07/10/2021
Wiki iliyopita, tarehe 30.09.2021, Kituo cha Ushauri wa Kisaikolojia - Nyakato kilitoa semina kwa wakufunzi 23 toka mradi wa Lulu Project unaotoa huduma kwa vijana wakike jijini Mwanza kuwafundisha masomo ya maisha, afya na biashara.
Semina ilihusu Mawasiliano bila Ukatili (MbU) au kwa kingereza Nonviolent Communication (NVC) ambayo ni mfuma wa mawasiliano unaosaidia watu kuelewana vizuri na kutatua migogora yao. Lengo la msingi ya MbU ni mawasiliano ya moyo kwa moyo, kwa upendo na bila lawama.
Katika mfumo wa MBU wahusika hueleza
a) nini kamili kimetokea kilichowakwaza?
b) walijisikiaje?
c) wana mahitaji gani?
d) sasa wanaomba nini kutoka kwa wenzao?
Sisi washauri wa kisaikolojia tulifurahi sana kuona ushirikiano mkubwa wa wajumbe wa semina, wakufunzi wa Lulu Project.
Tunawakatia makufunzi wa Lulu Project kila la heri katika kutumia na kufundisha MBU!