29/03/2026
πΈ AFYA YAKO NI MUHIMU! USIPUUZE DALILI HIZI πΈ
π΄ 1. UTI (Maambukizi ya njia ya mkojo)
Dalili zake kuu:
@ Maumivu au kuwaka moto wakati wa kukojoa
@ Kukojoa mara kwa mara (hata kidogo kidogo)
@ Mkojo kuwa na harufu kali au rangi isiyo ya kawaida
@ Maumivu chini ya tumbo
@ Wakati mwingine homa (ikiwa imezidi)
π Hii inaathiri zaidi njia ya mkojo.
βͺ 2. FANGASI (Maambukizi ya uke - yeast infection)
Dalili zake kuu:
@ Kuwashwa sana ukeni
@ Ute mzito mweupe k**a maziwa yaliyoganda
@ Harufu si kali sana (tofauti na UTI au PID)
@ Maumivu au muwasho wakati wa tendo la ndoa
@ Uke kuwa na muwasho au kuvimba
π Hii inaathiri zaidi uke (vaginal area).
π£ 3. PID (Pelvic Inflammatory Disease)
Dalili zake kuu:
@ Maumivu makali ya tumbo la chini au nyonga
@ Ute usio wa kawaida wenye harufu mbaya
@ Maumivu wakati wa tendo la ndoa
@ Kutokwa damu isiyo ya kawaida (nje ya hedhi)
@ Uchovu au mwili kulegea
π Hii ni hatari zaidi β huathiri viungo vya uzazi (mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi).