31/12/2023
USISITE KUTUPIGIA KWA MAHITAJI YA VIFARANGAππππ 0767 860 266
UTUNZAJI WA VIFARANGA.
Swali:Unaposema utunzaji wa vifaranga unamaanisha nini.*
Jibu:Ni hatua inayofuata baada ya yai kutotolewa , na Uleaji wa vifaranga ni jumla ya mambo yote yanayofanyika kwaajili ya kuhakikisha kifaranga anakua vema hasa ndani ya umri wa mwezi mmoja wa kwanza. Kipindi hiki ni muhimu kwakua mfugaji anapaswa kuweka mazingira sahihi mathalani kukuza vema kifaranga na kupunguza idadi ya vifo.
Hapa ndipo mwanzo wa kuku mkubwa kuanza kutengenezwa
*Swali:* *Mfugaji anapaswa kuzingatia mambo gani baada ya kifaranga kutotolewa* .
π *JIBU* : Kabla ya kuangalia mambo gani ya kufanya baada ya kifaranga muanguliwa, ni vema mfugaji akafahamu mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuingiza vifaranga hao bandani.
Mambo yafuatayo yazingatiwe kabla ya kuingiza vifaranga bandani
1: Andaa sehemu maalumu ya kulelea vifaranga Kinengunengu ( Brooder ) inaweza kuwa ya duara au ya pembe ila iwe na uwezo wa kutunza joto kwa muda wote itakavo hitajika.
Hii iwe ndani ya chumba ambacho kinaruhusu hewa kuingia
Kiruhusu mwanga kuingia ili vifaranga waone chakula na maji
Chumba kiwe na chanzo cha joto, unaweza kutumia Vyungu vya joto, Gas brooder, Electric heater, Bulb za umeme, Infrared bulb N.K, ni muhimu sana kuzingatia joto kwakua bila kufanya hivo utapoteza vifaranga wengi katika kipindi hiki.
Ikumbukwe kifaranga akiwa na umri chini ya wiki 2 mwiliwake unakua hauna uwezo wa kuzalisha joto la kutosha hivo anahitaji joto la ziada kumfanya astawi vema.
*Swali* :Wafugaji wengi hawana vifaa vya kupimia joto, je mfugaji atajuaje k**a joto bandani linayosha au halitoshi.*
*Jibu* : Nikweli nimuhimu mfugaji akatambua viashiria vya hali ya hewa bandani hatak**a hatakua na vifaa vya kupimia joto
*Vifaranga utawatambua kwa mwenendo wao bandani.*
π *Kipindi cha baridi* , au k**a bandani kuna baridi, Vifaranga wataonesha dalili zifuatazo
πWatakusanyika sehemu moja, au katika makundi makundi na watakua wakitetemeka
πWatakusanyika karibu na chanzo cha joto (chungu, jiko, bulb)
πVifo hutokea katika hayo makundi kwa kulaliana na kukosa hewa( suffocation ).
*Suluhu* : Pindi joto linapopungua ongeza chanzo cha joto, mfn k**a ulikua unatumia chungu kimoja unaongeza, au unazuia mianya ya kuingilia upepo wenye baridi. Au kuongeza bulb za joto n.k
π *K**a joto litazidi sana.*
Hapa vifaranga huonesha dalili ya kufumbua midomo na kuhema muda wote mdomo ukiwa wazi,
Pia vifaranga hukaa mbali na chanzo cha joto ( bulb , vyungu, gas brooder au heater) na husogea pembezoni kabisa mwa brooder mahali ambapo joto halitafika sana
Hapa vifaranga hawatakua wanakula na kunywa maji ipasavyo na ukuaji wao huwa si mzuri
Vifaranga huonesha kuganda kinyesi nyuma ( cheusi na vifo huongezeka kwa kupungukiwa maji ) dehydration.
*Suluhu* : Punguza chanzo cha joto mpaka utakapoona hali ya hewa bandani ni sahihi kwa vifaranga wako ( wasambae vema bandani).
K**a unatumia bulb unazinyanyua juu kidogo zisisogee zana karibu na migongo ya vifaranga
K**a unatumia Gas brooder unapunguza level ya kufungulia gas, fungulia wastani.
π *Joto sahihi* Vifaranga watasambaa vema bandani, wataendelea na mizunguko ya kawaida, watakua bize kula na kunywa maji na ukuaji wao huwa mzuri na wauwiano mzuri kabisa.
π *Upepo ukiingia sana bandani*
Vifaranga hukimbia kwa mizunguko ya makundi makundi na hurundikana mahali upepo unapoingilia, *mfn* upepo ukiingilia Magharibi kuelekea mashariki , vifaranga watakusanyika dirisha la magharibi kukwepa upepo usiwafikie mashariki.
