Jestycuny Health Builder

Jestycuny Health Builder Pona kisukari bila masharti ya kuzuiliwa kula vyakula. Pia epukana na matibabu ya maisha ya kisukari.

VYAKULA SALAMA KWA MWENYE KISUKARI1. Samaki hasa wale wenye fati kwa wingi k**a samlon na sardines2. Mbogamboga za majan...
20/06/2022

VYAKULA SALAMA KWA MWENYE KISUKARI
1. Samaki hasa wale wenye fati kwa wingi k**a samlon na sardines
2. Mbogamboga za majani
3. Palachichi
4. Mayai
5. Mbegu za chia
6. Maharagwe
7. Kitunguu thaumu
8. Nyama yandege wafugwao k**a kuku
9. Kahawa
10. Vinywaji visivyowekwa sukari
11. Jusi za mbogamboga
12. Usikoboe mahindi, mchele, na mtama
13. Matunda kwa uchache

VYAKULA HATARI KWA MWENYE KISUKARI
1. Nafaka zilizokobolewa
2. Nafaka zilizoongezwa sukari
3. Mikate yenye sukari
4. Nafaka zisizo na kini
5. Mboga zenye chumvi nyingi
6. Mboga zilizoongezwa maziwa
7. Vinywaji vyote vya sukari usitumie mpaka kiwango chako cha sukari kiwe kipo katika udhibiti hata asali epukana nayo kwanza
8. Juisi zilizowekwa sukari ama zenye utamu k**a za matunda
9. Vinywaji vya energy (energy drink)
10. Nyama ya kuoka
11. Nyama zenye mafuta mengi
12. Nyama ya ngurue
13. Maziwa fresh
14. Samaki wa kuoka
15. Soda

Njia za kujikinga na kisukari
1. Dhibiti uzito wako. Hakikisha huna uzito w akupitiliza
2. Fanya mazoezi mara kwa mara
3. Kula mlo kamili
4. Punguza misongo ya mawazo
5. Kunywa maji kwa wingi
6. Wacha kuvuta sigara
7. Punguza ama wacha unywaji wa pombe
8. Punguza ulaji wa sukari kwa wingi
9. Pendelea kunywa kahawa
10. Tumia dawa za asili kiasi uwezavyo

KWA mawasiliano zaidi nipigie na ushauri piaa

USHAURI KUHUSU ULAJI WA CHAKULA KWA  WAGONJWA WA KISUKARI ... Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanagharimu fedha nyingi. ...
17/06/2022

USHAURI KUHUSU ULAJI WA CHAKULA KWA WAGONJWA WA KISUKARI ...
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanagharimu fedha nyingi. Kwa hiyo ni muhimu kuzuia na kudhibiti athari za kisukari mapema.
Ili kudhibiti ugonjwa wa kisukari mgonjwa anapaswa kupatiwa matibabu sahihi, kufuatilia na kupima afya mara kwa mara pamoja na kuzingatia mtindo bora wa maisha na taratibu zinazofaa za ulaji wa chakula.

Zifuatazo ni kanuni za ulaji unaofaa zinazopaswa kuzingatiwa na mgonjwa wa kisukari:

1.Kula mlo kamili (angalau mara 3 kwa siku) kwa kuzingatia muda mahususi aliojipangia kwani hashauriwi kukaa na njaa kwa muda mrefu.

2.Dhibiti kiasi cha nishati โ€“ lishe (wanga) katika chakula ili kisizidi mahitaji ya mwili. Kiasi kitegemee mahitaji ya mtu binafsi.

3.Ongeza ulaji wa vyakula vyenye makapi โ€“ mlo kwa wingi. Kiasi kikubwa cha nishati-lishe kitokane na vyakula vya asili ya nafaka isiyokobolewa, mizizi na ndizi za kupika.

Sukari inayotoka katika vyakula hivi hufyonzwa kwa taratibu na hivyo kupunguza kasi ya ongezeko la sukari katika damu.

4.Punguza kiasi cha vyakula vinavyozalisha nishati lishe kwa wingi hususani vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

5.Panga utaratibu wa kula chakula na matumizi ya dawa. Iwapo unatumia insulin au dawa za kushusha kiwango cha sukari katika damu unapaswa kujipangia muda wa kula chakula na kumeza dawa ili kuzuia kupungua kwa sukari katika damu. Epuka kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula.

6.Kula mbogamboga kwa wingi katika kila mlo.

7.Kula tunda katika kila mlo.

8.Epuka kunywa pombe.

9.Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi k**a soda, keki, biskuti, p**i na asali.

Kanuni nyingine za kuzingatia ni:

1.Punguza uzito iwapo una uzito uliozidi - au dhibiti uzito wa mwili ili usifikie uzito uliozidi. Ni muhimu kuwa na uwiano sahihi wa uzito wa mwili kulingana na urefu wako.

