JointGuard

JointGuard Nutritional education

2025 maintain your health
03/01/2025

2025 maintain your health

29/10/2024

*Maumivu ya viungo yanaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na* :

*Maumivu ya misuli:* Haya yanaweza kutokea baada ya mazoezi makali au majeraha.
*Arthritis:* Hii ni hali inayosababisha uvimbe na maumivu katika viungo, k**a vile osteoarthritis au rheumatoid arthritis.
*Infection:* Maambukizi katika viungo yanaweza kusababisha maumivu na uvimbe.
*Marekebisho ya hali ya hewa* : Watu wengine hupata maumivu ya viungo yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.
*Saratani* : Katika hali chache, maumivu ya viungo yanaweza kuwa dalili ya saratani au matatizo mengine makubwa ya kiafya.

*Ikiwa unapata maumivu ya viungo mara kwa mara au yanaathiri maisha yako ya kila siku, ni vyema kutafuta ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari* .
Au wasiliana nasi
MM healthcaretz
0777037407

31/05/2024

Baada ya Alikiba kumchukua mtangazaji wa Clouds FM "Mwijaku" Mtangazaji wawasafi FM, Juma lokole ameibuka namadai yakwamba Crown Media sio ya Alikiba bali niya Boss wa Clouds Media Kusaga ivyo mwijaku kwenda kule wala aistui, Tazama video kwenye comment.👇

31/05/2024

Ushauri kuhusu ulaji wa chakula kwa wagonjwa wa kisukari
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanagharimu fedha nyingi. Kwa hiyo ni muhimu kuzuia na kudhibiti athari za kisukari mapema. Ili kudhibiti ugonjwa wa kisukari mgonjwa anapaswa kupatiwa matibabu sahihi, kufuatilia na kupima hali yake ya afya mara kwa mara pamoja na kuzingatia mtindo bora wa maisha na taratibu zinazofaa za ulaji wa chakula.

Zifuatazo ni kanuni za ulaji unaofaa zinazopaswa kuzingatiwa na mgonjwa wa kisukari:

1.Kula mlo kamili (angalau mara 3 kwa siku) kwa kuzingatia muda mahususi aliojipangia kwani hashauriwi kukaa na njaa kwa muda mrefu.

2.Dhibiti kiasi cha nishati – lishe (wanga) katika chakula ili kisizidi mahitaji ya mwili. Kiasi kitegemee mahitaji ya mtu binafsi.

3.Ongeza ulaji wa vyakula vyenye makapi – mlo kwa wingi. Kiasi kikubwa cha nishati-lishe kitokane na vyakula vya asili ya nafaka isiyokobolewa, mizizi na ndizi za kupika. Sukari inayotoka katika vyakula hivi hufyonzwa kwa taratibu na hivyo kupunguza kasi ya ongezeko la sukari katika damu.

4.Punguza kiasi cha vyakula vinavyozalisha nishati lishe kwa wingi hususani vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

5.Panga utaratibu wa kula chakula na matumizi ya dawa. Iwapo unatumia insulin au dawa za kushusha kiwango cha sukari katika damu unapaswa kujipangia muda wa kula chakula na kumeza dawa ili kuzuia kupungua kwa sukari katika damu. Epuka kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula.

6.Kula mbogamboga kwa wingi katika kila mlo.

7.Kula tunda katika kila mlo.

8.Epuka kunywa pombe.

9.Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi k**a soda, keki, biskuti, p**i na asali.

Kanuni nyingine za kuzingatia ni:

1.Punguza uzito iwapo una uzito uliozidi - au dhibiti uzito wa mwili ili usifikie uzito uliozidi. Ni muhimu kuwa na uwiano sahihi wa uzito wa mwili kulingana na urefu wako.

2.Zingatia usafi na usalama wa chakula

Kwa maelekezo zaidi wasilina nasi
Idala ya lishe na magonjwa
*MM HEALTHCARETZ*
0777037407

TATIZO LA KUOTA MATITI KWA WANAUME NA WATOTO (GYNECOMASTIA)Tatizo la kuota mat**i kwa wanaume na watoto limekuwa kubwa s...
20/05/2024

TATIZO LA KUOTA MATITI KWA WANAUME NA WATOTO (GYNECOMASTIA)

Tatizo la kuota mat**i kwa wanaume na watoto limekuwa kubwa sana katika dunia ya leo. Inawezekana kabisa wakati unatembea njiani ukaona wanaume au watoto wadogo wa kiume wakiwa na mat**i makubwa ambapo watu wengi huchukulia k**a ni kawaida. Kitaalamu gynecomastia ni kukuwa kuliko kawaida yake kwa tishu ya kwenye t**i inayojulikana k**a glandular tissue. Tatizo hili huonekana sana kwa watoto wachanga na wanaume waliokatika umri wa kubaleghe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.

