24/10/2023
Kusimikwa kwa viongozi wa Hospitali ya Nyakahanga. Tarehe 22/10/2023 ilikuwa siku ya furaha na tulivu, siku muhimu na ya kumbukumbu kwani Viongozi wawili Dr Furaha Kahindo - Mganga Mkuu na Mr Justine Kataraia - Muuguzi MKuu walisimikwa rasmi na Baba Askofu Benson Bagonza Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Dayosisi ya Karagwe kuongoza Hospitali kwa kipindi hiki.
Akisoma Hati ya Dayosisi ya karagwe kwa ajili ya viongozi wateule wa Hospitali ambao ni Dr Furaha Mganga Mkuu na Justine Kataraia Muuguzi Mkuu, Katibu mkuu wa Dayosisi Mch Jeremiah M Rugimbana alisema, kwa mujibu wa katiba ya Dayosisi ya Karagwe, ukurasa wa 27, kifungu cha 1.14.2.i kuna kazi za Halmashauri kuu. Halmashauri kuu ya Dayosisi ya Karagwe namba 142 iliyofanyika Karagwe Hoteli kayanga tarehe 7/6/2023, katika agenda yake namba HK/142/9 ilimchagua Dr Furaha Darlene aliyekuwa akikaimu nafasi ya Mganga Mkuu kuwa Mganga mkuu kamili. Aidha Manejimenti ya Dayosisi ya Karagwe kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya KKKT Dayosisi ya karagwe ilimteua Bwana Justine Kataraia kuwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Nyakahanga kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Kwenye nafasi hiyo ya Uongozi.
Hivyo baada ya kusomwa kwa hati hiyo Baba Askofu aliwasimika viongozi hao kila mmoja kwa nafasi yake. Mhesh Baba Askofu waombea kwa Mungu wa Mbinguni asiwapungukie wanapoamka, wanapoingi na kutoka na kuwatakia mafanikio katika wajibu huu mpya. Aidha aliwakumbusha kwamba kuwa kiongozi kuna garama zake, na nyingi ni chungu sana. Aliendelea kusema kuwa ukiwa kuongozi unapoteza uhuru wako binafsi,hutavaa k**a unavyopenda, hutakunywa k**a unavyopenda, hutakula popote unavyopenda, hutaenda popote k**a unavyopenda, utajichunga badala ya kuchungwa, utasengenywa lakini wewe huma haki ya kusengenya wengine, utalalamikiwa lakini wewe huna haki wala mahali pa kulalamika, waliochini yako wana haki ya kuonywa lakini wewe huna hiyo haki maana kosa moja unaondoka.