28/01/2021
TATIZO LA KUSHINDWA KUMUDU TENDO LA NDOA (S*XUAL DISFUNCTION) KWA WANAUME NA WANAWAKE
Mtayarishaji ni: Dr. Sophon, MD
Mawasiliano: 0744 996 795 (WhatsApp)
Ndugu msomaji wa makala haya ya Afya ninapenda kukukaribisha ili ujifunze mambo mbali mbali yanayohusiana na suala zima la tendo la ndoa kitaalamu zaidi. Nipende tu kusema makala haya hayana lengo la kuhamasisha ufanyaji wa mapenzi kiholela wala haitabeba lawama yoyote. Lengo kuu la Makala haya ni kuelimisha jamii na sio kutangaza biashara ya mtu yeyote yule. EPUKA NGONO ZEMBE ISHI SALAMA.
Tatizo la kushindwa kumudu tendo la ndoa (s*xual dysfunction) ni pale ambapo mtu (mwanaume / mwanamke) anaposhindwa kuwa aidha na hamu ya kufanya tendo la ndoa au kushindwa kufurahia tendo la ndoa. Tatizo hili huwapata wanaume na wanawake pia, japokuwa imezoeleka kwenye jamii zetu kwamba matatizo haya huwakumba wanaume tu tatizo linalojulikana zaidi k**a ukosefu wa nguvu za kiume. Leo hii nataka ubadilishe mtazamo kwamba wanawake pia hupatwa na tatizo hili la s*xual dysfunction. Tatifi za hivi karibu zinaonesha karibu asilimia 40 (approximately 40%) ya wanawake kote duniani wanakumbwa na tatizo la ufanisi wa tendo la ndoa inayotokana na matatizo binafsi (interpersonal distress) japo huwa haiongelewi sana k**a tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Wanaume na wanawake wa kila umri huathiriwa na tatizo hili japokuwa tafiti nyingi zinaonyesha tatizo hili ni kubwa kwa watu wenye umri mkubwa (wazee) na pia tatizo hili huongezekana kadiri umri unavyoongezeka.
Kwa lengo la kukuza uelewa wako msomaji wangu ningependa tujadili matatizo haya ya kushindwa kumudu tendo la ndoa katika makundi makuu mawili ambayo ni
1. Kwa wanaume (upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume)
2. Kwa wanawake
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME (S*XUAL DISORDERS) KWA WANAUME
Watu wengi wanaposikia upungufu wa nguvu za kiume hudhania kwamba ni kushindwa kutungisha mimba. La hasha! upungufu wa nguvu za kiume ni zaidi ya hiyo na pia sio wakati wote mtu mwenye upungufu wa nguvu za kiume atashindwa kutungisha mimba. Unaweza pia ukawa huna tatizo la nguvu za kiume na bado ukaishia kushindwa kumpa mwanamke ujauzito. Tunaposema s*xual disorders, ni Jumla ya matizo mengi sio kitu kimoja. Ndani ya upungufu wa nguvu za kiume kuna mambo makuu manne k**a ifuatavyo:
♣ Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa (hypoactive s*xual desire disorder)
♣ Kushindwa kusimamisha uume wakati wa tendo la ndoa (Erectile dysfunction)
♣ Kuwahi kufika kileleni au kukojoa (Premature ej*******on)
♣ Kuchelewa kufika au kutofika kileleni (Delayed ej*******on)
Suala zima la tendo la ndoa lina hatua (phases) kuu nne inayojulikana k**a Sexual Response Cycle.
HATUA YA KWANZA: Hatua ya matamanio (Desire Phase)
HATUA YA PILI: Hatua ya msisimko (Excitation Phase)
HATUA YA TATU: Hatua ya kileleni (Ogasmic Phase)
HATUA YA NNE: Hatua ya kujirudi kwenye hali ya kawaida (Resolution Phase)
Hatua hizi nne katika hali ya kawaida hupaswa kwenda kwa muda Fulani na kumalizika kwa muda fulani. Hatua hizi ni k**a mnyororo (chain) ulivyo, tatizo likitokea mahali popote katika mnyororo huu hupelekea kutokea kwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Hivyo basi, mwanaume mwenye tatizo la nguvu za kiume haina maana kwamba ana matatizo yote manne yaliyoorodheshwa hapo juu.
Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume wengi hutamani tendo la ndoa zaidi ya wanawake. Na wengi wao hutumia muda mwingi kufikiri kuhusu jambo hili kuliko wanawake. Licha ya hivyo, kuna kundi kubwa la wanaume wasiokuwa na matamanio ya kufanya tendo la ndoa (decreased libido).