Ukubwa wa tatizo (epidemiology)

Asilimia 60-90 ya watoto wachanga wanapata tatizo hili la kukuwa kwa mat**i kwa mpito linalojulikana kitaalamu k**a transient gynecomastia kutokana na kuwepo kwa kichocheo cha aina ya estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wa mama.

Kati ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika umri wa kubaleghe imeonekana wanapata tatizo hili kutokana na kuwepo kwa wingi kwa kimengenyo aina ya estradiol.Mara nyingi huonekana katika umri kati ya miaka 10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi 18, si kawaida yake kuonekana kwa vijana walio na umri ya zaidi ya miaka 17. Asilimia 24-65 ya watu wazima hupatwa na tatizo hili, hii hutokana na kubadilishwa kwa wingi kwa kichocheo aina ya testerone kuwa estradiol na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo hiki cha testerone kutoka kwenye korodani zinazoanza kuzeeka..Ikumbukwe ya kwamba kichocheo hiki testerone hutengenezwa katika korodani za mwanamume.

Pathofiziolojia (Nini hutokea?)

Kuongezeka ukubwa wa mat**i kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana k**a estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko (sensitivity) wa mat**i kwa kiwango cha zaidi ya kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu.Estrogen husababisha chembechembe zinazojulikana k**a ductal epithelia kuongezeka kwa wingi, kurefuka (ductal elongation) na kugawanyika, kuongezeka kwa chembechembe za mafuta (ductal fibroblasts) na kuongezeka kwa mfumo wa damu kwenye mat**i (increase vascularity).Estrogen hutengenezwa kutoka kwenye vichocheo vya testerone na androgen kwa kutumia kimengenyo kinachojulikana k**a aromatase.

Aina za gynecomastia

•Puffy ni***es – Kuongezeka ukubwa wa chuchu za mat**i kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular tissue.

•Pure glandular gynecomastia – Huonekana sana kwa wale wanaofanya mazoezi ya kujenga mwili (bodybuilders), kutokana na matumizi ya dawa za kujenga mwili (anabolic steroids) ambazo zinakuwa na kiwango kikubwa cha kichocheo aina ya testerone, ambacho hubadilishwa kuwa estrogen. Kwa wanaume wembamba, tatizo hili hutokea kutokana na kuongezeka kwa breast tissue gland pamoja na kuwepo/kutokuwepo kwa tishu aina ya adipose tissue.

Ni nani aliyekatika hatari ya kupata tatizo hili?

•Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50.

•Wenye uzito uliopitiliza (Obesity)

•Unywaji pombe kupindukia

•Magonjwa sugu ya figo au ya Ini

•Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika familia.

Visababishi vya kukuwa kwa mat**i kwa wanaume

•Pseudogynecomastia – Kuongezeka kwa tishu zinazozunguka chuchu za mat**i na huambatana na kuwepo kwa wingi wa tishu aina ya adipose. Mazoezi na kula vyakula venye virutubisho sahihi huondosha tatizo hili.

•Unilateral/asymetrical gynecomastia – Ni kuongezeka kwa t**i moja pekee au la upande mmoja wa mwili wa mwanamume kutokana na sababu mbalimbali. T**i la upande wa pili huwa kwenye umbile na saizi ya kawaida. Bilateral gynecomastia ni kuongezeka kwa mat**i yote mawili.

•Hypogonadism – Kutofanya kazi kwa korodani vizuri na kuwa ndogo. Hii husababishwa na magonjwa mbalimbali k**a klinifelter'rs syndrome, pitituary insuffiency na nk.

•Umri – Kuzeeka pia kumehusishwa kutokea kwa tatizo hili kutokana na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo cha testerone na kuongezeka kwa juhudi za kutengeneza kwa wingi kwa kimengenyo aina ya estradiol kutoka kwenye kichocheo aina ya testerone. Pia mabadiliko ya mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa kwa wale wenye uzito uliopitiliza.

•Uzito uliopitiliza (Obesity) – Watu wenye uzito uliopitiliza hupatwa na tatizo hili kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini na hivyo kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen mwilini mwao na wakati huohuo kupungua kwa kichocheo kingine aina ya testerone.