*Suluhu* : Weka matrubai kuzuia upepo unaoingia moja kwa moja pindi upepo unapozidi ila usizibe sana acha sehemu ya hewa kuingilia.
*Swali:* *Nitagunduaje k**a kifaranga anaumwa.?*
*Jibu:*
Inawezekana kutambua k**a kifaranga anaumwa mathalani kwa kuangalia vitu vichache
πUchangamfu, ulaji, kuzubaa, ila hii haikupi kujua huyu kifaranga anaumwa nini hakika
πKitu ambacho unapaswa kukizingatia ni kuangalia dalili, ili kutambua ugonjwa husika ( kinyesi, idadi ya Vifo, kukoroma, chafya) Usianzishe dozi ya dawa kwa kifaranga pasipo kujua dalili sahihi ya ugonjwaπͺ
*Magonjwa sumbufu kwa vifaranga*
π *Coccidiosis* , Vifaranga huzubaa, hushusha mabawa, hutoa vinyesi vya ugoro na hatimae kinyesi chekundu ( Tiba itategemea level ya ugonjwa ila Dawa zinazotumika Hasa , ni Amplorium, Vetacoxys , Agracox, (Anticox kwa anaehara damu) MUONE DAKTARI
π *Pullurm* Ugonjwa wa vifaranga kuganda kinyesi nyuma, hasa ranging ya njano, hii ni aina mojawapo ya typhoid na hurithiwa kutoka kwa wazazi kupitia yai
Suluhu pata vifaranga kutoka shamba salama lisilo na typhoid
Pindi wanapo umwa, tumia dawa k**a Trisul, Trimafarm au Biosol ( *fika clinic au muone daktari kwa msaada* )
π *Brooder Pneumonia,* kifaranga anakua anapumua ila hatoi sauti, hii imeripotiwa kuua vifaranga wengi sana kwenye mashamba mengi, Suluhu vifaranga wachanjwe chanjo za maambukizi ya mfumo wa hewa k**a IB, pia zingatia Joto kwenye Brooder. *(Case hii ni ngumu kwa wengi fika Clinic ya mifugo kwa msaada zaidi
*Swali:* *Kifaranga kwanini anachanjwa, na anatakiwa kuchanjwa kila baada ya muda gani?*
*Jibu:* Kutokana na aina ya kuku ratiba za chanjo zinatofautiana k**a ifuatavyo
π *Broilers/ kuku wa nyama*
Siku ya 7 Newcastle/ kideri
Siku ya 14 Gumboro
Siku ya 21 Newcastle /kideri
Au
Siku ya 7 kideri/ Newcastle
Siku ya 14 Gumboro
Siku ya 21 Gumboro
πKwa kuku wanaotaga (Chotara, Layers , kienyeji)
Siku ya 1 Marek's
Siku ya 7 Newcastle/ kideri
Siku ya 14 Gumboro
Siku ya 21 Newcastle /kideri
Siku ya 28 Gumboro
Siku ya 30 Ndui
Kila baada ya miezi mitatu Newcastle/kideri
*Swali* πKwanini kuku anachanjwa?
*Jibu:* Kuku anachanjwa ili apewe kinga dhidi ya ugonjwa husika kabla haujaingia, na hata k**a utaingia tayari mwili utakua umetengeneza kinga/immunity ya kutosha dhidi ya ugonjwa husika.
*Swali:* Ni kwanamna gani mfugaji anapaswa kuchanja vifaranga wake ipasavyo?
*Jibu:* Kwanza kabisa zipo njia nyingi za kuchanja kuku kutokana na aina ya chanjo , na namna za kuchanja hutofautiana kwa kuzingatia maelekezo ya chanjo
*Maelezo ya namna ya uchanjaji*
Mfn: Newcastle na Gumboro, ni chanjo ambazo huchanganywa kwenye maji na kuku akanywa
Ila *NEWCASTLE* ipo chanjo ya matone ambayo inawekwa tone moja kwa jicho moja pekee( usiweke macho yote)
Jitahidi kuchanganya kutokana na idadi ya kuku na nunua dozi stahiki.
*UCHANGANYAJI*
πDOZI 500 lita zisizidi 20 Lita
πDozi 10000 maji yasizidi Lita 40
πKwa sasa zipo dozi ndogo pia za kuku 200-300
πChanjo za sindano k**a NDUI huchomwa eneo la bawa( wing web)
πZipo chanjo za Kifua na za shingo. ( *Waone madaktari)*
*Mwisho kabisa*
Sio sheria kifaranga kupewa madawa wakati hawaumwi πͺπͺ
Vifaranga wapewe chakula sahihi
πSTARTER KWA UMRI WA wiki 7-8 KWA WANAO ANDALIWA KUTAGA
Kwa vifaranga Bora tucheck sasa JC VIFARANGA PROJECT 0767 860 266
IMEL jc.digital@ymail.com