Afya360

Afya360 Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Afya360, Medical and health, Mkoani B, Kibaha.

We Wish You Wellđź’Ş
31/12/2025

We Wish You Wellđź’Ş

MWENDELEZO8. Maambukizi ya Ngozi, Upele (Diaper rash, eczema, heat rash)Chanzo:>>Ngozi kukaa na unyevu (diaper rash)>>Jo...
31/12/2025

MWENDELEZO

8. Maambukizi ya Ngozi, Upele (Diaper rash, eczema, heat rash)

Chanzo:
>>Ngozi kukaa na unyevu (diaper rash)
>>Joto kali (heat rash)
>>Mzio kwa sabuni, mafuta au chakula
>>Fangasi

Tahadhari:
>>Badilisha nepi mara kwa mara
>>Tumia mafuta ya asili k**a petroleum jelly
>>Usitumie sabuni zenye kemikali kali
>>Muone mtaalam wa afya

9. Malaria

Chanzo:
>>Mbu wa Anopheles jike

Dalili:
>>Homa ya kupanda na kushuka
>>Kutapika, kukosa hamu ya kula
>>Uchovu
>>Kukosa hamu ya kula

Tahadhari:
>>Mtumie chandarua chenye dawa
>>Safisha mazingira na kuondoa mazalia ya mbu
>>Tibu haraka mara tu dalili zinapoanza

10. Utapiamlo (Malnutrition)

Chanzo:
>>Lishe duni, kutopata maziwa ya mama vya kutosha, au vyakula visivyo na virutubishi vya kutosha

Dalili:
>>Kudumaa kwa ukuaji
>>Ngozi kavu, nywele kukatika
>>Kulegea kwa mwili

Tahadhari:
>>Lishe bora (maziwa ya mama miezi 0–6, kisha vyakula vya nyongeza vilivyo kamili)
>>Ufuatiliaji wa uzito wa mtoto kila mwezi

11. Magonjwa ya kinywa (oral thrush, maumivu ya fizi)

Chanzo:
>>Fangasi (hasa Candida albicans)

Dalili:
>>Madoa meupe kwenye ulimi
>>Kukataa kunyonya

Tahadhari:
>>Safisha midomo ya mtoto kwa kitambaa safi cha mvua baada ya kunyonyeshwa
>>Daktari anaweza kupendekeza dawa za kuua fangasi

12. Upungufu wa damu (Anemia)

Chanzo:
>>Lishe duni (ukosefu wa chuma/iron). Ukosefu wa madini ya chuma.

Dalili:
>>Ngozi na midomo kuwa meupe
>>Mtoto kuchoka haraka

Tahadhari:
>>Ongeza vyakula vyenye madini chuma (mayai, maini, mboga za kijani, uji wa lishe)

13. Dehydration (Upungufu wa maji mwilini)

Hii ni hali ya hatari inayotokana na kuharisha, kutapika au homa kali.

Dalili:
>>Midomo mikavu
>>Macho kuingia ndani
>>Kukojoa kidogo sana

Tahadhari:
>>Tumia ORS mara moja
>>Mpeleke hospitali haraka

14. Magongwa yanayozuilika kwa chanjo

Watoto wengi hupata magonjwa haya ikiwa hawajachanjwa:

Surua (Measles)
Kifaduro (Pertussis)
Dondakoo (Diphtheria)
Polio
Kifua kikuu (TB)
Hepat**is B

Tahadhari:
>>Hakikisha mtoto anafuata ratiba ya chanjo ya Taifa (Immunization Schedule).

Ratiba Fupi ya Chanjo Muhimu (Tanzania)

• Kwanza kuzaliwa: BCG, Polio ya kwanza, Hepat**is B

• Wiki 6: DPT, PCV, Polio, Rotavirus

• Wiki 10: DPT, Polio, Rotavirus

• Wiki 14: DPT, PCV, Polio

• Miezi 9: MR (Surua-Rubella)

• Miezi 18: MR dozi ya pili

ZINGATIA

>>Maziwa ya mama kwa miezi 6 ya mwanzo

>>Lishe kamili kuanzia miezi 6

>>Chanjo kamili kwa wakati

>>Usafi wa mikono, vyombo na mazingira

>>Ufuatiliaji wa afya kila mwezi

We wish You🥰
25/12/2025

We wish You🥰

MAGONJWA YANAUOWASUMBUA WATOTO WA MIEZI 0–24 (CHINI YA MIAKA 2)1. Homa ya kawaida (Common Cold)Chanzo: Virusi (hasa rhin...
21/12/2025

