30/06/2023
Kuna mambo ambayo Madaktari wengi watakuambia ili hili ninalo kuambia hapa hutalisikia. Imekua ikijulikana kwa miaka mingi kuwa kitu fulani ni kibaya au kitu fulani sio salama kwa mtu fulani. Hebu ambatana nami nikufahamishe
1. Wagonjwa wenye magonjwa ya moyo wengi wamekua wakishauriwa au kuzuiwa kutumia chumvi ya mezani sababu ikiwa ni kwamba inasababisha shinikizo la damu kuwa juu (High Blood pressure, Hypertension). Je, ni kweli chumvi ni mbaya kiasi hicho au nini hasa kina sababisha?? Nikurahisishie tu, Chumvi ya mezani yaani chumvi unayoongeza wakati mnakula haina tofauti yoyote na Chumvi iliyochemshwa au kupikwa. Hakuna elimu ya kikemia inayoonyesha dhahiri utofauti huo ni msingi kiasi cha kuzingatia?. Ngoja nikuambie, Chanzo kikubwa cha magonjwa mengi haya ya moyo na mengine ambayo sio ya kuambukiza husababishwa na kitu kiitwacho SUKARI. Sukari ubayotumia kwenye chakula, sukari unaikuta kwenye vinywaji baridi na hata kwenye biskuti. Sukari ndio chanzo cha matatizo, k**a utaweza kuiondoa sukari maishani mwako basi utakua umeshinda na inawezekana magonjwa ya kuambukiza yakapotea kabisa maishani mwako.
2. Watu wamekua wakiambiwa wasile nyama nyekundu hasa hasa wagonjwa wenye ugonjwa gauti au ugonjwa magoti. Hii imekua hivyo kwa kile ambacho tafiti huko mwanzo ilionekana hivyo. Lakini tafiti zinaonyesha kuwa, Sukari hii inayoitwa FRUCTOSE ndio shida na ndio chanzo kikubwa cha ugonjwa wa magoti (Gauti). Ni ukweli usiopingika, Madaktari wengi wamekua wakiwashauri wateja ama wagonjwa wao kuhusu kuacha kutumia nyama nyekundu eti tu kwa sababu wanaogopa kupata gauti. Hii si kweli, nyama nyekundu ina mchango kidogo sana kupelekea kupata ugonjwa huu bali sukari hii iitwayo Fructose. Sukari hii utaipata kwa wingi kwenye vyakula k**a; Asali(kwa kiasi kikubwa), Ndizi, na vinywaji vya viwandani ambavyo hutengenezwa kwa kuongeza Fructose kukifanya kinywaji kuwa kitamu zaidi. Hivyo nikuombe tu ufahamu kuwa nyama ni moja ya chakula muhimu sana kwani kuna baadhi ya virutubisho hatuwezi kuvipata kwenye chakula kingine isiopokuwa nyama nyekundu. Ujumbe wabgu ni kwamba, usiache kula nyama nyekundu ukiogopa kupata gauti, punguza kula Vyakula vilivyo na sukari hiyo iitwayo Fructose. Zingatia namna nzuri za kuzingatia wakati wa kupika au kuandaa nyama kwa ajili ya chakula.
K**a umependa makala hii fupi acha ujumbe kwenye comment na mimi nitajibu na uulize swali ambalo ungependa niliweka hapa. Shirikisha marafiki zaidi na zaidi.