04/01/2023
TUJIFUNZE KUHUSU ULAJI WA NANASI WAKATI WA UJAUZITO.
👉JE, Ni kweli nanasi Halifai kuliwa wakati wa ujauzito?
Ni swali ambalo Wajawazito na watu wengi hulijadili na kutoa maoni mbalimbali kuhusu tunda hili, karibu ujifunze pamoja nami.
👉Nanasi Ni tunda zuri linalosaidia Kuongeza Kinga ya mwili, kutibu mafua, kupambana na saratani, kuondoka Maumivu pamoja na kulinda moyo.
👉Kwa mujibu wa USDA nanasi huundwa kwa maji, nishati, protini, wanga, nyuzilishe na Aina mbali mbali za Sukari na folate, pia Lina vitamin C pamoja na madini chuma, Calcium , potassium , magnesium pamoja na phosphorus
👉Licha ya Faida hizi zote tunda hili huusishwa na kuharibu Ujauzito mchanga kwa wanawake na Jambo Hili hutokana na uwepo wa vimeng'enya vya bromelain ambavyo kiasili hupatikana kwenye nanasi pekee
👉 Bromelain Ni Nini hasa?? ,Hili Ni kundi kubwa la vimeng'enya vunavyopatikana kwenye tunda la nanasi, na kazi kubwa ya Bromelain Ni kusaidia mmeng'enyo wa vyakula vyenye asili ya protini, Husaidia kutibu changamoto za mfumo wa upumuaji kwa kupambana na maambukizi ya bakteria na virusi, Husaidia kuondoa Maumivu ya mwili hasa Yale yanayotokea kwenye maungio ya mifupa , kuvimba kwa tishu pamoja na baridi yabisi, huzuia kuongezeka kwa shinikizo la juu la damu , kiharusi, shambulio la moyo pamoja na kuzuia kuganda kwa damu kwenye mishipa na hupambana na bakteria wabaya hasa wale wanaosababisha magonjwa ya kunywa , uzazi na mfumo wa chakula nk
👉Matumizi ya Vidonge vya Bromelain wakati wa ujauzito hayashauriwi kwa sababu vinaweza kumfanya apoteze damu nyingi pamoja na kuharibu Ujauzito
👉Lakini Kiasi Cha Bromelain Kinachopatikana kwenye nanasi Ni kidogo Sana kuweza kuleta athari zozote kwa Ujauzito , pia Hakuna tafiti za kisayansi zinazothibitisha madhara ya nanasi kwa binadamu hivyo nanasi linabaki kuwa tunda Bora Sana kwa wanawake Wajawazito.
👉Ili kufikia kiwango Cha kidonge kimoja Cha Bromelain ambacho kina madhara mjamzito anahitajika kutumia mananazi 10 kwa wakati mmoja, lakini Ulaji wa kawaida wa nanasi Ni salama kabisa kwa kipindi chote Cha Ujauzito wako.
Imeandialiwa
mtaalamu