22/06/2022
JUMBE BORA KATIKA JUMBE NILIZOWAHI POKEA TOKA NAJITAMBUA KWA FAHAMU ZANGU
Namshukuru Allah (SUBHAANAHU WA TA'ALA) kwa hali zote alizonijaalia.
Huwa Nakumbuka sana hali yangu niliyokuwanayo miaka 15 iliyopita kabla ya kupata ajali.
Allah alinipa Afya Nzuri Sana, Nilikuwa ninanguvu ya kufanya vitu mbalimbali, k**a vile Pumzi ya kuogelea na kufanya mazoezi makali na uwezo wa kutembea masafa marefu.
Lakini Huwezi kuamini, Yote hayo sasahivi naona k**a Hadithi au ndoto, Nahisi k**a sio mimi ambae nilikuwa naweza kufanya vitu vyote hivyo.
Nilijiona k**a nipo katika dunia nyengine nilivyoparalyze mwili mzima, siwezi hata kunyanyua kidole changu mwenyewe.😢😢😢
Lakini Alhamdulillah Namshukuru sana Allah (SUBHAANAHU WA TA'ALA) kwa Mtihani Huu alionipa, Na Kiukweli Naweza kuuita Huu MTIHANI ni zawadi kutoka KWAKE. 🤲🤲🤲
ALLAHUAKBAR. ☝💪
Kupitia Mtihani huu Najifunza vitu vingi na Allah hunifutia Madhambi kila siku kwaajili tu ya kuamini kuwa yeye ndie aliyenipa na yeye ndie atakaeniondolea
Na Namwabudu yeye Mmoja tu pekee Apasae Kuabudiwa kwa Haki na Simshirikishi na kitu chochote. ☝
ALHAMDULILLAH.
Kumbuka kuwa MwanaAdamu Halikufiki jambo lolote mpaka Mwenyezi Mungu atake Likufike na Halikuepuki jambo mpaka Mwenyezi Mungu atake Likuepuke.
Maradhi haya yamenifanya nimjue vizuri Mwenyezi Mungu na Utukufu wake.
ALHAMDULILLAH. 🤲
Nimegundua Mwenyezi Mungu Ananipenda na ndio maana amenipa ZAWADI hii ya maradhi haya niliyonayo ili mpaka siku ya kukutananae niwe sina DHAMBI hata moja. Ananisafisha.
SUBHANALLLAHU. (AMETAKASIKA MWENYEZI MUNGU)
Unaweza ukachukia kitu kumbe kina kheri kubwa na wewe na unaweza kupenda kitu kumbe kina shari na wewe. Mwenyezi Mungu anajua zaidi na sisi hatujui.
Naamini Mwenyezi Mungu ameniepusha na mitihani mikubwa zaidi kuliko huu wa Maradhi niliyonayo.
ALHAMDULILLAH. 🤲🤲🤲
Hii dunia tunapita tu usihadaike kwa afya nzuri, kwa mali na watoto, kwani kitu kilichokuwa bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni uchamungu tu.
SHUKURU KWA HALI ZOTE.