
14/07/2025
Kambi ya Madaktari Bingwa wa Samia Outreach kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kushirikiana na Good Samaritan Cancer Hospital (GSCH) watafanya kampeni ya utoaji wa elimu ya saratani pamoja na uchunguzi wa saratani ya Mlango wa kizazi, saratani ya Tezi dume na saratani ya Matiti bila malipo.
Walengwa:
👉🏼Wanaume wote wa miaka zaidi ya 40.
👉🏼Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 25.
Zoezi hili litafanyika Hospitali ya Good Samaritan Cancer Hospital iliyopo Mashimoni-Ifakara Tarehe 17/07/2025 hadi tarehe 19/07/2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Wote mnakaribishwa