Jari Afya yako na Dr.Bugota

  • Home
  • Jari Afya yako na Dr.Bugota

Jari Afya yako na Dr.Bugota Elimu juu ya afya

NAMNA RAHISI YA KUJIKINGA NA BAWASIRI(Hemorrhoids) Bawasiri ni vinyama vinavyojitokeza kwenye njia ya haja kubwa baada y...
01/01/2022

NAMNA RAHISI YA KUJIKINGA NA BAWASIRI(Hemorrhoids)

Bawasiri ni vinyama vinavyojitokeza kwenye njia ya haja kubwa baada ya mishipa ya damu inayosambaza kwenye eneo hilo kulegea kutokana na sababu mbalimbali

NJIA ZA KUJIKINGA NA BAWASIRI.
1.Kuepuka kufanya kazi nzito kwa muda mrefu mfano kunyanyua mizigo ya magunia, cement
2.Kuepuka uzito wa mwili uliopitiliza
3.Kunywa maji ya kutosha
4.Kula mlo kamili ukihusisha matunda k**a papai, ndizi ili kusaidia katika mmen'genyo wa chakula na kupata choo laini
5.Kuacha kushiriki ngono kinyume na maumbile
6.Kuepuka kukaa kwa muda mrefu sana
7.Pia kikohozi cha muda mrefu bila matibabu kinaweza kupelekea kupata bawasiri

Authored by Dr Bugota
Afya Yako ndio msingi wa maisha yako
#0759424664 #

SARATANI YA SHINGO YA UZAZI(Cervical CA) Hii ni saratani inayotokea katika shingo ya uzazi ya mwanamke yaani cervix, mar...
31/12/2021

SARATANI YA SHINGO YA UZAZI(Cervical CA)

Hii ni saratani inayotokea katika shingo ya uzazi ya mwanamke yaani cervix, mara nyingi huwapata wanawake wenye umri kuanzia miaka 55 na kuendelea lakini pia inaweza kutokea chini ya umri huo, maambukizi au saratani hii wanawake huipata katika umri mdogo ila dalili huanza kujionyesha katika umri mkubwa.

VITU VINAVYOWEZA KUPELEKEA MWANAMKE KUPATA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI.
1.Kuanza kushiriki ngono katika umri mdogo
2.Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
3.Kuwa na magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na virusi vya HPV
4. kushiriki ngono na mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara
5.Kinga ya mwili kupungua mfano mwenye maambukizi ya VVU.
6.Kuzaa watoto wengi mfano kuanzia watoto 8 na kuendelea yupo kwenye hatari ya kupata saratani ya shingo ya uzazi
7.Uvutaji wa sigara kwa mwanamke

DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI.
- Mwanamke kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa
- Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi
- Kuendelea kutokwa na damu baada ya kufikia ukomo wa hedhi yaani kuanzia miaka 50 na kuendelea
- Kutokwa na uchafu sehemu za siri unaoweza kuwa umechanganyikana na damj
- Kuumwa tumbo la chini
- Kutokwa na damu njia ya haja kubwa
- Kukojoa mkojo umechanganyikana na damu

NJIA ZA KUJIKINGA NA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI.
1.Kuchoma chanjo ya virusi vya HPV
2.Wasichana kuepuka kuanza ngono katika umri mdogo
3.Kuepuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
4.Kupata matibabu ya haraka ya magonjwa ya zinaa
5.Kuacha kuvuta sigara
6.kushiriki ngono salama kwa kutumia Kinga.

JE UNAYAFAHAMU MADHARA YANAYOTOKANA NA UTOAJI MIMBA (ABORTION) Abortion ni kitendo cha utoaji au mimba kutoka ikiwa chin...
25/12/2021

JE UNAYAFAHAMU MADHARA YANAYOTOKANA NA UTOAJI MIMBA (ABORTION)

Abortion ni kitendo cha utoaji au mimba kutoka ikiwa chini ya wiki 28 tangu mimba kutungwa.

Kuna aina mbili za Abortion
1.Spontaneous abortion -Hiki ni kitendo cha mimba kutoka yenyewe kutokana na kasoro za kimaumbile, maambukizi katika via vya uzazi na mwili kiujumla, pamoja na magonjwa k**a Kisukari.

2.Induced abortion-Kitendo cha kutoa mimba kwa kudhamiria ikihusisha utumiaji wa dawa za kutolea mimba, upasuaji na kutumia vifaa kwa lengo la kutoa mimba

Wapo watu ambao mimba hutoka kwa shida za kiafya na kasoro za kimaumbile lakini wapo ambao hutoa mimba kwa kudhamiria wakiangalia maslahi yao binafsi, kushinikizwa, hofu ya kuwa wataonekanaje katika jamii na sababu mbalimbali lakini ni kutokana na maamuzi wanayochukua.

