02/06/2026
Tafakuri ya Leo.
Licha ya serikali na sera ya elimu nchini kusisitiza umuhimu wa mtoto kupitia Darasa la Awali kabla ya kuingia Darasa la Kwanza, pamoja na jitihada za kuboresha miundombinu ya elimu hii, bado kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa walimu wenye taaluma maalumu ya Elimu ya Awali katika shule nyingi za msingi.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya shule hulazimika kutumia walimu wa kujitolea au walimu wasiobobea katika elimu hii kufundisha watoto wa Darasa la Awali.
Je, hali hii haiathiri haki ya msingi ya mtoto kupata elimu bora na stahiki kwake?
Kwa kuwa mtoto wa elimu ya awali anahitaji mwalimu mwenye uelewa wa saikolojia ya mtoto, ukuaji wake, pamoja na mbinu mahsusi za ufundishaji zinazolingana na umri wake, je ni sahihi kumuweka chini ya mwalimu ambaye hajapatiwa mafunzo maalumu ya Elimu ya Awali?
Ni wakati gani mfumo wa elimu utaweka uwiano sawa kati ya ongezeko la wanafunzi wa Darasa la Awali na ajira rasmi za walimu wa taaluma hii?