Hospitali (5 years strategic plan)M...
28/05/2025

Good Samaritan Cancer Hospital yafanya Warsha(Workshop) ya Kuandaa Mpango Mkakati wa Hospitali (5 years strategic plan)
Mpango Mkakati huo ni kwa ajili ya kuboresha matibabu ya Saratani katika jamii ya Kitanzania. Warsha hii imefanyika kwa ushirikiano na Mtaalamu wa Ushauri kutoka Chuo Kikuu cha Afya St. Francis, ikiongozwa na Mkuu wa Chuo, Prof. Albin Kalolo, na timu yake ya wataalamu.
Washiriki wa warsha kwa upande wa Good Samaritan Cancer Hospital waliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji ,Rev. Fr. Shibin James, pamoja na timu ya wakuu wa idara na vitengo, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Tiba, Dkt. Rosemary Mushi. Lengo kuu la warsha hii ni kuandaa mpango mkakati wa Miaka 5 ijayo, utakaowezesha Hospitali kutoa huduma bora na za kisasa kwa jamii ya Kitanzania, pia kuhakikisha upatikanaji wa matibabu ya Saratani unaboreshwa na kutolewa kwa Ufanisi wa Hali ya juu.

Wauguzi wa Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA  Waadhimisha siku ya Wauguzi Duniani.Katika Maadhimisho hayo ,Wauguzi ...
24/05/2025

Wauguzi wa Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA Waadhimisha siku ya Wauguzi Duniani.Katika Maadhimisho hayo ,Wauguzi waligawa zawadi mbalimbali kwa Wagonjwa ikiwa ni kuonesha namna wanavyowajali.

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA tunaendelea kuelimisha Wagonjwa ,na umma kwa ujumla juu ya suala zima la nafasi y...
22/05/2025

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA tunaendelea kuelimisha Wagonjwa ,na umma kwa ujumla juu ya suala zima la nafasi ya LIshe bora katika kuimarisha Afya .Kwa Ufafanuzi wa kina juu masuala ya Lishe Karibu Uonane na Mtaalamu wetu wa Lishe (Nutritionist).

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA kwa kutambua Umuhimu na nafasi ya Lishe Bora katika kuimarisha Afya kwa Wagonjwa ...
15/05/2025

Good Samaritan Cancer Hospital-IFAKARA kwa kutambua Umuhimu na nafasi ya Lishe Bora katika kuimarisha Afya kwa Wagonjwa , inakuletea mfululizo wa Elimu Lishe . Endelea kufuatilia, na izingatiwe kuwa Lishe bora siyo kwa wagonjwa tu ,bali ni kwa watu wote

Address


Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00
Saturday 08:00 - 13:00

Telephone

+255683617545

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Good Samaritan Cancer Hospital - Ifakara posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram