13/12/2023
ZIJUE CHANGAMOTO ZA VIUNGO NA MIFUPA NA ATHARI ZAKE:
Changamoto ya VIUNGO na MIFUPA ni changamoto ambayo hivi karibuni imekuwa ikiwakabili watu wengi (wa Kila rika)
Changamoto hii husababishwa na sababu mbalimbali k**a vile;
Kulika kwa gegedu(cartilage), kuisha kwa uteute(synovial fluid), upungufu wa madini ya Calcium n.k
Changamoto ya VIUNGO na MIFUPA inaweza kugawanywa katika makundi manne kulingana na sababu kuu iliyopelekea tatizo husika.
1. OSTEOARTHRITIS
Hili ni tatizo linaloathiri VIUNGO linalosababishwa na UMRI wa mtu husika.....
Inakadiriwa kuwa watu wenye UMRI kati ya miaka 30-45 na kuendelea wapo kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili kwani wanakuwa na upungufu wa virutubisho muhimu ambavyo ni mahsusi kwa ajili ya mifupa......
Tatizo hili linaathiri VIUNGO na baadae huathiri MIFUPA.....
Tatizo hili hutokea baada ya gegedu(cartilage) kulika kwenye VIUNGO na uteute(synovial fluid) kuisha.
OSTEOARTHRITIS huathiri VIUNGO mbalimbali vya mwili k**a vile nyonga, magoti, pingili za uti wa mgongo n.k.
SABABU ZINAZO ONGEZA UWEZEKANO WA KUTOKEA KWA OSTEOARTHRITIS
> Uzito uliopindukia
> Historia ya familia
> Ajali
> Kutumikisha viungo kupita kiasi mfano wanamichezo, wanamazoezi nk.
> Kufanya kazi ngumu hasa za kusimama kwa muda mrefu.
2. RHEUMATIC ARTHRITIS
Tatizo hili hutokea pale ambapo Kinga ya mwili hugeuka na kutafuna gegedu(cartilage) na kwasababu hiyo tatizo hili hufahamika kwa lugha ya kitaalamu k**a AUTOIMMUNE.......
Tatizo hili linaweza kuwapata watu wa rika zote (watoto, vijana na watu wazima)
NB:
Sababu ya tatizo hili SIYO upungufu wa virutubisho, bali ni Kinga ya mwili kushambulia gegedu (cartilage) hivyo mtu anayesumbuliwa na tatizo hili HATAKIWI kutumia dawa za kuongeza virutubisho
3. OSTEOPOROSIS
Hili ni tatizo linalosababishwa na upungufu wa madini ya Calcium yanayosaidia mifupa kuwa imara.....
Hivyo upungufu wa madini haya(Calcium) hupelekea viungo k**a vile mifupa ya mguu na uti wa mgongo kuvunjika kwa urahisi.
4. GAUT ARTHRITIS
Hili ni tatizo linalosababishwa na Uric acid (kemikali inayotokana na protini ya nyama)
DALILI ZA VIUNGO KUSAGANA:
1. MAGOTI
> Maumivu kwenye magoti
> Magoti kushindwa kujikunja kutokana na maumivu
> Kushindwa kupanda ngazi kwa urahisi
> Kusikia milio ya mifupa kusagana kwenye magoti
2. MGONGO/ UTI WA MGONGO
> Maumivu kwenye mgongo
> Kushindwa kuinama
> Kusikia maumivu makali wakati wa kuinama
> Ganzi kwenye mapaja au miguu.
3. BEGA
> Kushindwa kunyanyua mkono na kusikia maumivu makali kwenye BEGA
MUHIMU:
Katika harakati za kutatua changamoto hii, watu wengi wemekuwa wakitumia dawa za kutuliza maumivu ambazo huwapa nafuu ya muda na baadae maumivu kurejea tena.......
Kwasababu dawa hizi hazina uwezo wa kuzalisha gegedu (cartilage) na uteute (synovial fluid) ambazo ndiyo sababu kubwa ya tatizo.
Pia, baadhi Yao hushauriwa kufanya mazoezi ambayo huwasaidia kwa muda na baadae tatizo kujirudia tena.
Je, wewe ni mmoja wa watu wenye changamoto mojawapo kati ya hizo👆👆👆 na unahitaji msaada?
Tutafute kupitia:
Whatsapp/ Normal Call(simu)/ Message
Kwa Number: +255 612 113 809 kwa msaada zaidi