MADHARA YA KUTOA MIMBA.
- Kutokwa na damu nyingi shida ambayo inaweza kupelekea kifo kwa mhusika
- Upungufu wa kiwango cha maji mwilini(shock) kutokana na upotevu wa damu nyingi
- Maambukizi ambayo yanaweza kuletwa kwa kutumia njia zisizo salama kutoa mimba
- Maambukizi katika via vya uzazi yanayoweza kupelekea shida ya mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi
- Kushindwa kupata mtoto kwa sababu ya maambukizi na uharibifu wa via vya uzazi
- Kupata maumivu ya muda mrefu katika via vya uzazi

LUNG CANCER(KANSA YA MAPAFU)Kansa ya mapafu ni kansa inayotokea kwenye mfumo wa upumuaji wa mwanadamu yaani mapafu,na in...
09/09/2021

LUNG CANCER(KANSA YA MAPAFU)

Kansa ya mapafu ni kansa inayotokea kwenye mfumo wa upumuaji wa mwanadamu yaani mapafu,na inaweza kusambaa kuelekea kwenye ogani nyingine za mwili,Kansa hii huwapata wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea na ni vugumu sana kutokea kwa vijana.

WATU WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA KANSA YA MAPAFU.
1.Wavutaji wa sigara
2.Watu wanaokaa kwenye mazingira ya wavutaji sigara/wanavuta moshi wa sigara hata k**a wao sio wavuta sigara
3.Watu wanaofanya kazi migodini/gesi na kemikali zinazotumika migodini
4.Watu waliowahi kupata huduma ya mionzi kifuani(radiation therapy)
5.Kuwa na ndugu aliyewahi kupata kansa ya mapafu.

DALILI ZA KANSA YA MAPAFU.
1.Kukohoa damu
2.Kikohozi cha muda mrefu
3.Kifua kuuma
4.Kupata shida ya kupumua
5.Kupungua uzito wa mwili kwa kasi
6.Kupoteza hamu ya kula
7.Mwili kuchoka
8.Sauti kubadilika
9.Maambukizi ya kifua ya mara kwa mara

NJIA ZA KUJIKINGA NA KANSA YA MAPAFU.
1.Kuacha uvutaji wa sigara
2.Kuepuka mazingira ya wavutaji sigara
3.Kupata mlo kamili unaohusisha matunda na mboga za majani
4.Kufanya mazoezi ya mwili
5.Kujiepusha na hatari/mazingira ya hatari yaliyoorodheshwa hapo juu.

Authored by Dr.Bugota
Afya Yako ndio msingi wa maisha yako
#0759424664 #

BREAST CANCER (SARATANI YA MATITI)Saratani ya matiti ni saratani ambayo hutokea katika matiti ya mwanadamu,saratani hii ...
05/09/2021

BREAST CANCER (SARATANI YA MATITI)

Saratani ya matiti ni saratani ambayo hutokea katika matiti ya mwanadamu,saratani hii huwapata sana wanawake na wanaume kwa asilimia chache sana(1%) pia ni moja kati ya saratani ambazo huwapata sana wanawake.

WATU WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA SARATANI YA MATITI.
1.Wanawake
2.Wanawake wenye umri zaidi ya miaka 50 pia inaweza kutokea chini ya miaka 50
3.Wanawake wenye ndugu waliowahi kupata saratani ya matiti au historia ya kupata saratani ya matiti hapo nyuma.
4.Waliowahi kupatwa na mionzi k**a X-ray, ultraviolet rays
5.Wanawake wenye unene uliopitiliza
6.Wanawake waliochelewa kupata watoto(zaidi ya miaka 30) au kutokupata kabisa
7.Wanawake wasionyonyesha au kunyonyesha kwa muda mfupi sana
8.Wanawake wanaotumia uzazi wa mpango
9.Wanawake wanaokunywa pombe
10.Wanawake wanaovuta sigara
11.Wanawake weupe (wazungu) wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti kuliko wanawake weusi.

DALILI ZA SARATANI YA MATITI.
1.Kupata uvimbe kwenye matiti.
2.Matiti au chuchu kubadilika rangi.
3.Chuchu kurudi kwa ndani
4.Kutokwa na damu kwenye chuchu
5.Maumivu ya matiti au chuchu.