MAGONJWA YANAUOWASUMBUA WATOTO WA MIEZI 0–24 (CHINI YA MIAKA 2)

1. Homa ya kawaida (Common Cold)

Chanzo:
Virusi (hasa rhinovirus au RSV)

Dalili:
>>Mafua au pua kutoa k**asi
>>Kukohoa
>>Homa ya wastani
>>Kukosa usingizi au hamu ya kula

Hatari: Ikiwa haitadhibitiwa, inaweza kusababisha maambukizi ya mapafu (pneumonia).

Tahadhari:
>>Mpe maji au maziwa ya kutosha
>>Epuka kumkaribia mtoto ukiwamazingira
>>Epuka kumpa dawa bila ushauri wa daktari
>>Dumisha usafi wa mikono na mazingira
>>Tumia matone ya chumvi (saline drops) kupunguza pua kuziba.

2. Maambukizi ya Kifua / Mapafu (Pneumonia)

Chanzo:
Bakteria (Streptococcus pneumoniae au virusi (RSV)

Dalili:
>>Kupumua haraka / kifua kubana
>>Sauti k**a filimbi unapopumua
>>Homa kali
>>Kukosa hamu ya kula

Hatari: Hii ni moja ya magonjwa yanayoua watoto wengi chini ya miaka 2.

Tahadhari:
>>Chanjo ya PCV na Hib (H. influenzae)
>>Maziwa ya mama husaidia kinga
>>Usimfunike mtoto kupita kiasi (inaweza kuzuia upumuaji vizuri)
>>>Wahi hospitali mara moja ukiona dalili hizi

3. Kuharisha (Diarrhea)

Chanzo:
Maambukizi (hasa Rotavirus), maji machafu au chupa chafu

Dalili:
>>Kinyesi chepesi mara nyingi
>>Mtoto kuwa legevu, midomo mikavu, macho kuingia ndani.

Tahadhari:
>>Chanjo ya Rotavirus
>>Maziwa ya mama pekee hadi miezi 6
>>Mpe ORS
>>Safisha mikono kabla ya kumlisha

4. Maambukizi ya njia ya hewa ya juu (URTI)

Chanzo:
Virusi k**a influenza au RSV

Dalili:
>>Kukohoa
>>Mafua
>>Homa ya kawaida

Tahadhari:
>>Tumia mvuke wa maji moto kusaidia kupumua
>>Epuka moshi wa sigara na vumbi

5. Maambukizi ya sikio (Ot**is media)

Chanzo:
>>Bakteria
>>Mara nyingi baada ya mafua

Dalili:
>>Mtoto kushika sikio au kulia sana
>>Homa
>>Kutoa usaha kwenye sikio

Tahadhari:
>>Usitumie dawa ya sikio bila ushauri wa daktari
>>Tibu mafua kwa wakati
>>Epuka moshi na vumbi

6. Homa ya Njano ya Watoto Wachanga (Neonatal Jaundice)

Chanzo:
Ini bado halijakomaa vizuri

Dalili:
Ngozi na macho kuwa ya njano

Tahadhari:
>>Weka mtoto apate mwanga wa jua asubuhi kidogo (dakika 10–15)
>>Wahi hospitali ikiwa rangi inaongezeka

7. Homa ya matumbo (Gastroenteritis)

Chanzo:
Virusi (hasa Rotavirus)

Dalili:
>>Kuharisha + kutapika
>>Upungufu wa maji mwilini

Tahadhari:
>>ORS, maziwa ya mama, na uangalizi wa daktari

Itaendelea...

Lishe ya Mtoto wa Miezi 12–24👉Kipindi hiki ni cha mpito kutoka utoto wa kunyonya kuelekea kula k**a familia, na ndicho k...
19/12/2025

Lishe ya Mtoto wa Miezi 12–24

👉Kipindi hiki ni cha mpito kutoka utoto wa kunyonya kuelekea kula k**a familia, na ndicho kinachoamua afya, ukuaji, na tabia ya kula ya mtoto katika maisha yake yote.
Mtoto sasa ni mtoto mchanga anayejitegemea zaidi, anaanza kutembea, kuzungumza maneno ya kwanza, na kuelewa ladha mbalimbali za chakula.

