Amken Herbal Clinic

Amken Herbal Clinic Amkeni herbal clinic Tunajikita katika nyanja zifuatazo⁣

Afya ya mama na mtoto⁣, Afya ya uz

08/11/2019

JE, WAJUA AINA ZA UVIMBE(FIBROIDS AU MYOMA), DALILI ZAKE NA VISABABISHI VYAKE?

Leo Amkeni herbal clinic tunakuletea kwa kifupi Aina za uvimbe. Hii ni kutokana tukiangalia tatizo la uvimbe Kwa kina mama sasa linazidi kuongezeka kwa kasi sana. Mabinti wengi na hata wanandoa wanazidi kupatwa na janga hili. Baadhi ya kina mama wamekuwa wakiondolewa kizazi kwa ajili ya tatizo hili.

Sasa hebu tuangalia ili tufahamu Kwa undani zaidi aina ya uvimbe, dalili zake na visababishi vyake.

AINA ZA UVIMBE(FIBROIDS)

- Zipo aina kuu tatu za uvimbe.

1. Uvimbe unaotokeza juu ya tumbo la uzazi, na unaweza kuwa ndani ya kizazi pia, nao kitaalamu hujulikana, “Intramural Fibroids”.

- Dalili zake huwa k**a ifuatavyo:
(a). Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.
(b). Maumivu ya nyonga
(c). Maumivu ya mgongo
(d). Kukosa choo na tumbo kujaa gesi
(e). Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
(f). Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa hasa uvimbe unapokuwa sehemu ya shingo ya kizazi.

2. Uvimbe unaotokea ndani ya nyama ya Kizazi, nao kitaalamu hujulikana, “Submucosal Fibroids”.

Uvimbe huu unaweza kujitokeza mmoja au zaidi ya mmoja(multiple) na ukawa mkubwa zaidi.

- Dalili zake ni:
(a). Kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu, yaani wiki 2 hata mwezi mzima.
(b). Kuhisi maumivu makali K**a chango wakati wa hedhi.
(c). Kupata hedhi Mara mbili ndani ya mwezi au hedhi kuvurugika.
(d). Kukosa hedhi miezi 2-3
(e). Maumivu ya tumbo chini ya kitovu, mgongo na tumbo.

Aina hii ya uvimbe husabisha ugumba Kwa wanawake wenye umri wa kuzaa. Zipo njia kadhaa ambazo aina hii ya uvimbe husababisha ugumba, kwa mfano: uvimbe wa aina hii unaweza kuziba mirija ya mayai, na hivyo kuzuia mbegu za mwanaume zisirutubishe yai.

3. Uvimbe utokezao nje juu ya ukuta wa kizazi, nao kitaalamu hujulikana, “Subserol Fibroids”.

- Dalili zake huwa k**a ifuatavyo:
(a). Kuhisi vichomi na maumivu tumboni
(b). Maumivu makali kutokana na vivimbe kushik**ana tumboni.
(c) Kukosa choo na tumbo kujaa gesi
(d). Mgongo au nyonga kuuma
(e). Kuhisi kukojoa mara Kwa mara

VISABABISHI VYAKE
Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni Wingi wa vichocheo vya estrogen ambavyo vipo katika miili ya wanawake hasa walio katika umri wa kuzaa, na vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake.

Unaweza wasiliana nasi kwa tiba na ushauri kwa namba 0676796421 au fika katika clinic yetu iliyopo Nane nane- Mbeya.

05/11/2019

Lifahamu tatizo la maumivu chini ya kitovu.

- Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadae hupelekea watu wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.

Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu.

Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi.

- Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.

- Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye anamaumivu chini ya kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kunauwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.

- Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huo huo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kunauwezekano akawa na PID hasa hasa k**a amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano.

-Afya mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara.

05/11/2019

SABABU ZINAZO SABABISHA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA UJAUZITO.

Tatizo la kutopata mimba linawasumbua wengi na huwapata familia kadhaa katika jamii, huweza kumpata mtu mmoja kati ya wanandoa 12 na ni tatizo linalowapata watu zaidi ya milioni 24 duniani kote.

Ugumba ni hali ya kutoweza kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango. Mtiririko wa upataji ujauzito ni k**a ifuatavyo;

Baada ya mwezi mmoja wa ndoa uwezo wa kushika ujauzito ni asilimia 20, baada ya miezi mitatu ya ndoa ni asilimia 50, baada ya miezi sita ya ndoa ni asilimia 75 na baada ya miezi 12 ni asilimia 90 mwanamke huweza kupata ujauzito.