NJIA ZA KUJIKINGA NA SARATANI YA MATITI.
1.Kuacha kuvuta sigara kwa wanawake
2.Kuacha unywaji wa pombe
3 Kupunguza unene na kuwa na mwili wa kawaida
4.Kunyonyesha
5.Kufanya mazoezi ya mwili
6.Kujikinga na mionzi k**a X-rays,ultraviolet rays
7.Kujikinga na kujiepusha na hatari zilizoorodheshwa hapo juu.

Authored by Dr.Bugota
Afya yako ndio msingi wa maisha yako
#0759424664 #

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUMETatizo la Upungufu wa Nguvu za kiume limekuwa likiikumba jamii kubwa ya Tanzania,Africa na Dun...
15/05/2021

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la Upungufu wa Nguvu za kiume limekuwa likiikumba jamii kubwa ya Tanzania,Africa na Duniani kote,hapo awali lilikuwa likiwakumba wanaume kuanzia miaka 40 na kuendelea lakini sasa hata vijana(Chini ya miaka 40) ambao bado hawajaingia kwenye ndoa wanapatwa na tatizo hili.

Pia watu hukimbilia kutumia dawa za kuongeza Nguvu za kiume bila kujua visababishi au vyanzo vya matatizo yao ya Upungufu wa Nguvu za Kiume ili kujikinga au kutibu Tatizo hilo. Leo tuone visababishi vya UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME ili kujikinga na Tatizo hili.

VISABABISHI VYA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
1.Kujichua(Masturbation)-kitendo hiki huathiri mishipa ya damu ya uume na hata kupelekea ulegevu wa uume na kushindwa kufanya kazi k**a kawaida.
2.Kutokupata mlo kamili(Balanced Diet)
3.Uvutaji wa sigara
4.Unywaji wa pombe kwa muda mrefu
4.Matumizi ya madawa ya kulevya k**a bangi na co***ne
5.Kufanya kazi au mazoezi kupita kiasi na kukosa muda wa kupumzika
6.Matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi pamoja na vyakula vya kisasa k**a kuku wa kisasa na mayai yake
7.Ugonjwa wa Kisukari
8.Pressure ya kupanda na kushuka
9.Kutokufanya mazoezi ya mwili
10.Uzito mkubwa/Unene uliopitiliza
11.Maambukizi ya mfumo wa uzazi k**a Gonorrhoea
12.Kemikali za madawa ya kupulizia mboga za majani na mimea-kwa kutumia mboga ambazo zina mda mchache tangu zipuliziwe dawa
13.Mionzi k**a X-ray

Authored by Dr.Bugota
Afya yako ndio msingi wa maisha yako
0759424664.

KIDNEY STONESKidney stones ni mrundikano wa madini(hard mineral deposits) ndani ya figo ambayo hupelekea kupata maumivu ...
10/05/2021

KIDNEY STONES

Kidney stones ni mrundikano wa madini(hard mineral deposits) ndani ya figo ambayo hupelekea kupata maumivu ya tumbo la chini kwa pembeni.

NJIA ZA KUJIKINGA NA KIDNEY STONES

1.Kunywa maji ya kutosha-kwa siku kunywa maji kuanzia lita 2 hadi 3.
2.Kula chakula chenye madini mengi ya Calcium k**a maziwa.
3.Kutumia Chumvi kidogo katika chakula au ya kawaida pamoja na kuepuka matumizi ya chakula vyenye chumvi nyingi
4.Kupunguza matumizi ya nyama-nyama ya ng'ombe,kuku,nguruwe na samaki.
5.Kupunguza matumizi ya Vitamin C-matunda k**a Chungwa,nanasi pamoja na mboga za majani.

Authored by Dr.Bugota
Afya yako ndio msingi wa maisha yako
Mawasiliano #0759424664 #

HEART DISEASES(MAGONJWA YA MOYO)Kwa zaidi ya miaka kumi Shirika la Afya Duniani linaonesha kuwa Magonjwa ya moyo ndio ya...
23/04/2021

HEART DISEASES(MAGONJWA YA MOYO)

Kwa zaidi ya miaka kumi Shirika la Afya Duniani linaonesha kuwa Magonjwa ya moyo ndio yanaongoza kwa vifo vya watu wengi duniani.Magonjwa ya moyo huwapata wenye umri kuanzia miaka 45 na zaidi.

Kuna mazingira au tabia ambazo husababisha magonjwa haya kuwapata watu.

NJIA ZA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MOYO.
-Kuacha uvutaji wa sigara
-Kupunguza matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi
-Kufanya mazoezi ya mwili kila siku
-Kupata mlo kamili kwa kupendelea zaidi mboga za majani na matunda na kupunguza kutumia nyama
-Kuwa na mwili wa kawaida/kupunguza unene uliopitiliza
-Kuepuka kazi/kukaa kwa mda mrefu bila kusimama na kutembea mfano maofisini.