Maendeleo muhimu ya kimaumbile na kiakili katika umri wa miezi 12–24

👉Mtoto anaongezeka haraka uzito na urefu, japo si kwa kasi k**a miezi ya awali.

👉Ubongo wake unaendelea kukua kwa kasi, hivyo unahitaji lishe yenye virutubishi vya ubongo (omega-3, protini, madini, chuma).

👉Anaanza kuwa na hisia za ladha na harufu, hivyo anaanza kuchagua chakula anachokipenda.

👉Mfumo wa mmeng’enyo umekomaa zaidi, unaweza kumeng’enya vyakula vingi vya familia.

👉Meno zaidi yanachipuka, hivyo anaweza kutafuna chakula kigumu kidogo.

👉Hapa ndipo wazazi wengi hufanya kosa — ama kumlisha chakula cha watu wazima kilicho na chumvi nyingi, au kumbakiza kwenye uji laini kwa muda mrefu.

Uhusiano na Maziwa ya Mama

👉Maziwa ya mama bado ni muhimu, hasa hadi mtoto anapofikisha miaka 2.

👉Yanampa kinga, mafuta mazuri, protini na joto la kihisia.

👉Hata hivyo, sasa chakula ndicho chanzo kikuu cha nishati na virutubishi.

✔️Ushauri: Endelea kumnyonyesha mara 2–3 kwa siku (asubuhi na usiku), lakini lishe kuu iwe kwenye vyakula vya kawaida vya familia.

Makundi ya Chakula Muhimu kwa Umri wa Miezi 12–24

👉Vyakula vya Wanga (nishati)
>>Nafaka: wali, ugali, uji mzito wa mtama, ulezi, ngano, au mahindi.
>>Mizizi: viazi, ndizi, mihogo, viazi vitamu, au yam.
>>Tambi au chapati laini.

Faida: Hutoa nguvu nyingi kwa michezo, kutembea, na ukuaji wa mwili.

👉Vyakula vya Protini (kujenga mwili)
>>Wanyama: nyama laini, kuku, samaki, dagaa, mayai.
>>Mimea: maharage, dengu, soya, njegere, karanga au siagi ya karanga.

Faida: Kujenga misuli, damu, kinga ya mwili, na ubongo.

✔️Angalia usafi wa nyama au samaki; iwe imeiva vizuri kabisa.

👉Mafuta Mazuri (energy + ukuaji wa ubongo)
>>Mafuta ya alizeti, karanga, n**i, parachichi, samaki (hasa dagaa), au mafuta ya zeituni.
>>Kila chakula kikuu kiwe na kijiko 1–2 cha mafuta haya.

✔️Faida: Kukuza ubongo (omega-3, omega-6).
Kusaidia vitamini k**a A, D, E, K kufyonzwa.
Kusaidia uzito mzuri.

👉Mboga za majani
>>Spinachi, mchicha, matembele, karoti, pumpkin, sukuma wiki, brokoli.
>>Ziive vizuri, zipondwe au zikate kwa vipande vidogo.

✔️Faida: Huongeza vitamini A, chuma, na fiber kwa mmeng’enyo mzuri.

👉Matunda
>>Parachichi, papai, apple, ndizi, embe, tikiti, nanasi (kiasi kidogo).
>>Pendelea matunda halisi, si juisi ya dukani.

✔️Faida: Vitamini C, madini, na kusaidia choo (fiber).

👉Vyakula vya Maziwa
>>Maziwa ya mama au ya ng’ombe (yasiyotiwa sukari).
>>Mtindi (natural yoghurt) au jibini laini.

✔️Faida: Kalsiamu kwa mifupa na meno.

Ratiba ya Milo (Meal Schedule)

Mtoto wa mwaka mmoja na zaidi anatakiwa kula mara 5–6 kwa siku: Milo 3 mikuu + vitafunwa 2–3.