Hali hii inaweza kutokea kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke, ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakidhani wanawake peke yao ndio ambao hupata tatizo hilo.

NINI SABABU ZA KUSHINDWA KUSHIKA UJAUZITO

- Kuziba kwa mijrija ya kupitisha mayai
- Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi au kutoa mayai isiokuwa na nguvu (lazy egg).
Mirija ya kupitisha mayai inaweza kuziba kutokana na;
- Ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambao unatokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa k**a kisonono na klamidia.
- Mirija ya mayai kujaa maji
- Utoaji mimba usio salama (unsafe abortions)
- Upasuaji maeneo ya kiunoni
- Ugonjwa wa endometriosis
Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi inaweza kutokana na;
- Umri mkubwa wa mwanamke, hasa miaka 35 – 40 na kuendelea.
- Uvutaji wa sigara
- Saratani ya Ovari
- Mionzi (radiations)
- Ugonjwa wa Polycystic ovarian disease (Ovarian Cyst)
Sababu nyingine za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa;
- Makovu katika mji wa uzazi kutokana na kutoa mimba.
- Mabonge ya kizazi (uterine fibroids)
- Kuziba kwa shingo ya uzazi
- Kulegea shingo ya uzazi
- Kisukari
- Matatizo ya tezi ya shingo (hyperthyroidism)
- Kufanya mazoezi ya kupitiliza (excessive exercising)

MATIBABU

Matibabu ya ugumba huhusishwa wenzi wote wawili, mwanaume na mwanamke. Yanahitaji uvumilivu na uelewa kwani wakati mwingine yanaweza yasiwe na mafanikio haraka au kabisa k**a tunavyotarajia. Kuna njia mbalimbali za kutibu ugumba, hizi zote zikijumuisha kuondoa tatizo linalosababisha mimba ishindwe kutunga au kutumia njia za kusaidia mimba itunge.
Njia za matibabu ya ugumba hujumuisha:

Mirija iliyoziba, vivimbe kwenye mji wa uzazi au kuta za uzazi kushik**ana huweza pia kutibiwa kwa Dawa tulizonazo hapa. Matatizo ya ugumba yanayotokana na ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi huweza kutibiwa kwa dawa . Dawa hizi hutumika kuziwezesha ovari kutoa mayai ya uzazi ili yawe tayari kurutubishwa. Mara nyingi huweza kusababisha kutoa mayai mengi katika mzunguko mmoja na kusababisha ujauzito wa watoto wengi (mapacha au zaidi) pale yanaporutubishwa..

Kwa ushauri na tiba wasiliana nasi Amkeni Herbal clinic kwa simu 0676796421.

30/10/2019

SARATANI YA DAMU (Leukemia)

Leukemia ni saratani inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph (lyphatic system). Kwa maneno rahisi, leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia, nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.

Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi mbalimbali.

K**a zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.

Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu zinapobadilika muundo wake wa kinasaba yaani viasili vyake vya DNA, ambavyo kwa kawaida hubeba maelekezo yanayoifanya seli yeyote ya kiumbe hai iweze kuishi, kutenda kazi zake, kujizaa na hata kufa, vinapobadilika maumbile na muundo wake kutokana na sababu mbalimbali. Kitendo cha kubadilika kwa maumbile na muundo wa DNA hujulikana k**a mutation. Ndiyo kusema basi, seli yeyote iliyopatwa na tatizo hili huwa na tabia ya kukua kwa haraka na kujizaa (kujigawa) kwa kasi zaidi kuliko kawaida, na pindi inapofikia muda wake wa kufa seli hiyo hugoma kufa badala yake huendelea kujizaa zaidi hatimaye kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa damu, hali inayosababisha saratani ya damu.

Ndiyo vipo! Pamoja na kwamba chanzo halisi cha saratani ya damu hakijulikani, lakini kuna mambo ambayo humuongezea mtu hatari ya kupata ugonjwa wa saratani ya damu.