Authored by Dr.Bugota
Afya yako ndio msingi wa maisha yako
Mawasiliano #0759424664 #

HEPATITIS (HOMA YA INI)Homa ya ini ni jeraha au maambukizi ya ini katika mwili wa binadamu ambayo hutokea kwa sababu mba...
17/04/2021

HEPATITIS (HOMA YA INI)

Homa ya ini ni jeraha au maambukizi ya ini katika mwili wa binadamu ambayo hutokea kwa sababu mbalimbali.

NJIA ZINAZOWEZA KUSABABISHA HOMA YA INI.
-Virusi aina ya Hepatitis A,B,C,D na E
-Utumiaji wa pombe
-Matumizi ya madawa k**a Panadol,Aspirin kwa muda mrefu
-Upungufu wa usafirishwaji wa damu katika ini

NJIA ZINAZOSABABISHA MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI INAYOSABABISHWA NA VIRUSI(HEPATITIS B,C).
-Tendo la ndoa(Kujamiiana): Hii ni njia kuu ya maambukizi ya Virusi vya Hepatitis B na C
-Kuongezewa damu ambayo haijafanyiwa vipimo vya Virusi vya Hepatitis
-Kuguswa au kumwagikiwa na damu au kimiminika cha mwili k**a vile mate,jasho na maziwa
-Kushea vitu vyenye ncha kali k**a vile sindano,miswaki na viwembe
- Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto


DALILI ZA HOMA YA INI.
-Mwili kuchoka
-Kuumwa misuli na joint
-Kupoteza hamu ya kula
-Kichefuchefu na kutapika
-Kupata manjano katika macho na ngozi
-Kukojoa mkojo mweusi
-Mwili kuchemka
-Kupungua uzito wa mwili

MADHARA YANAYOSABABISHWA NA HOMA YA INI.
-Ini kushindwa kufanya kazi yake k**a kawaida ambayo hupelekea madhara k**a kukoseakana kwa uwezo wa kugandisha damu mwilini,tumbo kujaa......
-Kansa ya ini

NJIA ZA KUJIKINGA NA HOMA YA INI.
- Kupata chanjo ya Homa ya ini inayosababishwa na virusi
-Kuacha kunywa pombe
-Kuepuka kuongezewa damu ambayo haijafanyiwa vipimo vya Virusi vya Hepatitis
-Kuepuka kushea vitu vyenye ncha kali k**a sindamo na miswaki
-Kuepuka kugusa damu au kimiminika cha mwili k**a mate,jasho,na maziwa ya mama.

Authored by Dr.Bugota
Afya yako ndio msingi wa maisha yako
Mawasiliano #0759424664 #

SICKLE CELL ANAEMIA(SELI MUNDU).Seli mundu ni ugonjwa wa kurithi ambao unasababishwa na uzalishwaji wa hemoglobin zenye ...
09/04/2021

SICKLE CELL ANAEMIA(SELI MUNDU).

Seli mundu ni ugonjwa wa kurithi ambao unasababishwa na uzalishwaji wa hemoglobin zenye muundo usio wa kawaida ambao hupelekea kuvunjika kwa seli za damu.

Ugonjwa huu hutokea pale ambapo wazazi au mume na mke wanapokuwa na gene za sickle cell anaemia au mzazi mmoja ana gene na mwingine amebeba gene za sickle cell wanapopata mtoto atarithi ugonjwa wa sickle cell kutoka kwa wazazi.

Pia hutokea pale ambapo wazazi wote wamebeba gene za sickle cell ingawa hawaonyeshi kuwa na dalili za ugonjwa hivyo kati ya watoto wao atapata ugonjwa wa sickle cell.

MADHARA YA UGONJWA WA SICKLE CELL.
-Mtoto kupata maambukizi ya mara kwa mara k**a malaria
-Mtoto kuvimba ini pamoja na bandama
-Kupungukiwa damu mara kwa mara
-Kupanuka kwa mishipa ya damu kwa sababu ya kuzalisha damu kupita kiasi
-Kukojoa damu
-Mtoto kushindwa kukua kwa wakati au kudumaa
-Kupata shida ya kuona
-Maambukizi ya kifua(pneumonia)
-Kupata vidonda vya mda mrefu
-Kufeli kwa mifupa(bone marrow) kuzalisha damu.

Jamii kubwa ya Kanda ya ziwa ina wagonjwa wengi wa Sickle Cell Anaemia kwa sababu ya kuoana wao kwa wao na hivyo kupelekea kuongezeka kwa wagonjwa.