👉Asubuhi (1:00–2:00): Maziwa ya mama au maziwa ya ng’ombe + uji mzito wa nafaka mchanganyiko + tunda

👉Saa 4:00: Kifungua kinywa kidogo (mtindi au parachichi)

Saa 7:00 mchana: Chakula 👉kikuu: wali + samaki + mboga + kijiko cha mafuta mazuri

👉Saa 10:00 jioni: Tunda au viazi vilivyochemshwa

👉Saa 1:00 usiku: Chakula kikuu (ugali/ndizi + maharage/kuku + mboga)

👉Kabla ya kulala: Kunyonya au kikombe cha maziwa

👉Maji safi yaliyochemshwa yatolewe muda wote, hasa wakati wa joto.

Kiasi cha Chakula

👉Kila mlo mkuu: kikombe 1 (250–300 ml).

👉Kila vitafunwa: kiasi cha nusu kikombe (125 ml).

👉Kila mtoto ana njaa tofauti — angalia dalili zake (akitaka zaidi, mpe zaidi).

Vyakula vya Kuepuka

👉Chumvi nyingi, sukari, vyakula vya kukaanga.

👉Juisi za dukani, p**i, biskuti zenye kemikali.

👉Vyenye viungo (pilipili, curry) au vyakula vizito kwa mmeng’enyo.

👉Asali kwa watoto chini ya miezi 18 (inaweza kuwa na botulism).

Mbinu Bora za Kumlisha

👉Mtoto ale na familia: Hii humsaidia kujifunza haraka tabia ya kula vizuri.

👉Usimlazimishe: Tumia maneno mazuri, tabasamu, na subira.

👉Tumia vyombo vya rangi au sauti za kuchekesha kumvutia kula.

👉Kinga usafi: Mikono, sahani, na vyombo viwe safi kila wakati.

👉Rudia vyakula alivyokataa: mara kadhaa bila kulazimisha — watoto wengi hukubali baada ya mara kadhaa.

👉Weka ratiba: usimlishe kiholela, mpe muda maalum kila siku ili mwili wake uelewe mpangilio wa kula.

Faida Kuu za Lishe Bora Kipindi Hiki

✔️Ukuaji bora wa mwili na ubongo.

✔️Kinga imara dhidi ya maradhi (hasa upungufu wa damu na utapiamlo).

✔️Meno, mifupa, na ngozi zenye afya.

✔️Tabia nzuri ya kula kwa nidhamu.

✔️Ujasiri, nguvu, na umakini katika kujifunza.

Mfano wa Menyu ya Kila Siku (Kwa Mtoto wa Mwaka 1–2)

👉Asubuhi: Uji wa ulezi uliopikwa kwa maziwa + kijiko cha mafuta ya karanga + parachichi

👉Mchana: Wali + samaki wa kukaangwa kwa mafuta kidogo + mboga za majani

👉Jioni: Papai lililoiva au mtindi

👉Usiku: Ugali + maharage + karoti + kijiko cha mafuta ya n**i

👉Kabla ya kulala: Kikombe cha maziwa au kunyonya

Maendeleo ya mtoto katika kipindi cha miezi 9–11👉Mtoto huanza kutambaa, kucheza, na kujifunza kushika vyakula kwa vidole...
19/12/2025

Maendeleo ya mtoto katika kipindi cha miezi 9–11

👉Mtoto huanza kutambaa, kucheza, na kujifunza kushika vyakula kwa vidole (finger foods).

👉Mifupa, ubongo, na misuli huendelea kukua haraka.

👉Haja ya nishati na madini (k**a chuma na zinki) huongezeka zaidi kuliko miezi ya awali.

👉Maziwa ya mama bado ni muhimu, lakini hayawezi peke yake kumtosheleza.

Uhusiano wa lishe na maziwa ya mama

👉Mtoto bado anatakiwa kunyonya angalau mara 3–5 kwa siku (usiku na mchana).

👉Maziwa ya mama hubaki kuwa chanzo kikuu cha:
>>Kinga ya mwili (antibodies)
>>Mafuta mazuri (hasa DHA kwa ukuaji wa ubongo)
>>Protini nyepesi

👉Lakini sasa, vyakula vya nyongeza (complementary foods) vinapaswa kuwa nusu ya lishe yake ya kila siku.

