15/02/2021
_Tunaendelea....._
Pharm_golden.💉 *SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (Cervical Cancer)*
SEHEMU YA 2.🍀
Na PHARM HASHIM..🌴
📌.BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
1.Kutokwa na maji maji au uchafu wenye harufu kali ukeni
2.Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa
3.Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area)
4.Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiana
5.Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia pia mkojo wenye matone ya damu.
📌.JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA?
📤.Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema.
📚.PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST); Pap- smear ni test ambayo hutumika kuchunguza mabadiliko ya chembe zilizo katika mlango wa kizazi ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo na hivyo kuwahi kuyakabili mapema.
📌.UMRI WA KUFANYA PAP TEST
📚.Test hii hushauliwa kwa wanawake wa umri wa miaka 21 hadi 65 na chini ya um ri wa miaka 21 endapo umeingia katika tendo la ndoa au kujamiana kwa kipindi kisichopungua miaka 3.
📌.KUPUNGUZA HATARI YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
🌹.Pap test
📚.Waweza kupata Pap test mara moja kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2-3, hii inategemea ushauri wa daktari, umri, hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika test zilizotangulia na mfumo wako wa maisha
🌹.Pata HPV Vaccine (hii yashauliwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari)
🌹.Kuwa na mpenzi mmoja. Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
🌹.Tumia kinga (Condoms). Hii husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
MWISHO NA AHSANTENI….🙏🙏