11/10/2020
KISASI CHA WACHAWI
SEHEMU YA ( 8 )
ILIPOISHIA,,,,
Nusu kati yao walikuwa ni warefu sana, wanakaribia kimo cha mnazi. Wengine waliobakia walikuwa ni wafupi mfano wa mbilikimo waishio katika msitu wa nchi ya Kongo, ilikuwa pengine yapata saa nane hivi usiku.
INAENDELEA,,,
Kwa makisio ya haraka haraka watu hao wa ajabu walikuwa wanaelekea hapo kwenye mwembe ambako ndiko nilikojibanza ili kuwapisha wapite. "Mama yangu weee,, hee,! Wanakuja huku, hivi wakiniona hapa usiku huu si itakuwa balaa kubwa sana kwangu ?
Nikajiambia moyoni,,,.
Watu hao walikuwa wakiimba wimbo ambao hata mie niliusikia mtamu huku wakicheza na kuruka ruka, k**a vile ngoma ya kabila la kimasai. Wahenga walisema "tembea uone". Lakini mie sikutembea kwa hiari yangu, pamoja na kwamba ni kweli nimeyaona.
Nikasikiliza kwa makini wimbo waliokuwa wanaimba huku baadhi yao wakiitikia. "Tuwapeleke, tuwapeleke hao kwenye makao yetu. Chaaa chaaa chaaaa!! "Tuwapeleke, tuwapeleke hao kwenye makao yetu. Chaaa chaaa chaaa!!. Wengine walikuwa wanaimba. Tuwapeleke, tuwapeleke hao, baadhi yao walikuwa wakiitikia chaaa, chaaa, chaaaa!!!
Sasa pamoja na woga niliokuwa nao nikautafakari na kuuchambua huu wimbo ulioonekana dhahiri kuwakolea mno k**a vile wale waupendao muziki wa taarabu ama reggae au bongo fleva. Kwanza nikalitafakari hili neno "tuwapeleke", nikajiuliza ni akina nani kati yao wanapelekwa ?
Kisha nikalichambua neno "kwenye makao yetu". Nikajiuliza, jee, wanawapeleka wapi huko ambako ndiko kwenye maskani yao ? Pamoja na kuwaza nikashindwa kupata jibu. Watu hao walipoukaribia huu mti wa mwembe nami ndivyo nikazidi kuoatwa na mfadhaiko. Kuna wakati niliamua nitoke mbio, lakini nafsi ikanizuia.
Kwanza nikajiuliza nikimbie, nikimbilie wapi na wakati watu hao tayari wameshafika hapo nilipokuepo. Jambo lililonitia tashtit i zaidi kufanya nishindwe kuondoka hapo mtini haswa nikikumbuka maneno aliyoniambia bibi kizee kuwa watu wabaya hawatoweza kunidhuru kamwe, nikajipa ujasiri japo sio sana.
Nikahisi kuwa hao ndio watu wazuri, watu hao machoni mwangu niliwaona ni wa ajabu sana, walipofika kwenye huu mti wa mwembe ambao ndipo nilipokuwepo nikajibanza. Waliuzunguka mti huo ili hali wakiendelea kuimba, niliona ajabu mie nilipokuepo hapo, lakini sikuona wakunishtukia bali waliendelea na ngoma yao wakiicheza na kuuzunguka mti huo.
"Au yule bibi aliniambia kweli kwamba watu wabaya hawataniona ?" Kidogo nilianza kupatwa na imani. Ghafla k**a dakika tato hivi, nikaona wameisimamisha ngoma yao, na watu wanne kati yao wakaitana chemba.
Niliwasikia wakizungumza kwa sauti ya chini, "hapa leo hapafai kabisa tuondokeni", walinong'onezana. Nikahisi kuwa hao huenda ndio wakubwa wa kundi hilo. Mmoja kati yao nilimsikia akiuliza, jee, kwa nini anasema hapa hapafai ?
"Ndio nasikia harufu mbaya kwa vyovyote kuna kitu sio kizuri hapa chini ya mwembe au juu" akajibiwa. Nikashusha presha, nikagundua kuwa kwa vyovyote dawa ya kunywa na kupaka aliyonipa bibi imefanya kazi yake kiusahihi. Kwa sababu wao niliwaona laivu mambo yote waliyokuwa wakifanya , lakini inaonyesha kwamba wao hawakuniona kabisa.
Ila huenda walihisi kwamba mahala hapi siku hiyo palikuwa "pazito" sikuelewa ni kwa nini, lakini nikaona kwamba hiyo ndiyo heri yangu. Baada ya dakika chache tuu walipatana waote waondoke mahala hapo na kuendelea na safari yao.
Safari hii waliondoka kimya kimya bila wimbo waliokuwa wakiuimba walipokuwa wanakuja. Nikawashuhudia wakitokomea zao, hatimae wakatoweka machoni mwangu.
ITAENDELEA,,,
BY RANIM,,