Aina ya vyakula vinavyopendekezwa

Makundi makuu 6 ya chakula:

👉Wanga (Carbohydrates):
>>Uji mzito wa nafaka mchanganyiko (mtama, ulezi, ngano, mchele).
>>Viazi vilivyopondwa, ndizi zilizochemshwa, au ugali laini.
>>Tambi laini au wali laini.

👉Protini (Body building foods):
>>Mayai (yolk hasa kwa chuma).
>>Samaki waliopondwa vizuri (k**a dagaa, sangara, au sato).
>>Maharage, dengu, soya, njegere zilizosagwa vizuri.
>>Kuku au nyama laini iliyopondwa au iliyosagwa.

👉Mafuta mazuri (Energy & brain growth):
>>Mafuta ya alizeti, karanga, parachichi, n**i, au samaki (omega-3).
>>Kikombe kimoja cha chakula kiongezwe kijiko kimoja cha mafuta mazuri.
>>Mafuta haya husaidia ubongo, ngozi, na kuongeza nguvu.

👉Matunda:
Ndizi, papai, parachichi, apple au embe lililoiva.
>>Hutoa vitamini A, C, na antioxidants.

👉Mboga za majani:
Spinachi, matembele, mchicha, karoti, pumpkin, au sukuma wiki zilizoiva vizuri.
>>Huongeza madini, vitamini, na nyuzinyuzi (fiber).

👉Vyakula vyenye madini ya chuma na zinki:
>>Mayai, samaki wadogo, nyama nyekundu laini, dengu, soya, nafaka zisizokobolewa.

Ratiba ya milo

👉Asubuhi: Kunyonya + uji mzito wenye mafuta (k**a kijiko cha parachichi)

👉Saa 5–6 mchana: Chakula kikuu (wali laini + samaki/dengu + mboga)

👉Saa 9 jioni: Tunda lililosagwa (ndizi/parachichi/papai)

👉Saa 12 jioni: Chakula kingine kikuu (viazi/ugali laini + protini + mboga)

👉Kati ya milo (mlo hado mlo): Kunyonya au maji safi kidogo (ikiwezekana yaliyochemshwa na kupozwa)

Kiasi cha chakula

👉Kila mlo uwe takriban ½ kikombe hadi kikombe 1 (125–250 ml).

👉Ongeza kadiri mtoto anavyoongeza hamu ya kula.

👉Usimlishe kwa nguvu, bali mshawishi kwa upole na tabasamu.

Vyakula vya kuepuka

👉Chumvi nyingi au sukari.

👉Vyakula vya kukaanga, vinywaji vya soda, au vyenye viungo kali.

👉Asali (inaweza kuwa na bakteria hatari “botulism”).

👉Vyakula vigumu au vinavyoweza kumkwamisha k**a karanga nzima, p**i, au matunda magumu.

Vidokezo vya kivitendo

✔️Kila mlo uwe mchanganyiko wa vyakula angalau 3 vya makundi tofauti. Mfano: wali + dagaa + mchicha + kijiko cha mafuta.

✔️Tumia mafuta mazuri kila mlo kuongeza nishati.

✔️Usafi ni muhimu: mikono, vyombo, na chakula viwe safi kila wakati.

✔️Mpe mtoto nafasi ya kujifunza kula mwenyewe taratibu (self-feeding).

Faida kuu za lishe bora kipindi hiki

👉Ukuaji bora wa ubongo na kumbukumbu.

👉Kuongezeka uzito na urefu kwa kiwango kinachotakiwa.

👉Kinga thabiti dhidi ya magonjwa.

👉Tabia nzuri ya kula na kutafuna.

LISHE YA MTOTO MIEZI 6–8Miezi 6 ndiyo umri rasmi wa kuanza vyakula vya nyongeza (complementary foods), kwa sababu:✔️Mahi...
18/12/2025

LISHE YA MTOTO MIEZI 6–8

Miezi 6 ndiyo umri rasmi wa kuanza vyakula vya nyongeza (complementary foods), kwa sababu:

✔️Mahitaji ya mtoto huzidi uwezo wa maziwa ya mama peke yake.

✔️Mfumo wa mmeng’enyo (tumbo, utumbo) umekomaa kiasi cha kumeng’enya chakula laini.

✔️Mtoto anaonyesha hamu ya kula (anafuatilia chakula cha wengine, kufungua mdomo, au kujaribu kutafuna).

