18/09/2022
*Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni nini?*
Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke au ugonjwa wa PID (pelvic inflammatory disease) ni maambukizi ya bakteria kwenye shingo ya uzazi, mirija ya fallopio, ovari na tumbo la uzazi (uterasi).
Sababu kuu ya ugonjwa huu kutokea ni maambukizi yanayosambazwa kwa kujamiiana (STI). Ugonjwa huu unaweza kuwaathiri wanawake wenye umri wowote, lakini wale wenye umri kati ya maika 15 na 24 huathirika zaidi.
Utambuzi na matibabu ya mapema ni muhimu katika kuzuia madhara ya kupata makovu na utasa.
Vihatarishi vya ugonjwa wa PID
Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke ni semi ya kitabibu inayoelezea maambukizi ya shingo ya uzazi, tumbo la uzazi na mirija ya fallopio. Kwa kawaida maambukizi haya husababishwa na bakteria.
Ingawa mara nyingi ni maamkubizi yanayosambazwa kwa njia ya kujamiiana (STI), k**a vile klamidia au kisonono, wakati mwingine maambukizi haya huweza kusababishwa na bakteria wengine. PID inaweza kuwaathiri wanawake wenye umri wowote,
Dalili za PID huweza kujumuisha:
Maumivu kwenye nyonga na tumbo
Maumivu wakati wa kujamiiana
Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi
Kutokwa na majimaji yasiyo ya kawaida ukeni
Baadhi ya watu huweza kupata homa, kichefuchefu, kutapika au maumivu wakati wa kujisaidia.
Utambuzi.
Utambuzi mara nyingi huweza kufanywa kulingana na dalili na uchunguzi wa sehemu za siri. Wakati wa uchunguzi, sampuli za majimaji au usaha huchukuliwa ili kutambua bakteria anayesababisha maambukizi.
Matibabu (PID treatment)
Maambukizi ya via vya uzazi vya mwanamke hutibika na hutofautiana kulingana na ukali wa maambukizi.
kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kupiyia namba +255 785 759 296