2.Zingatia usafi na usalama wa chakula

Kwa tiba na ushauri kuhusu kisukari Wasiliana nami kupitia namba 0629981577
WhatsApp 0629981577...

*๐—จ๐—ก๐—”๐—ช๐—˜๐—ญ๐—”๐—๐—˜ ๐—ž๐—จ๐—ฃ๐—จ๐—ก๐—š๐—จ๐—ญ๐—” ๐—›๐—”๐—ง๐—”๐—ฅ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฃ๐—”๐—ง๐—” ๐—จ๐—š๐—ข๐—ก๐—๐—ช๐—” ๐—ช๐—” ๐—ž๐—œ๐—ฆ๐—จ๐—ž๐—”๐—ฅ๐—œ*Elewa hatari iliyo mbele ya Afya yako.Aina ya 2 ya kisukari in...
15/06/2022

*๐—จ๐—ก๐—”๐—ช๐—˜๐—ญ๐—”๐—๐—˜ ๐—ž๐—จ๐—ฃ๐—จ๐—ก๐—š๐—จ๐—ญ๐—” ๐—›๐—”๐—ง๐—”๐—ฅ๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฃ๐—”๐—ง๐—” ๐—จ๐—š๐—ข๐—ก๐—๐—ช๐—” ๐—ช๐—” ๐—ž๐—œ๐—ฆ๐—จ๐—ž๐—”๐—ฅ๐—œ*

Elewa hatari iliyo mbele ya Afya yako.

Aina ya 2 ya kisukari inaweza kuchukua miaka kadhaa kupevuka, na baadhi ya watu hawatambui dalili zozote mpaka wamechelewa sana.

Kwahiyo kwa kadiri unavyoelewa zaidi kuhusu vihatarishi, ndivyo utakavyokuwa umejidhatiti vizuri zaidi kutambua kitu chochote cha kushangaza na kufanya maamuzi sahihi ya mtindo wa maisha.

Mwanzo mzuri ni kuangalia kiwango chako cha hatari kwa kutumia kikokotoo cha mtandaoni cha ukaguzi wa hatari ya aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari. Unaweza pia kumuuliza daktari wako kuhusu hatari yako.

Tabia zenye manufaa kiafya husaidia sana
Kudumisha uzito wa mwili ambao ni mzuri kiafya.

๐—ธ๐˜‚๐—ณ๐—ฎ๐—ป๐˜†๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐˜‡๐—ผ๐—ฒ๐˜‡๐—ถ. kunaweza kusaidia kupunguza hatari yako ya kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari. Zaidi ya hilo, pia utajihisi ni mwenye afya zaidi na furaha zaidi.

Tafiti zinaonyesha kwamba hata dakika 30 tu za kutembea haraka kila siku zinaweza kupunguza hatari yako ya kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.

Kwahiyo vaa viatu vyako vya kutembelea na uende kutembea bila kuhofia kupata kesi ya uzururaji na jihusishe pia na mazoezi mengine ya viungo k**a kuruka kamba n.k

๐—น๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฒ ๐—ฏ๐—ผ๐—ฟ๐—ฎ.
Ila usijali: kwani hiyo haimaanishi kupiga marufuku vyakula vyako vyote uvipendavyo. Jambo la muhimu zaidi ni kuzingatia ulaji wa kiasi. Hiyo inamaanisha kula mara kwa mara milo kamili usiyozidisha ujazo.

Jaribu kupanga ratiba ya chakula chenye afya kwa wiki.

Kuwa na friji iliyojaa chakula kinachofaa itakusaidia kuepuka kukosa kula na kula kupita kiasi. Na bado unaweza kustahili kufurahia chakula au kitafunio ukipendacho.

Kwa kufanya mabadiliko machache kadhaa, ni rahisi kutunza afya yako.

kwa ushauri nasaha piga 0629981577
WhatsApp 0629981577

*๐—Ÿ๐—˜๐—ข ๐—ง๐—จ๐—ง๐—”๐—ญ๐—จ๐—ก๐—š๐—จ๐— ๐—ญ๐—œ๐—” ๐—”๐—œ๐—ก๐—” ๐—ฌ๐—” 2 ๐—ฌ๐—” ๐—จ๐—š๐—ข๐—ก๐—๐—ช๐—” ๐—ช๐—” ๐—ž๐—œ๐—ฆ๐—จ๐—ž๐—”๐—ฅ๐—œ*Aina ya 2 hutokea wakati kongosho linapopunguza uzalishaji wa insuli...
13/06/2022

*๐—Ÿ๐—˜๐—ข ๐—ง๐—จ๐—ง๐—”๐—ญ๐—จ๐—ก๐—š๐—จ๐— ๐—ญ๐—œ๐—” ๐—”๐—œ๐—ก๐—” ๐—ฌ๐—” 2 ๐—ฌ๐—” ๐—จ๐—š๐—ข๐—ก๐—๐—ช๐—” ๐—ช๐—” ๐—ž๐—œ๐—ฆ๐—จ๐—ž๐—”๐—ฅ๐—œ*

Aina ya 2 hutokea wakati kongosho linapopunguza uzalishaji wa insulini au wakati insulini haiathiri seli namna ifaavyo.