✔️Hata hivyo, maziwa ya mama bado ndiyo lishe kuu. Vyakula vya nyongeza ni kuongeza, si kubadilisha.

Lengo la kipindi hiki

>> Kumzoesha mtoto ladha mbalimbali.

>> Kumtayarisha kwa chakula cha kawaida.

>> Kutoa virutubishi ambavyo maziwa pekee hayawezi tena kumtosheleza (k**a chuma, zinki, nishati zaidi).

Jinsi ya kuanza vyakula vya nyongeza

>> Anza kidogo, ongeza taratibu.

>> Vyakula viwe laini (puree, uji mzito, vilivyopondwa vizuri).

>> Usitumie chumvi, sukari, au viungo vya chakula vya watu wazima.

>> Usafi ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote.

>> Mtoto awe anatulia, si mwenye hasira au usingizi.

Aina za vyakula vya kuanza navyo

Uji:

Uji mzito kidogo (si maji maji) wa:

Mahindi, mtama, ulezi, ngano, au mchele.

Unaweza kuuchanganya na maziwa ya mama, mafuta ya alizeti, au unga wa karanga/mbaazi kuongeza nguvu.

Kiasi: kijiko 1–2 mwanzo, kisha ongeza hadi nusu kikombe.

Vyakula vilivyopondwa:

Viazi vitamu, viazi mviringo, ndizi, boga, karoti, au mihogo laini.

→ Chemsha vizuri, pondaponda hadi laini.

Matunda yaliyopondwa:

Parachichi, papai, embe, apple, pear.

→ Yasichanganywe na sukari.

Vyakula vya protini (kidogo kidogo):

Yai lililochemshwa vizuri (anza na kijiko kidogo cha kiini pekee).

Samaki laini bila mifupa.

Maharage au dengu yaliyopondwa vizuri.

Mpangilio wa mlo kwa siku

Asubuhi: Uji mzito wa nafaka (ulezi + unga wa karanga kidogo). Tumia kijiko 2–4

Mchana: Viazi vilivyopondwa + karoti au boga. Kijiko 2–4

Jioni: Matunda yaliyopondwa (parachichi/papai). Kijiko 2–4

Kati ya milo: Anyonye maziwa ya mama mara kadhaa.

Kumbuka: Mlo wa nyongeza mara 2–3 kwa siku + maziwa ya mama kadhaa.

Kadri wiki zinavyopita, ongeza kiasi na wingi wa vyakula.

Ubora wa lishe (chakula mchanganyiko)

Kila sahani ya mtoto iwe na angalau makundi matatu kati ya haya:

Wanga: Uji, viazi, ndizi, wali. Kwa ajili nishati mwilini

Protini: Maharage, samaki, yai. Kujenga mwili

Mboga na matunda: Karoti, boga, papai, parachichi. Vitamini na kinga ya mwili

Mafuta: N**i, karanga, mbegu za maboga au alzeti, n.k. Kwa ajili ya nguvu na ukuaji wa ubongo.

Usafi wa chakula

Kwa umri huu, mtoto yuko hatarini sana kupata maambukizi.

Masharti:

Mikono ya mlezi iwe safi kabla ya kulisha.

Chakula kiwe kimepikwa siku hiyo hiyo.

Usitunze chakula muda mrefu nje ya jokofu.

Vyombo vya mtoto viwe safi na vya plastiki isiyo hatarishi.

Ishara kwamba mtoto anakubali vyakula

Anafurahia kula.

Anafungua mdomo anapoona kijiko.

Anaanza kumeza vizuri.

Kinyesi kinabadilika rangi au umbile (ni kawaida, mradi si kuharisha sana).

Ikiwa: Mtoto anatema kila kitu. Anakataa kula siku kadhaa. Rudia aina tofauti ya chakula au ushauriane na daktari/mtaalamu wa lishe.

Maziwa ya mama yabaki kuwa msingi

Mtoto bado anahitaji angalau 6–8 kunyonya kwa siku.

Maziwa ya mama yanatoa kinga, maji, na virutubishi vya ziada.

Hakikisha mama anaendelea kula vizuri ili maziwa yasiishe.