VISABABISHI VYA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
Upungufu wa nguvu za kiume husababishwa na mambo mengi sana k**a ninavyoeleza hapa chini:
1. Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa (decreased libido): tatizo hili hukadiriwa kuwa asilimia 5 hadi 15 ya wanaume. Huongezeka kadiri umri unavyoongezeka. Miongozi mwa visabibishi ni:
- Matumizi ya dawa k**a vile za sonona (SSRIs), maumivi (opioids) n.k
- Unywaji wa pombe
- Sonona (depression)
- Uchovu (fatigue)
- Matumizi ya dawa za kulevya
- Upungufu wa homoni za kiume (testosterone)
- Magonjwa mbali mbali k**a kisukari, shinikizo la juu la damu (pressure)
Visababishi vingi hapa hutibika hivyo ni vema ukaenda kuonana na daktari.
2. Kushindwa kusimamisha uume (Erectile dysfunction): Hili ni tatizo sugu (common s*xual problem) kwa wanaume miongoni mwa matatizo yote manne ya upungufu wa nguvu za kiume. Husababishwa na:
- Umri (uzee)
- Kisukari (DM)
- Shinikizo la juu la damu (Hypertension)
- Uzito uliopindukia au kiribatumbo (obesity)
- Kuzidi kwa mafuta mwilini (dyslipidemia)
- Upungufu wa hormone za kiume (testosterone)
- Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (cardiovascular disease)
- Uvutaji wa sigara
- Matumizi ya dawa k**a zile za kutibu sonona (antidepressants i.e SSRIs), methyldopa, clonidine, spironolactone n.k
- Magonjwa ya figo (chronic kidney disease)
- Upasuaji wa tezi dume (Radical Prostatectomy)
- Magonjwa ya misuli ya uume (carvenous diseases) k**a vile Peyronie’s disease, carvenous fibrosis na pe**le fracture.
- Magongwa yanayoathiri mfumo wa fahamu (neurologic) k**a vile ajali za uti wa mgongo na ubongo, ugonjwa wa kutetemeka (Parkinson disease), ugonjwa wa kusahau (Alzheimer disease) na multiple sclerosis
- Tatizo la kisaikolojia (Psychogenic) mfano Historia mbaya ya matukio ya nyuma (Post-Traumatic Stress Disorder), msongo wa mawazo (stress), sonona (depression), changamoto za mahusiano, hofu (anxiety) n.k
3. Kuwahi kufika kileleni au kukojoa (Premature ej*******on): Hii hutokea pale ambapo mwanaume hukojoa (ej******es) kabla au ndani ya dakika moja ya kuingiza uume kwenye uke. Wanaume wengi wenye tatizo hili mara nyingi huwa na tatizo la ugumba (kushindwa kumpa mwanamke mimba). Kisababishi kikuu hakijulikani ingawaje kuna mambo kadhaa yanayochangia kukojoa haraka k**a vile:
- Matatizo ya kisaikolojia k**a msongo wa mawazo, historia mbaya ya unyanyasaji wa kingono (s*xual abuse), kukosa kujiamini (impaired self-body image), na hofu wakati tendo la ndoa (performance anxiety).
4. Kuchelewa au kutofika kileleni au kukojoa (Delayed ej*******on/anej*******on): wako wanaume wanochelewa kukojoa na wapo wengine ambao hawakojoi kabisa. Sababu nyingi ni hizo nilizozitaja hapo juu pamoja na matatizo ya kisaikolojia, ajali au oparesheni zinazohusisha mfumo wa fahamu na uti wa mgongo.
MATIBABU
Matibabu ya upungufu wa nguvu za kiume hutegemeana na aina ya kisababishi cha upungufu wa nguvu za kiume na aina ya tatizo la nguvu za kiume. Mengine huhitaji ushauri wa kisaikolojia, matibabu ya dawa na upasuaji wa kurekebisha misuli ya uume. Makala haya hayajakusudiwa kutoa dawa au kuchukua mbadala wa daktari, hivyo ninakushauri nenda kamuone daktari ukiwa na tatizo lolote.
TATIZO LA KUSHINDWA KUMUDU TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE (S*XUAL DYSFUNCTION IN WOMEN)
K**a nilivyotangulia kusema hapo awali tatizo hili kwa upande wa wanawake halijulikani sana na wala halisemwi sana k**a upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume. Jambo hili pia limesababisha lawama kutupwa kwa wanaume kwamba wao ndiyo wenye matatizo lakini tafiti nyingi zinaonyesha asilimia 40 (maana yake ni kwamba kati ya wanawake kumi kuna wanne wenye tatizo hili) ya wanawake kote ulimwenguni wana tatizo la kushindwa kufurahia tendo la ndoa. K**a ilivyokuwa kwa wanaume, kwa wanawake pia kuna makundi manne yanayopelekea kushindwa kumudu au kufurahia tendo la ndoa:
♣ Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa (s*xual interest or desire disorder)
♣ Kushindwa kusisimka au kushika moto (Arousal disorder)
♣ Kushindwa kufika kileleni (Or****ic disorder)
♣ Maumivu wakati wa tendo la ndoa (Painful Pe*******on disorder)
Maumivu wakati wa tendo la ndoa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya wanawake jambo linalopelekea hata kukosa hamu ya kufanya au kufurahia tendo la ndoa. Maumivu haya sio yale yanasababishwa na ugonjwa k**a chango la uzazi (Pelvic Inflammatory Disease, PID) bali ni yale maumivu yanayotokea bila uwepo wa ugonjwa wowote kwenye mfumo wa uzazi au mfumo wa mkojo. Kukosa mood ya kufanya tendo la ndoa ni kawaida kabisa kwa kila mtu lakini inapotokea tatizo hili limedumu kwa muda mrefu (walau miezi sita) ndipo kuna haja ya kumuona Daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kuna usemi unaosema kwamba mwanamke ni k**a chungu huchelewa kushika moto na pia huchelewa kupoa. Ni ukweli usiopingika kwamba mwanaumke huhitaji kuandaliwa kabla ya tendo la ndoa kwa kigezo hiki cha chungu lakini wapo wanawake ambao hawashiki moto kabisa na hawafiki kileleni kabisa kutokana na matatizo mbali mbali k**a tutakavyona hapo chini.
Tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa (low libido) ndiyo tatizo kuu miongoni mwa wanawake wengi. Wanawake wengi wenye tatizo hili hukosa hamu au hata mawazo ya kufanya mapenzi. Tatizo hili huwakumba wanawake wa rika zote.
VISABABISHI VYA KUSHINDWA KUMUDU AU KUFURAHIA TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE.
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa upungufu wa homoni ya k**e iitwayo Estogen hupelekea mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa. Upungufu hutokea mara nyingi kwa wanawake waliopita umri wa kuzaa (postmenopose) lakini pia huweza kutokea kwa wale walio katika umri wa kuzaa (reproductive age). Miongoni mwa visababishi kwa wanawake ni k**a ifuatavyo:
1. Matatizo ya kisaikolojia k**a vile; sonona, hofu (anxiety), mawazo, ukosefu wa usiri (lack of privacy) au mazingira rafiki kwa tendo la ndoa, historia mbaya ya matukio ya nyuma (posttraumatic stress disorder) k**a vile ubakaji na unyanyasaji wa kingono, n.k
2. Matatizo ya kimahusiano (relationship factors) k**a vile, ugomvi,
3. Uchovu na mawazo
4. Umri wa mwanamke (wale wenye umri mkubwa)
5. Magonjwa ya akili
6. Mimba na baada ya kutoka kujifungua
7. Magonjwa k**a vile kisukari, hyperthyroidism, hyperprolactinemia, pressure/shinikizo la damu,
8. Matumizi ya dawa za kupanga uzazi hasa zile zenye homoni (hormonal contraceptives), dawa za pressure, matumizi ya dawa za kulevya k**a ni****ne, n.k
9. Mengine k**a vile, kutokujiamini na kujiona k**a unaupungufu kwenye mwili wako (poor body image), uzito mkubwa (obesity).
10. Magonjwa ya uzazi k**a vile PID, endometriosis, uvimbe kwenye kizazi (fibroids) n.k
MATIBABU:
Matibabu ya matatizo haya kwa wanawake pia itategemea na kisababishi cha tatizo. Miongoni mwa njia zinazotumika kutibu matatizo haya ni ushauri wa kisaikolojia, kubadili mtindo wa maisha, dawa, na upasuaji.
Kwa tatizo la kukosa hamu ya mapenzi, wanawake wengi hushauriwa kubadilisha wapenzi (japokuwa sio vizuri kimaadili ya dini) k**a tatizo limetokana na migogoro ya kimapenzi. Tatizo la kukosa hamu ya mapenzi huletwa na kuzoeana kwenye ndoa. K**a chanzo ni hiki wanandoa hushauriwa kujipa likizo kidogo ya kujitenga na wenza wao ili kurudisha hamu, kubadilisha style ya kufanya mapenzi, kubadilisha muda wa kufanya mapenzi au kufanya mapenzi sehemu tofauti na ilivyozoeleka mfano sebuleni, guesthouse, shambani n.k
MWISHO, K**a umependa Makala haya usisite ku-like na ku-share ukurasa (page) yangu ya facebook. Nenda kwenye Facebook tafuta doctor WANGU AFYA YANGU kisha unifuatilie kwa ajili ya elimu mbali mbali za afya.
Ahsanteni.