Mambo ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya damu ni pamoja na:

Historia ya matibabu ya saratani hapo kabla: Watu ambao wamekuwa kuwa na aina nyingine za saratani hapo awali, na wakati wa matibabu wakapewa tiba ya mionzi au madawa makali ya saratani, wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya damu kwa sababu baadhi ya dawa hizi pamoja na mionzi huwa na tabia ya kuathiri pia seli nyeupe za damu pamoja na tishu zinazotengeneza seli hizo.
Kuwa na magonjwa mengine ya vinasaba: Ingawa haieleweki sawasawa uhusiano wake ulivyo, kuwa na baadhi ya magonjwa ya kinasaba k**a vile ugonjwa wa Down syndrome, yasemekana huongeza uwezekano wa muathirika kuugua pia ugonjwa wa saratani ya damu.
Baadhi ya magonjwa mengine ya damu: Watu wenye magonjwa mengine ya damu k**a vile ugonjwa wa damu unaoshambulia tishu za supu ya mifupa na kuzifanya zizalishe seli nyingi za damu bila uwiano unaotakiwa yaani myelodysplastic syndromes, huongeza pia uwezekano wa mtu kuugua saratani ya damu.
Kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi: Watu ambao wamewahi kupigwa na kiasi kikubwa cha mionzi k**a vile mlipuko wa mabomu au kulipuka kwa vinu na mitambo ya nuklea (nuclear reactors), wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya damu pamoja na saratani nyingine.
Kupigwa/kutumia baadhi ya kemikali: Watu waliowahi kukumbana na baadhi ya kemikali k**a vile benzene au zile zinazotumika kwenye viwanda vya kuyeyusha vyuma au kutengeneza magurudumu au mabomba ya plastic, nao pia wapo katika uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu.
Uvutaji sigara: Jambo hili pia huongeza uwezekano wa kupata aina mojawapo ya saratani ya damu.
Kuwa na historia ya ugonjwa huu katika familia: Watu ambao, baadhi ya ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu, nao pia wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya damu. Hata hivyo, hii haina maana kwamba leukemia inaambukizwa isipokuwa kuna uhusiano wa kifamilia tu katika kusababisha ugonjwa huu.
Jambo moja la kufahamu ni kuwa, wapo watu wengi ambao wamewahi kukumbana na vihatarishi nilivyovieleza hapo juu bila kupata leukemia, kadhalika wapo waliopata leukemia bila kukumbana na kihatarishi hata kimoja kati ya hivi. Kwahiyo. Uwepo wa vihatarishi hivi haimaanishi kuwa ni lazima mtu apate leukemia isipokuwa inaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Makundi ya leukemia
Wataalamu wa afya wanaiainisha leukemia katika makundi mbalimbali kulingana na kasi ya kusambaa kwa ugonjwa pamoja na aina ya chembe damu zilizoathirika.
Kulingana na aina ya chembe damu zilizoathirika, leukemia inaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili, ambayo ni:

Leukemia inayoathiri zaidi chembe damu zinazounda mfumo wa lymph ambayo kwa kitaalamu huitwa Lymphocytic leukemia. Mfumo wa lymph au lymphatic system ndiyo unaolinda mwili wako dhidi ya maradhi na maambukizi mbalimbali k**a vile VVU n.k. Chembe damu zinazohusika hapa huitwa lymphocytes.
Leukemia inayoathiri zaidi chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani kwa kitaalamu Myelogenous leukemia. Aina hii ya leukemia huathiri chembe zinazoitwa myeloid cells, ambazo ndizo huzaa chembe nyekundu za damu, chembe nyeupe za damu pamoja na chembe sahani. Chembe nyekundu husaidia kusafirisha hewa safi ya oksijeni mwilini na kutoa hewa chafu ya kabondioksaidi, chembe nyeupe hupambana na vimelea wa magonjwa mbalimbali k**a vile uti wa mgongo, minyoo, kifua kikuu, nk., wakati chembe sahani husaidia kuganda kwa damu pindi mtu unapoumia au kujikata.
Njia ya pili ya kuainisha makundi ya leukemia ni kwa kuangalia kasi ya kusambaa kwa ugonjwa wa saratani ya damu mwilini mwa muathirika. Kwa njia hii, kuna makundi makuu mawili ya leukemia, ambayo ni:

Leukemia inayosambaa kwa haraka au wataalamu wanaita acute leukemia. Katika aina hii, chembe damu huwa changa, zenye mambo mabaya yasiyo ya kawaida, na zisizoweza kufanya kazi zao vizuri. Lakini mbaya zaidi, hujigawa na kuzaliana kwa kasi kubwa kiasi cha kusambaa na kujazana katika damu kwa muda mfupi sana.
Leukemia inayosambaa taratibu au kwa kitabibu chronic leukemia. Katika aina hii, chembe damu huwa zimekomaa na zenye uwezo wa kujigawa na kuzaliana taratibu na hata kufanya kazi zake k**a kawaida. Chembe damu huweza kuishi kwa muda mrefu bila hata mgonjwa kuonesha dalili yeyote ya kuugua leukemia.
Aina za Leukemia
Bila kujalisha kasi ya kusambaa kwa ugonjwa au aina ya chembe damu iliyoathirika, leukemia inaweza kugawanywa katika aina zifuatazo:

