17/05/2022
KWA UPANDE WA WANAUME: JE, KITAMBI KINAWEZA KUATHIRI NGUVU ZA KIUME?
Tunapojadiri unene, ni kawaida kabisa kuzingatia ugonjwa unaojulikana mara nyingi huletwa na uzito wa ziada. Kwa kawaida tunasikia juu ya wagonjwa walioathiriwa na uzito mbaya kutokana na ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo, kukosa usingizi au mafuta mengi kwenye damu.
NUKUU: Athari nyingine za uzito ambazo hujadiriwa mara chache sana huwa ni kushindwa kufanya mapenzi, na hili lipo pande zote mbili kwa wanaume na wanawake pia, hali ambayo inaweza kutokana na mkazo wa kihisia na usumbufu wa homoni.
Je, Mambo Ya Hatari Yanakuwaje?
Wanaume wengi wanaosumbuka na tatizo la unene au kitambi pia wanakuwa na tatizo la kushindwa kushiriki tendo la ndoa. Asilimia 43% ya wanaume kati ya umri wa miaka 40 hadi 70 wana matatizo ya kushindwa kushiriki tendo la ndoa. Kuna mambo mengi ya hatari kwa wanaoshindwa kushiriki tendo la ndoa ikiwa pamoja na;
• Umri
• Ugonjwa wa moyo
• Shinikizo la juu la damu
• Homoni za testosterone kushuka
• Uvutaji sigara na kisukari pamoja na lishe duni
Na tafiti nyingi zinazokinzana, haijulikani ikiwa uzito mkubwa wa mwili au unene wa kupindukia husababisha kupungukiwa nguvu za kiume au unaweza kusababisha vihatarishi vikubwa, hata hivyo, ni wazi kwamba unene unachangia kiwango kikubwa sana mwanaume kupungukiwa nguvu za kiume. Na mabadiriko makubwa ya afya yanapofanyika pamoja na mitindo ya maisha, basi hali ya upungufu wa nguvu za kiume, inaweza kutoweka.
NUKUU: Kwa kuongezeka kwa umri pekee, kuna kupungua nguvu za kiume. Ikiwa k**a kuna magonjwa mengine, basi fahamu kwamba ni hatari kubwa. Upungufu wa nguvu za kiume ndio chanzo kikubwa cha kuwa na wasiwasi na hofu kwa wanaume wote. Utendaji usioeleweka husababisha utendaji mbaya na mafadhaiko hata kwa wanaume wanaojiamini zaidi! Uzito unaweza kuleta magonjwa haya na pia kuukuza wasiwasi huu wa kisaikolojia.
Je, Jinsi Gani Kazi Ya Usimamishaji Wa Uume Hufanya Kazi?
Hebu tuangalie kwanza jinsi gani kazi ya udindishaji inavyofanya kazi. Hali ya uume kusimama hutokea pale mishipa ya damu inayoelekea kwenye uume inapopanuka, na kusababisha ijae damu. Mchakato huu hutegemea na njia ya mishipa ya damu ikitoa seli za nitriki oksidi. Nitriki oksidi husababisha misuli laini kulegea na uume kukak**aa na kusimama.
NUKUU: Kitu chochote kinachoharibu mishipa ya damu kinaweza kuingiliana na mchakato unaosababisha nguvu za kiume kupungua. Kwahiyo, vitu vinavyo sababisha ugonjwa wa moyo na kiharusi kinaweza kusababisha nguvu za kiume kupungua.
Unene Pamoja Na Upungufu Wa Nguvu Za Kiume
Kitambi au unene unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa kuharibu mishipa ya damu, kupunguza homoni ya testosterone na kupelekea hali ya kuvimba kwa mwili kwa ujumla. Unene au kitambi vinaweza kusababisha kuharibika kwa mishipa ya damu kutokana na ugonjwa wa moyo, kisukari cha kupanda, mafuta kwenye mishipa ya damu pamoja na kuvimba kwa mwili.
Inapendekezwa kuwa hali ya kuongezeka kwa kuvimba kunaweza kusababisha mabadiriko makubwa mwilini yanayoweza kusababisha maharibufu kwenye tishu za mwili wako. Madhara makubwa ya ugonjwa wa moyo, kisukari, nk, hutolewa mafunzo yake na hivyo hupokelewa na watu wanaopenda kujifunza zaidi. Wanaume wanaokuwa wameathiriwa na unene wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu au mafuta kwenye damu, na shinikizo la juu la damu pamoja na kisukari, na yote haya huchangia mwanaume kupungukiwa nguvu za kiume.