Mabadiliko ya ukuaji katika miezi hii

Uzito: Unaongezeka kwa wastani wa 0.5–0.7 kg kwa mwezi

Urefu: Unaongezeka 1.5–2 cm kwa mwezi

Uwezo wa kutafuna: Ananza kuuma kwa fizi na kuzoea kijiko

Kujifunza: Anachunguza ladha na texture mpya

Harakati: Kuparamia vitu, kukaa bila msaada

Makosa ya kawaida kipindi hiki

Kumwachisha maziwa mapema – bado anayahitaji sana.

Kumpa chakula kigumu – kinaweza kumkosesha hamu au kuharisha.

Kumpa chumvi/sukari/mapishi ya watu wazima.

Kumpa vyakula vya viwandani (biscuits, juice, chocolate) — havina virutubishi.

Kumlisha bila usafi — huleta kuharisha.

Lishe ya mama kipindi hiki

Kwa kuwa mtoto bado ananyonya:

Mama aendelee kula vizuri na kunywa maji mengi.

Aongeze vyakula vyenye protini na madini ya chuma.

Epuke pombe, dawa bila ushauri wa daktari, na msongo wa mawazo (unapunguza maziwa).

Hitimisho:

Kipindi cha miezi 6–8 ni daraja muhimu kati ya maziwa pekee na kula kawaida. Mama azingatie usafi, vyakula sahihi, na utaratibu mzuri wa kunyonyesha. Mtoto atapata kinga imara, ubongo utakomaa vizuri, na hatopata utapiamlo.

LISHE KWA WATOTO WA MIEZI 0–6• Hii ni hatua ya kwanza ya maisha ya mtoto baada ya kuzaliwa.• Ni wakati ambao mwili, ubon...
15/12/2025

LISHE KWA WATOTO WA MIEZI 0–6

• Hii ni hatua ya kwanza ya maisha ya mtoto baada ya kuzaliwa.
• Ni wakati ambao mwili, ubongo, na mfumo wa kinga unajengeka haraka sana.
• Kwa hiyo, lishe yake inapaswa kuwa rahisi, salama, yenye virutubishi kamili na kinga asilia.

Chakula pekee kinachofaa:

>> Maziwa ya mama pekee (Exclusive Breastfeeding).

>> Hakuna haja ya kumlisha maji, uji, asali, juisi, au kitu chochote kingine.

Virutubishi vilivyomo katika maziwa ya mama:

>> Maziwa ya mama yana mchanganyiko kamili wa kila kitu mtoto anachohitaji kwa miezi sita ya kwanza. Maziwa ya mama yana virutubishi vifuatavyo:
1. Protini (lactalbumin). Kazi yake ni kujenga misuli, ubongo, na tishu mpya.

2. Mafuta (lipids). Ni chanzo cha nishati na ukuaji wa ubongo.

3. Wanga (lactose). Huongeza nguvu ya mwili na ukuaji wa ubongo.

4. Vitamini & Madini (Ca, Fe, Zn, Vit A, D, E, K). Husaidia kinga ya mwili, macho, kuimarisha mifupa, na kuongeza damu mwili.

5. Antibodies & Enzymes. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Faida kuu za maziwa ya mama kwa mtoto:

>> Huimarisha kinga ya mwili (immunity) — mtoto anakuwa na ulinzi wa asili dhidi ya magonjwa ya tumbo, mafua, n.k.

>> Hupunguza hatari ya kuharisha au kupata mzio (allergy).

>> Huimarisha ubongo na akili (mafuta ya DHA yanayopatikana tu kwenye maziwa ya mama).

>> Hujenga uhusiano wa kihisia kati ya mama na mtoto.

>> Huchelewesha mimba nyingine (asili ya mpango wa uzazi wa muda mfupi).

Maziwa ya mwanzo (Colostrum)

>> Saa 0–3 baada ya kujifungua, mama huzalisha maziwa ya njano meupe yanayoitwa colostrum.

Umuhimu wa colostrum:

>> Ni dozi ya kwanza ya chanjo ya asili kwa mtoto.

>> Ina antibodies nyingi (hasa IgA) zinazolinda tumbo la mtoto.

>> Husaidia kutoa kinyesi cha kwanza (meconium) na kusafisha utumbo.

>> Ina protini nyingi, mafuta kidogo — inarahisisha mmeng’enyo wa kwanza.