Leukemia inayosambaa kwa haraka huku ikishambulia chembe damu zinazounda mfumo wa lymph yaani Acute lymphocytic leukemia (ALL). Aina hii huwapata zaidi watoto wenye umri mkubwa kidogo ingawa pia inaweza kwa kiasi fulani kuwapata hata watu wazima.
Leukemia inayosambaa kwa haraka huku ikishambulia chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani Acute myelogenous leukemia (AML). Aina hii ya leukemia inaongoza kati aina nyingine zote na huwapata watoto pamoja na watu wazima.
Leukemia inayosambaa taratibu huku ikishambulia chembe damu zinazounda mfumo wa lymph yaani chronic lymphocytic leukemia (CLL). Aina hii huwapata zaidi watu wazima, na nadra sana kutokea kwa watoto. Wagonjwa wa aina hii ya leukemia huweza kuishi vizuri kabisa bila kuwa na dalili zozote zile.
Leukemia inayosambaa taratibu huku ikishambulia chembe/seli zinazounda chembe damu nyingine za mwili yaani chronic myelogenous leukemia (CML). Watu wazima ndiyo waathirika wakubwa zaidi wa aina hii ya saratani ya damu. Mtu mwenye aina hii ya leukemia anaweza akapata dalili chache au asiwe na dalili kabisa kwa miezi hata miaka kabla ya ugonjwa kufumuka ghafla na kuanza kumshambulia.

Dalili za leukemia ni zipi?
Dalili za leukemia hutofautiana kutoka aina moja mpaka nyingine. Hata hivyo, dalili za jumla za leukemia ni pamoja na;

Homa au kujihisi baridi
Uchovu na ulegevu wa mwili
Maambukizi ya mara kwa mara
Kupoteza uzito bila kukusudia
Kuvimba tezi za mitoki
Kuvimba wengu (splenomegaly)
Kuvimba ini (hepatomegaly)
Kutokwa damu kirahisi na kupata michubuko ya mara kwa mara

Kuvilia kwa damu chini ya ngozi
Kutokwa jasho kupita kiasi hasa nyakati za usiku
Kuhisi maumivu ya mifupa
Kupungukiwa damu mara kwa mara
Mara nyingi dalili za Leukemia hazipo wazi na ni rahisi sana kwa mgonjwa kuchanganya na dalili za magonjwa mengine, hivyo ni vema kuwahi hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina na vipimo, mara tu uonapo dalili zilizotajwa hapo juu.

Uchunguzi na vipimo
Ni rahisi kwa daktari kugundua leukemia inayosambaa kwa kasi (acute leukemia) kuliko ile inayosambaa taratibu (chronic leukemia). Mara nyingi leukemia inayosambaa taratibu hugunduliwa mgonjwa anapoenda hospitali kwa ajili ya matibabu ya kitu kingine tofauti.

Pamoja na kukuuliza historia yako kwa lengo la kufahamu dalili na vihatarishi vya ugonjwa huu, daktari pia atakufanyia uchunguzi wa kina wa mwili kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa viashiria vya saratani ya damu k**a vile ngozi nyeupe (katika viganja, macho au ulimi), kuvimba kwa tezi za mitoki, kuvimba wengu na ini; kuvilia damu katika ngozi, michubuko, au k**a una dalili zozote za upungufu wa damu mwilini.

Vipimo utakavyofanyiwa ni pamoja na

Kipimo cha damu almaarufu k**a Full Blood Picture ambacho huonesha kiwango cha kila chembe damu iliyopo mwilini. FBP huonesha k**a chembe damu nyeupe zimeongezeka ama la, sambamba na chembe damu nyingine. Pia huonesha kiasi cha wingi wa damu, na iwapo mgonjwa ana upungufu wa damu ama la. Kwa ujumla wagonjwa wa leukemia huwa na ongezeko kubwa la chembe damu nyeupe zilizo changa, wakati chembe damu nyekundu pamoja na chembe sahani huwa chini.

Kipimo cha supu ya mifupa (bone marrow biopsy) hufanyika kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa seli za saratani. Kipimo hiki hufanyika kwa kuchukua sehemu ya mfupa wa nyonga au paja, kisha kuepelekwa maabara kwa uchunguzi. Biopsy husaidia kutofautisha kati ya leukemia na magonjwa mengine ambayo husababisha kuwepo kwa ongezeko la chembe damu nyeupe. Kwa maneno mengine, hiki ni kipimo tosha cha uthibitisho wa kuwepo kwa leukemia.

Vipimo vingine ni pamoja na vile vinavyoonesha utendaji kazi wa figo (renal function tests) na ini (liver function tests).

Baadhi ya madaktari hupenda pia kufanya kipimo cha uti wa mgongo (lumbar puncture) ili kuchunguza uwepo wa chembe za leukemia katika maji ya uti wa mgongo (spinal fluid).

Unaweza wasiliana nasi Amkeni Herbal Clinic kwa namba +255676796421 ili kupata ushauri wa kitabibu na tiba kwa mgonjwa ambae ameshafanya vipimo. Ahsante!.

VIDONDA VYA TUMBO (Peptic Ulcer Disease).Vidonda vya tumbo hujumuisha vidonda vya tumbo (stomach), vidonda vya utumbo mw...
29/10/2019

VIDONDA VYA TUMBO (Peptic Ulcer Disease).

Vidonda vya tumbo hujumuisha vidonda vya tumbo (stomach), vidonda vya utumbo mwembamba na vidonda vya koo la chakula
Mara nyingi vidonda hivi husababishwa na bakteria aitwae Helicobacter pylori, utumiaji wa dawa za maumivu mara kwa mara na mawazo mengi.

Kutokana na ukubwa wa uvamizi huu wa vidonda vya tumbo ni wazi kwamba vidonda vya tumbo hutofautiana na magonjwa yanayohusiana na tindikali (acid) ya kawaida k**a kuchubuka kwa kuta za tumbo na uathirikaji wa tumbo

Vidonda vya tumbo husababishwa na sababu zaidi ya moja. Vidonda vya tumbo hutokea mara baada ya uzalishaji wa tindikali ya Hydrochloric acid na kemikali ya pepsin kisha hupelekea kuliwa kwa kuta za tumbo au utumbo au koo.

Tumbo hujikinga kwa kutumia maji maji mithili ya k**asi, kemikali za bicarbonate, mzunguko wa damu kwenye tumbo na chembe hai zenye kujizalisha kwa haraka baada ya kuuliwa (epithelia cells)

Pindi tindikali ya Hydrochloric acid na pepsin zinapovamia kuta za tumbo, kemikali aina ya histamine huzalishwa ili kusababisha tindikali na pepsin zizalishwe kwa wingi zaidi. Mzunguko huu ukiendelea wa histamine na tindikali hupelekea vidonda vya tumbo kutokea

VIDONDA VYA TUMBO VITOKANAVYO NA BAKTERIA .

Bakteria aina ya Helicobacter Pylori ana uwezo mkubwa wa kupenya na kuingia ndani ya kuta za tumbo, huingia ndani ya tumbo kwasababu mazingira ya tumbo sio rafiki kwake. Bakteria huyu husababisha vidonda vya tumbo kwa njia zifuatazo;

* Kwa kuongeza uzalishaji wa homoni iitwayo gastrin ambayo huhusika na uzalishaji wa tindikali (acid)

* Huathiri kuta za tumbo kwa kuzalisha sumu zinazopelekea uzalishaji wa kemikali ya ammonia (Kwa lugha ya kawaida bakteria huyu hujikinga zaidi kwa kuzalisha urease)

VIDONDA VYA TUMBO VITOKANAVYO NA DAWA ZA MAUMIVU.

Dawa za maumivu hupelekea kuliwa kwa kuta za tumbo moja kwa moja
Dawa za maumivu hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa prostaglandin (ambayo hulinda kuta za tumbo), ni kwasababu dawa za maumivu huzuia cyclooxgenase( COX-1 na COX-2) isizalishe prostaglandin

COX-2 zipo mwili mzima na huhusika zaidi kwenye uzalishaji wa prostaglandin kwaajili ya kuongeza maumivu na homa.
COX-1 zipo kwenye tumbo, figo, utumbo mwembamba na chembe hai za platelets (zinazohusika na ugandaji wa damu)
- COX-1 na COX-2 zote huzalisha prostaglandin na kemikali nyingine za mwilini. Kumbuka prostaglandin hupelekea homa na maumivu lakini kwa wakati huo huo prostaglandin hio hio husaidia kulinda kuta za tumbo.
- Kwahiyo matumizi ya mara kwa mara ya dawa za maumivu hupelekea vidonda vya tumbo

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ambavyo husababishwa na bakteria H pylori na dawa hupelekea madhara yafuatayo;-

Damu kuvuja na kuvilia kwenye tumbo, kutobolewa kwa kuta za tumbo na utumbo, tumbo kujikunja au kujivilinga au tumbo kushindwa kupitisha chakula.

Kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo matumizi ya dawa za maumivu hupelekea madhara haya mara nne zaidi ya mtu ambae hana vidonda vya tumbo

Watu waliopo kwenye hatari ya vidonda vya tumbo ni k**a ifuatavyo
Yule mwenye historia ya vidonda vya tumbo
Mwenye umri mkubwa
Ambae ameathirika na bakteria H.pylori
Anaetumia dozi kubwa ya dawa za maumivu
Anaetumia dawa za maumivu pamoja na dawa za allergy tena kwa wingi
Anaetumia Aspirin
Anaetumia dawa za kulainisha damu au dawa za kuzuia damu kuganda

KITU CHA KUKUMBUKA; Ni uhusiano wa bakteria H.Pylori na vidonda vya tumbo

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili kubwa ya vidonda vya tumbo ni maumivu ya tumbo juu ya kitovu mara baada ya kula chakula (Vidonda vya tumbo la juu), wakati maumivu ya vidonda vya utumbo mwembamba hutokea kati ya masaa 2 hadi 5 baada ya kula chakula na maumivu wakati umelala
Maumivu haya hutoweka mara baada ya kula chakula, au kutumia dawa za antacids k**a magnesium na dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali k**a pantoprazole
Vidonda vya tumbo vya kudumu havina dalili kwasababu ya utumiaji mkubwa wa dawa za tumbo
Mgonjwa anaeonesha dalili zifuatazo husadikika kuwa na vidonda vya tumbo;-
Upungufu wa damu
Kutapika damu
Upungufu wa uzito
Maumivu ya kudumu juu ya tumbo
Maumivu makali kuelekea mgongoni

Kwa tiba dhidi ya ugonjwa huu ndani ya siku tano fika Amkeni Herbal Clinic Nane Nane -Mbeya au wasiliana nasi kwa simu 0676796421.

29/10/2019

HORMONE IMBALANCE MAANA YAKE NINI?

Hili neno unaweza kuwa ushawahi kuliskia mara nyingi au ushawahi kwenda hospitali na ukaambiwa una "Hormone Imbalance" lakini hukuwahi kujua ina maaana gani kwa kina.

Leo Amkeni Herbal Clinic tutafafanua kwa undani nini maana ya Hormone imabalance na athari zake ni zipi.

Katika mwili wa binadamu kuna mamilioni ya Hormone ambazo hufanya kazi zake katika kiwango maalumu na kwa uhitaji .hivyo basi hormone hizi zina kiwango chake maalumu ambacho hutakiwa kisipungue au kisizidi ili kuhakikisha shughuli zake haziathiriki.

Ikitokea hormone imeongezeka au imepungua ufanisi wake huathiriwa na yaweza kuathiri hormone zingine pia,kwa hiyo inapozungumziwa hormone imbalance inategemea ni hormone gani ambayo imeathiriwa.

Katika makala hii tutazungumiza hormone ya oestogen.

Zipo sababu mbali mbali ambazo zaweza kusababisha hormone kutobalance au kupishana.

1.msongo wa mawazo (Stress), 2.mfumo wa ulaji, 3.matumizi mbalimbali ya njia za uzazi wa mpango

ZIFUATAZO NI DALILI ZA KUA NA HORMONE IMBALANCE.

1.Kutokwa kwa mimba, 2.Kuongezeka uzito ghafla, 3.Wasiwasi, 4.Kukosa usingizi, 5.Maumivu au uvimbe kwenye maziwa, 6.Kupata kizunguzungu mara kwa mara, 7.Ugumba.

UPUNGUFU WA HORMONE YA OESTROGEN

Aina hii ya upungufu wa hormone ipo hasa hasa kwa wanawake wanaopitia ukomo wa hedhi kutokana na umri(menopause) na ikumbukwe kua wananwake wembamba hukumbwa sana na upungufu wa hormone hii ya oestrogen.

dalili za upungufu wa hormone ya Oestrogen ni .

1.Ukavu ukeni
2.maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa
3.Homa za vipindi
4.Kuvuja jasho usiku
5.Kujiskia mzito kufanya kazi
6.Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa

ONGEZEKO LA HORMONE YA OESTOGEN

hali hii hutokea kwa wanawake wanene sana na waliotumia vidonge au sindazo au vipandikizi za uzazi wa mpango
Na dalili za ongezeko la hormone ya Oestrogen ni k**a zifuatazo
1.Tumbo kujaa gesi
2.Mabadiliko ya hisia mara kwa mara
3.Wasi wasi au msongo wa mawazo
4.Kukosa usingizi
5.Vipele vyekundu usoni
6.Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.
7.Muamivu ya kichwa mara kwa mara

Kwa ushauri/ Tiba kuhusu Afya ya uzazi kwa mwanamke /Mwanaume fika Amkeni Herbal Clinic Nane nane - Mbeya au wasilina nasi kwa simu 0676796421.