NUKUU: K**a umeathiriwa na unene, basi hatari ya kuwa na ugonjwa wa kisukari iko zaidi ya mara mbili au mara tatu kuliko mtu yule ambaye hajawahi kuathiriwa na tatizo la unene. Zaidi ya asilimia 50% ya wanaume wenye ugonjwa wa kisukari ndio huteseka sana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Imefanyiwa utafiti vyema na kukubarika kwamba, unene mara nyingi hupelekea mtu kupata ugonjwa wa kisukari pamoja na magonjwa ya moyo ambayo yanaweza kusababisha upunguvu wa nguvu za kiume. Hatujui sana kwanini, lakini unene unaonekana kuharibu sehemu ya ndani ya mishipa ya damu(endothelium) na pale hii sehemu inapoharibika, basi uume hauwezi kupata mtiririko wa damu nyingi ya kutosha na kusaidia uweze kudindisha. Kimsingi, kitendo cha kudindisha huwa ni tukio la moyo na mishipa yake, na k**a mtiririko wa damu hauwezi kuongezeka kwasababu ya mishipa ya damu haiwezi kupanuka kwa kawaida, basi kutakuwa na mapungufu katika udindishaji wa uume.
NUKUU: Chakula chenye mafuta k**a vile nyama rosti, blue band, nk, kutokufanya mazoezi ambavyo vyote hivi huchangia mwili kuwa mnene pamoja na magonjwa ya moyo vinaweza kusababisha mishipa ya damu kusinyaa na kuwa migumu(atherosclerosis), hali ambayo inaweza kupunguza mwendo kazi wa damu.
Sababu nyingine ya hatari katika upungufu wa nguvu za kiume, ni kupungua kwa kiwango cha homoni ya testosterone, ambayo pia hutokana na unene au kitambi. Viwango vinavyofaa vya homoni hii ni muhimu sana ili kufanikisha uume uweze kudindisha na kuutengeneza mfumo wa uzazi kuwa mzuri. Pale mgonjwa anapokuwa na kiwango kikubwa cha mafuta kwenye kitambi, basi kuna madhara makubwa katika viwango vya homoni ya testosterone.
NUKUU: Kwa wanaume, mafuta kwenye tumbo hubadirisha homoni ya testosterone na kuwa homoni ya estrogen na kusababisha kutokuwa na uwiano sawa wa homoni yaani(hormonal imbalance). Viwango vya homoni ya testosterone haviwezi kukuathiri haraka sana wala kupungua uzito haraka mno, hivyo basi, kunaweza kukawa na uhitaji wa kuandikiwa matibabu kwa ajili ya kuongeza homoni ya testosterone.
Habari Njema Ni Hii!
Utafiti unatuonyesha kwamba, upunguvu wa nguvu za kiume unaweza kuboreshwa kwa kufanya mabadiriko maalumu ya mitindo ya ulaji huku ukitumia tiba! K**a umeathiriwa na unene au kitambi, basi utakuwa umejiruhusu mwenyewe kuingia kwenye hatari kubwa ya ugonjwa wa kisukari, shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa moyo, na hivyo basi, kwa upande wa wanaume, ndipo hutokea hali ya kupungukiwa na nguvu za kiume na kushindwa kushiriki tendo la ndoa. Ogopa unene! Jifunze kula vyakula vyenye afya, fanya mazoezi, na usipende kuvuta sigara. Ukifuata ushauri huu, hakika tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume litatoweka!
NUKUU: Wanaume wanaopunguza uzito au unene, wao huboresha mfumo wa wa uzazi na huwa na nguvu nyingi za kushiriki tendo la ndoa. Kuwa hai zaidi na kutekeleza utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku kutapunguza hatari ya kupungukiwa na nguvu za kiume. Utafiti unaonyesha kwamba, kile kitendo cha kupunguza uzito kwa asilimia 10% tu ndani ya vipindi vya miezi miwili huboresha kabisa mfumo wako wa uzazi na kukufanya uwe na nguvu katika kushiriki tendo la ndoa.
Hakuna Mtu Anayeweza Kusema Kwamba Inaweza Kuwa Ni Rahisi. Ni Mara Nyingi Watu Huwa Na Tumaini Kwamba Itawezekana!
Hivyo, nafahamu kwamba kupunguza uzito huwa sio jambo rahisi tu kulifanya. Wengi wenu wamesumbuka na tatizo la uzito katika maisha yao yote. Unaweza kuwa umeshajaribu kila mlo ili kupunguza uzito lakini bado unateseka na kitambi. Unapaswa uanzie pale ulipo na hatimaye utafute msaada.
Kitu kimoja chenye uhakika ni kwamba, unapohitaji kuwa na ubora wa afya katika mfuko wako uzazi, ni lazima uwe na maisha yenye raha, afya na amani. K**a unateseka na tatizo la kupungukiwa na nguvu za kiume, basi jitahidi kutafuta tiba bora za asili ili kuondoa changamoto hiyo. K**a unateseka na uzito au kitambi na kupungukiwa na nguvu za kiume, basi fanya maamuzi leo kutibu ugonjwa wa wa unene na mpango wa uamuzi. Rudisha mawazo yako nyuma! Anza kula vizuri na anza kuwa unatembea zaidi kila siku. Ninakupa changamoto ya kuanza safari ya maisha yako mapya.!
Tiba Zake
tuna dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo la unene na madhara ya unene k**a vile kupungukiwa nguvu za kiume, nk.
Dawa hizo ni Suma fit kit.