Baada ya kuzitambulisha kwa ufupi aina hizi mbili za ugonjwa wa kisukari, tunaendelea na makala hii kwa kuzingatia aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.

Ni yapi yanayohusiana na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari?

Aina ya 2 ya kisukari ni ugonjwa ulioenea zaidi duniani.

Ni nani aliye katika hatari?
Kila mtu ana kiwango tofauti cha hatari ya kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.

Kiwango cha hatari kinahusishwa na mtindo wa 1: maisha
2: umri
au sababu za kimaumbile (jenetiki).

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea mtu kuwa kwenye hatari ya kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari:

*kuwa na uzito wa kupita kiasi

*kutokujishughulisha kimwili mfano kutofanya mazoezi ya viungo

*kuwa na umri wa miaka 45 au zaidi

*kuwa na historia ya ugonjwa wa kisukari,, aina ya 2 katika familia
kuwa na asili ya Waafrika Weusi, Waafrika wa Karibiani, au Asia ya Kusini.

Ni muhimu kukumbuka kwamba unaweza kupata aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari bila kuwa na historia yoyote ya ugonjwa huo katika familia.

Na pia kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia haimaanishi kuwa utaupata. Jambo la msingi zaidi ni kuelewa sababu zinazoathiri kiwango chako cha hatari ya kuupata.

Nini hutokea unapokuwa na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari?

Watu wenye aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari wanaweza kupata dalili kadhaa.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili ambazo ni kawaida kutokea:

*kwenda haja ndogo mara nyingi sana, haswa wakati wa usiku.

*kuhisi kiu kuliko kawaida

*kuhisi uchovu sana

*kupungua uzito bila sababu

*mikato au vidonda kuchukua muda mrefu kupona

*uwezo hafifu wa kuona (kuona ukungu).

Baadhi ya watu hawatambui dalili zao kwa muda mrefu. Kwahiyo ni muhimu uelewe ni nini kinakuweka hatarini. Ikiwa haujatibiwa.

KWA USHAURI 0629981577
WhatsApp: 0629981577

*UGONJWA WA KISUKARI NI NINI?*Kabla ya kuzungumza kuhusu ugonjwa wa kisukari, acha kwanza tuangalie jinsi mwili unavyopa...
12/06/2022

*UGONJWA WA KISUKARI NI NINI?*

Kabla ya kuzungumza kuhusu ugonjwa wa kisukari, acha kwanza tuangalie jinsi mwili unavyopata glukosi.

Unapokula chakula, mfumo wa kumengโ€™enya chakula hukichakata na kutengeneza glukosi.

Glukosi hiyo inapoingia kwenye mfumo wa damu, husababisha kongosho kutoa homoni inayoitwa insulini.

Insulini huzunguka mwilini kupitia damu, na hii huwezesha seli kupata glukosi na kuitumia kuleta nguvu na joto mwilini.

Unaweza kuifikiria insulini k**a funguo isiyoonekana kwa macho inayoruhusu glukosi kuingia kwenye seli.

Wakati ufunguo huo haupo au unaacha kufanya kazi, glukosi katika mwili haiwezi kwenda mahali popote.

Ikiwa viwango vya glukosi katika damu vinabaki kuwa juu sana kwa muda mrefu, unaweza kuanza kujihisi mgonjwa. Huo ndiyo ugonjwa wa kisukari.

*AINA ZA KISUKARI*

Kuna aina kuu 2 za ugonjwa wa kisukari: aina ya 1 na aina ya 2.

Aina ya Kwanza:
Hutokea wakati mfumo wa kinga ya mwilini unashambulia kongosho ili lisiweze kutoa insulini ya kutosha.

Katika hali fulani, kongosho linaweza kuacha kabisa kutoa insulini.

0629 981577

Nimewasaidia watu wengi wenye changamoto ya ugonjwa wa kisukari wamepona kabisa kwa kutumia virutubisho lishe. Karibu nikushauri nikupatie tiba pia.

Afya yako utajiri wako

Address

Mbeya

Opening Hours

Monday 08:00 - 19:00
Tuesday 08:00 - 19:00
Wednesday 08:00 - 19:00
Thursday 08:00 - 19:00
Friday 08:00 - 19:00
Saturday 08:00 - 19:00
Sunday 10:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jestycuny Health Builder posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Jestycuny Health Builder:

Share