MADHARA KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA PERIODKufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na ms...
20/10/2019

MADHARA KUFANYA TENDO LA NDOA WAKATI WA PERIOD

Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake,
Hii imeongelewa katika vitabu vya dini kua si vizuri kushiri tendo la ndoa pindi mwanamke akiwa katika siku zake,

Amkeni Herbal Clinic leo tutazungumzia athari ambazo unaweza kuzipata kwa kufanya mapenz wakati wa hedhi..,

MADHARA KWA MWANAUME.
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

2.Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.

3.Kuziba kwa njia ya mkojo.

4.Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu

MADHARA KWA MWANAMKE.

1.Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi k**a vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID (tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

2.Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).

3.Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

4.Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

Unaweza fika kituoni kwetu Nane Nane - Mbeya kwa ushauri na tiba dhidi ya magonjwa mbalimbali au wasiliana nasi kwa simu 0676796421.

MAMBO 10 YA KUTEGEMEA MIEZI 3 YA KWANZA YA UJAUZITO.Safari ya ujauzito ya miezi 9 ndio imeanza, wakati huu yamkini umesh...
19/10/2019

MAMBO 10 YA KUTEGEMEA MIEZI 3 YA KWANZA YA UJAUZITO.

Safari ya ujauzito ya miezi 9 ndio imeanza, wakati huu yamkini umeshapima na kuthibitishamimba yako. Mimba inapotungwa huleta mabadiliko mbalimbali ya kimwili na kisaikolojia kutokana na homoni za uzazi kuzalishwa kwa wingi zaidi. Mabadiliko haya hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, na pia kwa mwanamke mmoja katika nyakati tofauti.

Kipindi hiki cha miezi 3 ya mwanzo ya ujauzito hujulikana k**a first trimester na mjamzito huweza kupata mabadiliko yafuatayo ambayo huwa pia k**a dalili za mwanzo za ujauzito;
Kichefuchefu Na Kutapika Hasa Wakati Wa Asubuhi.

- Kichefuchefu na kutapika ni moja ya hali zinazojitokeza wakati wa mwanzo wa mimba. Kutapika huku huwa hasa wakati wa asubuhi na kuacha kadri siku inavyoenda. Hutokea kwa wanawake wengi wakati wa mwanzo wa ujauzito, na hupungua kadri mimba inavyokua. Ikiwa unatapika sana karibu siku nzima kila kitu unachokula basi onana na daktari mapema.

-Kukosa Hedhi.
Kukosa damu ya hedhi ni ishara mojawapo kuu ya ujauzito. Mimba inapotungwa, homoni huzuia ukuta wa mji wa mimba kubomoka na hivyo hedhi haitokei. Mara chache unaweza kutokwa na damu kidogo (matone kidogo kwenye nguo za ndani kwa siku moja au mbili). Kupata hedhi ya kawaida au kutokwa damu nyingi wakati wa ujauzito huashiria hatari ya ujauzito kutoka, hivyo ni muhimu kwenda hospitali mapema.

Kutokwa na Damu Kidogo Ukeni
Unaweza ukatokwa damu kidogo ukeni (matone kwenye nguo za ndani) kwa siku moja au mbili halafu ikaacha. Hutokea kwa baadhi ya wanawake kutokana na kiinitete (embryo) kujipandikiza katika mji wa uzazi. Hali hii ni ya muda mfupi na damu hutoka kidogo sana, na pia hutokea kwa baadhi ya wanawake.

Hali ya Kuchoka Haraka Zaidi ya Kawaida
Katika kipindi hiki cha mwanzo cha ujauzito, unaweza ukawa unapata hali ya uchovu mara kwa mara. Na hii inaweza kuwa uchovu wa kawaida au kuchoka sana zaidi ya kawaida (ukilinganisha na kipindi ambacho hakuwa na ujauzito).

- Kukojoa Mara kwa Mara.
Miezi ya mwanzo ya mimba, tumbo la uzazi huanza kukua na hivyo hukandamiza kibofu cha mkojo (kwa sababu mji wa mimba upo juu ya kibofu kidogo). Hali hii hufanya kibofu kijae mapema na hivyo kuleta hali ya kukojoa mara kwa mara.