Chukua hatua kuzuia ugonjwa/magonjwa yanayoepukika.

NOTE:Wewe kaka au dada zuia mtoto wako kupata Seli Mundu kwa kupima damu pamoja na mwenzi wako au mchumba wako kabla ya kuona ili kumlinda na kumkinga mtoto wako asipate Seli Mundu hata k**a mzazi umebeba gene za Seli Mundu.

Authored by Dr.Bugota
Afya Kwanza,Afya Muhimu,Afya ndio Maisha
Mawasiliano #0759424664 #
Afya Yako ndio msingi wa maisha yako.

TRICHOMONIASIS(KUTOKWA NA UCHAFU WA KIJANI SEHEMU ZA SIRI).Habari za leo wapendwa,leo tujifunze kuhusu Trichomoniasis.Tr...
15/03/2021

TRICHOMONIASIS(KUTOKWA NA UCHAFU WA KIJANI SEHEMU ZA SIRI).

Habari za leo wapendwa,leo tujifunze kuhusu Trichomoniasis.

Trichomoniasis ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume,maambukizi haya husababishwa na vimelea aina ya protozoa vinavyojulikana k**a Trichomonas vaginalis.

Maambukizi haya huwapata jinsia zote yaani wanaume na wanawake lakini hutokea sana kwa wanawake.

NJIA ZINAZOSABABISHA MAAMBUKIZI YA TRICHOMONIASIS.
1.Kujamiiana
2.Kushea mavazi k**a taulo na nguo za siri
3.Kupitisha vitu k**a midoli,vidole,tango sehemu za siri(mwanamke) ambavyo sio sahihi na salama.

DALILI ZA TRICHOMONIASIS.
-Kuwashwa sehemu za siri kwa mwanamke
-Kuumwa tumbo la chini kwa mwanamke
-Kupata vidonda sehemu za siri
-Maumivu wakati wa kukojoa
-Kutokwa na uchafu mwingi wa kijani au njano sehemu za siri kwa mwanamke.

NJIA ZA KUJIKINGA NA TRICHOMONIASIS.
1.Kutokushiriki tendo la ndoa
2.Kutumia kinga wakati wa tendo la ndoa
3.Kujihusisha na mahusiano katika umri sahihi na wakati sahihi.
4.Uaminifu kati ya wanandoa au wenzi.

Authored by Dr.Bugota
Afya yako ndio msingi wa maisha yako
Mawasiliano #0759424664 #

TUBERCULOSIS(KIFUA KIKUU)Habari za leo wapendwa,leo tujifunze kuhusu Kifua KikuuTB ni maambukizi katika mapafu ya mwanad...
07/03/2021

TUBERCULOSIS(KIFUA KIKUU)

Habari za leo wapendwa,leo tujifunze kuhusu Kifua Kikuu

TB ni maambukizi katika mapafu ya mwanadamu na nje ya mapafu k**a vile mifupa na uti wa mgongo.

TB inasababishwa na bacteria wanaoitwa Mycobacterium tuberculae

TB humpata mtu mwenye upungufu wa kinga ya mwili mfano mwenye maambukizi ya VVU,Kisukari na pia pia inaweza kumpata mtu yeyote ambaye kinga yake ya mwili sio imara

Bacteria wanaosababisha TB wanaweza kumpata mtu na wasionyeshe dalili yoyote ile mpaka pale kinga yake ya mwili itakaposhuka(pungua) hivyo ni muhimu kujikinga na TB

NJIA YA MAAMBUKIZI YA TB.
-TB inaambukizwa kwa njia ya kupatwa na maji au matone yenye bacteria wa TB kupitia kukohoa,makohozi.

DALILI ZA TB.
- Kukohoa kikohozi kibichi zaidi ya wiki 2
-Kukohoa damu
-Kutokwa na jasho wakati wa usiku
-Mwili kuchemka sana
-Mwili kupungua sana ndani ya mda mfupi
-Kupata shida ya kupumua

NJIA ZA KUJIKINGA NA TB.
1.Kuepuka mikusanyika k**a Disco,Club,Madarasa yasiyo na madirisha ya kutosha na mikusanyiko mingine
2.Kutunza na kujali afya ya mwili kwa kujikinga na maambukizi ya VVU,Kisukari
3.Kukaa mbali na mtu anaekohoa bila kujifunika mdomo na kuepuka kugusa makohozi ya mtu ni hatari kiafya.
4.Kutumia dawa za kujikinga na TB
5.Kutumia dozi ya maambukizi ya VVU ipasavyo na kutumia IPT.

Address

Maswa

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jari Afya yako na Dr.Bugota posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Jari Afya yako na Dr.Bugota:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram