20/10/2024
RC Kagera azindua Kampeni ya "Wasitiri."
- BIBI CARE kuja na taulo za k**e za migomba
MKUU wa mkoa wa Kagera, Bi Fatma Mwassa, amezindua kampeni ya Wasitiri inayolenga kutoa elimu ya hedhi salama na kuhamasisha upatikanaji wa taulo za hedhi kwa ajili ya kuwasitiri maelfu ya wanafunzi wasichana nchini, ikianzia mkoa wa Kagera.
Kampeni hiyo inayotekelezwa na Shirika la BIBI CARE kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ilizinduliwa jana Jumamosi katika ukumbi wa KCU, mjini Bukoba katika tamasha la Huruma ya Mungu lililosheheni burudani ya kwaya mbalimbali kutoka nchini na nchi jirani ya Uganda.
Akizindua kampeni hiyo, Bi Mwassa alisema uhitaji wa taulo za k**e ni mkubwa kuliko inavyofikiriwa, kwani yeye binafsi aliwahi kufanya kampeni iliyotoa misaada ya shuka, vyandarua, sare za shule, viatu vya ngozi, soksi, madaftari, kalamu na taulo za k**e kwa wasichana wa shule za bweni, lakini alipowarudia kuhoji wamefurahia nini zaidi, wanafunzi wengi walitaja taulo za k**e.
"Yaani umempa binti shuka mbili, chandarau, sare za shule, viatu vya ngozi, soksi, madaftari na kalamu, lakini anakwambia amefurahia zaidi taulo za k**e. Hii inaashiria kwamba uhitaji wa taulo za k**e ni mkubwa zaidi kuliko tunavyofikiria," alisema Bi Mwassa.
Awali, Mwenyekiti wa BIBI CARE, Edward Kinabo, alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya kampeni ya "Wasitiri," shirika hilo pamoja na wadau wake, wamejipanga kutoa elimu na kusaidia taulo za k**e kwa wanafunzi ili kupunguza tatizo la baadhi yao kukosa masomo kwa sababu ya kushindwa kujisitiri wakati wa hedhi.
Alisema utafiti wa UNICEF uliofanyika kwenye wilaya 19 nchini ulithibitisha kuwa asilimia 16.8 ya wanafunzi wa k**e wanakosa masomo wakiwa katika siku zao za hedhi, huku akiweka angalizo kuwa k**a ukifanyika utafiti mpana zaidi wa ngazi ya taifa basi huenda tatizo hilo likaonekana kuwa kubwa zaidi kuliko lilivyoonekana kwenye wilaya 19 zilizofanyiwa tafiti.
Akigusia awamu ya pili ya kampeni hiyo, Kinabo amesema ili kuhakikisha upatikanaji endelevu na nafuu wa taulo za k**e, BIBI CARE imejipanga kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana kumiliki na kuendesha viwanda vidogo vya kuzalisha taulo za k**e za kutengenezwa kwa kutumia nyuzi za mgomba.
"Kagera mnalima ndizi. Tunakwenda kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Taulo za k**e za mgomba zitaleta fursa ya kutengeneza vipato kwa wakulima wa zao la ndizi na wakati huo huo tutakuwa tumechangia upatikanaji endelevu na nafuu wa taulo za k**e. Tutahakikisha taulo hizo zinakidhi viwango vya ubora na kupata ithibati ya TBS," alisema Kinabo.