- Kukosa Hamu kwa Baadhi ya Vyakula
Kutopenda aina fulani ya vyakula, vinywaji na baadhi ya harufu za vitu huweza kutokea kwa mjamzito. Mara nyingi hutokana na mabadiliko ya kihomoni mwiIini. wakati mwingine unaweza kuvutiwa na aina fulani za vyakula au vitu k**a barafu au udongo. Kuwa makini kupata vyakula vyenye lishe, epuka kula vitu k**a udongo.

- Kununa na Kukasirika (mood changes)
Hizi moods hubadilika mara kwa mara wakati mwingine .furaha, uchangamfu, na wengine inakuwa ni rahisi sana kumchukiza hata kwa kitu kidogo. Kuna wajawazito wengine hutokea kuwachukia wenzi wao pia. Hivyo ni muhimu kuwachukulia katika hilo.

Matiti Kuvimba na Kuuma
Mara nyingi mabadiliko ya kihomoni huchangia kuleta hali hii. Polepole matiti huanza kukua kujiandaa kutengeneza maziwa kwa ajili ya mtoto, mabadiliko haya huchangia kuleta hali ya matiti kuvimba na kuuma.

Mabadiliko katika Hamu ya Kufanya Mapenzi
Na hili pia hutokea, ikitofautiana kati ya wakati na wakati. Kuna wajawazito au wakati mjamzito anakuwa na mihemko mikubwa ya kimapenzi na wakati mwingine inakuwa kinyume kabisa. Ingawa inaweza isiwe kwa kiasi kikubwa katika miezi hii 3 ya mwanzoni.

- Mabadiliko ya Ngozi
Ingawa inaweza isikupate, mabadiliko ya ngozi hutokea hasa kutokana na mabadiliko ya kihomoni mwilini. Chunusi huweza kutokea.
Mabadiliko haya hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, hata siku kwa siku. Ukipata dalili zozote zinazokupa wasiwasi, onana na daktari wako haraka.

Amkeni Herbal Clinic tupo kwa ajiri yako kwa ushauri na tiba ya magonjwa mbalimbali, fika kituoni kwetu Nane Nane - Mbeya au waweza wasiliana nasi kwa simu 0676796421.

SABABU ZA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI AU KUJAA MAJI.Hdrosalpinx’ ni hali ambayo mirija ya uzazi ya mwanamke inakuwa inavimba ...
18/10/2019

SABABU ZA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI AU KUJAA MAJI.

Hdrosalpinx’ ni hali ambayo mirija ya uzazi ya mwanamke inakuwa inavimba kwa kujaa majimaji na inaziba upande wa mwishoni mwa mirija. Mirija hii inapovimba huwa na uvimbe k**a soseji, uvimbaji huu wa mirija na kuziba huwa wa pande zote mbili, kulia na kushoto. Tatizo hili la kuvimba na kuziba kwa mirija husababisha ugumba kwa mwanamke.
Pamoja na kujaa maji pia mirija inaweza kujaa usaha au kujaa damu

K**a tulivyokwishaona, tatizo hili huweza kumfanya mwanamke apoteze uwezo wa kuzaa yaani kuwa mgumba. Chanzo kikuu cha hali hii ni maambukizi katika viungo vya uzazi, ‘Pelvic Inflammatory Disease’ au kwa kifupi ni ‘PID’.
Maambukizi haya hupanda taratibu na huanzia ukeni. Kwa hiyo mwanamke anayesumbuliwa na tatizo la maambukizi ya mara kwa mara ukeni ni vema atibiwe vinginevyo baadaye anaweza kujikuta anashindwa kupata ujauzito.

Dalili za maambukizi ya mara kwa mara ukeni ambayo yanaweza kukufanya ukose uwezo wa kuzaa kwa kupata tatizo hili la ‘Hydrosalpinx’ ni kutokwa na uchafu au majimaji ukeni yenye harufu mbaya na muwasho, maumivu ukeni, maumivu wakati wa kujamiiana na kuhisi uvimbe ukeni k**a gololi.

Unaweza fika Amkeni Herbal clinic Nane Nane-Mbeya kwa ushauri na tiba au wasiliana nasi kwa simu namba +255676796421.

Address

Nane Nane
Mbeya

Opening Hours

Monday 08:00 - 18:00
Tuesday 08:00 - 18:00
Wednesday 08:00 - 18:00
Thursday 08:00 - 18:00
Friday 08:00 - 18:00
Saturday 08:00 - 18:00

Telephone

+255676796421

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Amken Herbal Clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category