• Wazazi wengi hufanya kosa la kumwaga colostrum wakidhani ni chafu au nzito — ni kosa kubwa sana!

Jinsi ya kunyonyesha kwa usahihi

Ratiba:
>> Mtoto anyonye mara nyingi anapotaka — wastani wa mara 8–12 kwa siku.

>> Kila zamu ya kunyonyesha ichukue dakika 10–20.

>> Anyonyeshe mbele na nyuma ya t**i ili apate maziwa yote (maziwa ya mwanzo na ya mwisho).

Maziwa ya mwanzo vs ya mwisho:

• Foremilk (maziwa ya mwanzo). Dakika za mwanzo. Yana maji na sukari nyingi. Huzuia kiu

• Hindmilk (maziwa ya mwisho). Baada ya dakika 10+ . Yana mafuta mengi. Hutoa nguvu na kushibisha

Kwa hiyo: usimbadilishe t**i mapema — mpe muda amalize upande mmoja kabla ya kubadilisha.

Ishara kwamba mtoto anapata maziwa ya kutosha:

>> Anatulia baada ya kunyonya.

>> Anakojoa mara 6+ kwa siku (mkojo wa njano hafifu).

>> Anaongeza uzito kila wiki.

>> Ngozi yake ni laini na yenye mng’ao.

>> Anahema kwa utulivu na anapunguza kulia kupita kiasi.

Ikiwa:
>> Analia sana,
>> Ana uzito unapungua,
>> Au hana haja ndogo mara kwa mara,
Muone mtaalamu wa afya mapema.

Lishe ya mama anayenyonyesha:
Lishe ya mama inaamua ubora wa maziwa.

Mama anatakiwa kula:

>> Vyakula vyote vikuu: wanga, protini, mafuta, mboga, matunda.

>> Vyakula vya kuongeza maziwa: uji wa ulezi, karanga, maziwa, supu ya samaki, majani ya maboga, kitoweo cha kunde.

>> Maji mengi: vikombe 8–10 kwa siku.

• Epuka: pombe, sigara, kahawa nyingi, vyakula vyenye viambato bandia (vya viwandani).

Makosa ya kawaida ya wazazi:

>> Kumpa maji kabla ya miezi 6. Hupunguza maziwa ya mama na huleta maambukizi ya tumbo.

>> Kutonyonyesha usiku — wakati huu ndiyo maziwa huzalishwa zaidi.

>> Kutonyonyesha mara kwa mara — maziwa hupungua.

>> Kutonyonyesha vizuri (mtoto hakushika t**i lote vizuri).

>> Kumwachisha mapema bila sababu.

Faida kwa mama:

>> Husaidia tumbo kurudi haraka baada ya kujifungua.

>> Hupunguza hatari ya saratani ya mat**i na ya kizazi.

>> Hutoa utulivu wa kihisia (kutokana na homoni ya oxytocin).

>> Husaidia mpango wa uzazi wa asili (LAM method).

Ukiona dalili zifuatazo muone mtaalam wa afya:

>> Mat**i kuvimba au maumivu (mast**is).

>> Chuchu kuvimba au kukatika.

>> Mtoto kutopata mkojo wa kutosha.

Itaendelea (miezi 6+)

15/12/2025

Leo jioni tunaanza masomo rasmi.

Afya360: Health in Full Circle

Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Afya360, mahali ambapo afya, urembo na ustawi wa mwili hukutana kwa ukamilifu.Hapa utapat...
10/12/2025

Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Afya360, mahali ambapo afya, urembo na ustawi wa mwili hukutana kwa ukamilifu.

Hapa utapata:

1. Elimu sahihi kuhusu afya na jinsi ya kuishi kwa mwili ulio na nguvu na kinga imara

2. Maarifa ya urembo wa ngozi na nywele kwa njia salama na za kisasa

3. Bidhaa bora za afya na urembo zinazokupa matokeo ya kweli

4. Ushauri, tips, na mafunzo ya kuboresha mwili na afya akili kila siku

Lengo letu ni kukupa afya kamili – kimwili, kiakili na kiroho.

Asante kwa kujiunga nasi!

Usisahau ku-like, Share & Invite rafiki zako tujifunze pamoja.

: Health in Full Circle

Address

Mkoani B
Kibaha
61102

Telephone

+255621247015

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya360 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share