
30/04/2022
JINSI YA KUTUMIA VIASHIRIA VYA HEDHI ILI KUTAMBUA UWIANO WA HOMONI ZAKO.
Hapa chini nimeelezea uhusiano kati ya viashiria hivi na homoni zako. Lengo langu ni kukuonesha namna ya kuusoma mwili na kuusikiliza pale unapoeda nje ya mstari. Mzunguko wa hedhi ni njia muhimu ya kuusoma mwili kuhusu uwezo wa kushika mimba.
1. Kukosa hedhi
Kukosa hedhi mara moja inaweza isiwe tatizo. Mpangilio wa homoni ni kitu sensitive sana na kinaweza kuathiriwa tu na msongo wa mawazo, lakini kwa kiasi kikubwa unaweza kujirekebisha wenyewe. Kukosa hedhi pekee siyo kiashiria kwamba hutaweza kushika mimba, manake yawezekana mayai yanatolewa(ovulation) lakini usipate hedhi. Kukosa hedhi kwa zaidi ya miezi 6 huitwa Amenorrhea na inaashiria kuna tatizo ambalo unahitaji kumwona Dactari haraka.
2. Period fupi
Mzunguko mfupi unaweza kuleta matatizo kwenye uwezo wa kushika mimba. Baadhi ya vihatarishi ambavyo hufupisha mzunguko wako ni k**a kukosa ovulation, upungufu wa virutubisho mwilini, uzito mdogo sana, upungufu wa damu .
3. Period ndefu
Mzunguko mrefu wa hedhi unaweza kuashiria kuvurugika kwa homoni na yai kutotolewa kwa yai kwenye kikonyo chake. Homoni ya progesterone ambayo hutolewa na mwili husaidia kuzuia bleed kuemdelea. K**a estrogen ni nyingi na progesterone ni kidogo bleed inaweza kuendelea kwa siku nyingi zaidi kuliko kawaida
4. Hedhi nzito na nyingi zaidi.
Kupata hedhi nzito na nyingi kupita kiasi husababishwa na ukuta wa uterus kusisimka zaidi kutokana na wingi wa estrogen, inapelekea ukuta kumomonyoka kupita kiasi. Tatizo hili linaweza kurekebishwa kwa kurekebisha lishe yako na kutumia tiba ya mimea kwa ajili ya kurekebisha homoni. Upungufu wa vitamin A na C inaelezwa kuchangia bleed nzito. unaweza kutumia Virutubisho k**a Multivitamin.
5. Hedhi kidogo inayoambatana na maumivu makali ya tumbo.
K**a unapata hedhi nyepesi, nyekundu inaweza kuashiria kwamba mzunguko kwenye mfuko wa mimba ni mdogo. Unaweza kupunguza hali hii kwa kufanya masaji kwenye eneo la tumbo ukitumia mafuta ya castor,ama kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya moto.
6. Hedhi ya damu nyekundu inayong’aa.
K**a hedhi yako inakuwa ni damu nyekundu inayong’aa basi hakuna tatizo endelea kufurahia hedhi yako.
Hedhi nzito yenye weusi ama brown
Hii inaonesha kwamba kuna masalia ya damu ya zamani kwa hedhi iliyopita. Kubaki kwa damu husababishwa na utokaji wa polepole sana na mzunguko mdogo ndani ya mfuko wa mimba. Unaweza kurekebisha tatizo hili kwa kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha, kufanya masaji eneo la tumbo.
7. Hedhi yenye damu mpauko na maji zaidi.
K**a unapata hedhi ya namna hii inaonesha kwamba damu yako kiujumla haina ubora na inakosa virutubishi muhimu. Kula lishe nzuri husaidia unaweza pia kutumia virutubishi vingine k**a Multivitamin na Spiriluna kuimarisha damu yako.
8. Kuganda kwa damu ya hedhi.
Kuganda kwa damu ya hedhi inaweza kuwa siyo jambo na kutisha ukilinganisha na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu. Lakini yatakiwa kuendelea kufatitilia hedhi yako pia. K**a kuganda kwa hedhi yako kunatokea mara chache hasa mwanzoni mwa period, ni mabonge madogo madogo, yenye rangi nyekundu inayong’aa basi ni salama. Lakini k**a unapata mabonge mabubwa na inakuwa mfululizo basi yahitaji kumwona Daktari kupata ushauri. Unatakiwa kumwona Daktari haraka kwani kupata Damu nzito yenye mabongemabonge k**a unahisi unaweza kuwa na ujauzito yaweza kuashiria kwamba mimba imeharbika.Tumia maji ya kutosha na kufanya masaji eneo la tumbo kwa kutumia mafuta ya nyonyo (castor) ili kupunguza tatizo hili.
9. Kupata bleed kwenye kipindi kisichokuwa na hedhi.
Bleed katikati ya vipindi vya hedhi ni tatizo linalowachanganya sana wanawake. Yaweza kusababishwa na kuvurugika kwa mpangilio wa homoni (rejea maelezo yangu pale juu)Yai kutotolewa kwenye kikonyo chake(ovulation),
Uvimbe unaotokana na kukua kupita kiasi kwa tishu laini za ukuta wa uterus(endometriosis),Matumizi ya dawa za kupanga uzazi, Mazoezi magumu naLishe duni
10. Kukosa kabisa hedhi(Amenorrhea)
Inaweza kutatiza pale ambapo unashika ujauzito lakini hupati hedhi kabisa. Kuwa na mzunguko mzuri ni hatua ya kwanza katika kujua kwamba unaweza kushika ujauzito. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuchangia hedhi yako kuvurugika k**a msongo wa mawazo, lishe duni, uzito mdogo sana, kutumia vidonge vya kuzuia mimba, kuvurugika kwa homoni, umri kwenda (kukaribia menopause) na matatizo mengine ya kiafya.