•Saratani – Baadhi ya saratani k**a saratani ya kwenye korodani, kwenye tezi lililojuu ya figo (adrenal gland), saratani ya tezi la kichwa (pitituary tumor), huharibu mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa wa kuweka sawa vichocheo kati ya uanaume na uanawake (male-female hormonal balance).

•Hyperthyroidism – Kukuwa kwa ukubwa wa tezi la koo (thyroid gland) na hivyo kutengeneza kwa wingi kichocheo aina ya thyroxine.

* Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi (Renal/Kidney failure) - Nusu ya wagonjwa wote wanaotibiwa tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa kutumia hemodialysis hupatwa na tatizo hili la kukuwa kwa mat**i kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance).

•Matatizo ya Ini – Dawa za kutibu magonjwa ya kwenye Ini k**a liver cirrhosis, liver failure husababisha kutokea kwa tatizo hili kutokana na kukosekana kwa uwiano sawa wa mfumo wa vichocheo mwilini.

•Utapia mlo, ukame – Utapia mlo, ukame au kujikondesha husababisha kupungua kwa kichocheo aina ya testerone na kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen na hivyo kuharibu mfumo wa vichocheo mwilini. Hii hutokana na

kukosekana kwa virutubisho sahihi mwilini ambavyo vingi husaidia kurekebisha mfumo wa vichocheo mwilini na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa mbalimbali pamoja na tatizo hili.

•Madhara ya dawa za kurefusha maisha (Antiretroviral therapy) kwa wagonjwa wa ukimwi.

•Utumiaji wa madawa ya kulevya k**a bangi/marijuana.

Vipimo vya Uchunguzi

Vipimo hivi vitafanywa kulingana na historia ya mgonjwa, dalili na viashiria vya mgonjwa baada ya kupimwa na daktari.

•Kipimo cha damu (Complete Blood Count) – Kuangalia wingi wake, aina mbalimbali za chembechembe za damu na uwepo wa maambukizi ya bakteria.

•X-ray ya mat**i (Mammogram) – Hutumiwa kuangalia tishu za kawaida na zile ambazo si za kawaida zilizo kwenye mat**i. Husaidia kugundua uwepo wa saratani, cysts, na calcifications kwenye mat**i.

•Liver function test – Mjumuiko wa vipimo vya damu kuangalia aina mbalimbali za vichocheo na vimengenyo ili kuweza kutambua k**a mgonjwa ana ugonjwa wowote ule wa Ini na chanzo chake, vipimo hivi huangalia albumin, Alanine transaminase (ALT), Aspartate transaminase (AST), Alkaline phosphatase (ALK), Total bilirubin (TBIL), Direct bilirubin (Conjugated Bilirubin), Gamma Glutamyl Transpeptidase (GGT), Lactate Dihydrogenase (LDH).

•Tumor markers – Kipimo cha damu cha kuangalia viashiria vya saratani ya korodani k**a AFP alpha feto 1 protein, Beta-HCG, LDH.

•Kipimo cha damu cha kuangalia wingi wa kichocheo cha aina ya testerone (Total and Free Testerone) Hufanyika asubuhi ambapo kiwango cha testerone huwa juu. Kiwango cha kawaida cha kichocheo cha testerone ni 300 - 1000 ng/dl (Kiwango hiki hupungua kwa asilimia 13 wakati wa mchana).

•Kipimo cha damu cha kuangalia vichocheo vinavyoonekana kwenye ugonjwa wa kukua ukubwa wa tezi la koo ( hyperthyroidism) k**a kichocheo aina ya Thyroid Stimulating Hormone (TSH) ambacho huwa katika kiwango kidogo

wakati wa kuugua ugonjwa wa hyperthyroidism, hutolewa na tezi la kwenye kichwa aina ya pitituary gland, vichocheo vyengine aina ya anti-TSH receptor antibodies (kwa wenye ugonjwa wa Grave’s disease), anti-thyroid – peroxidase

(kwa wenye ugonjwa wa Hashimoto’s disease), na pia kuangalia wingi wa vichocheo aina ya T3 na T4. Kipimo cha Thyroid Scintigraphy pia huweza kutumiwa kutofautisha kati ya ugonjwa wa hyperthyroidism na ugonjwa wa thyroiditis. Kipimo hiki hutumia madini ya mionzi ya iodine (Iodine-131 ama Iodine-123).

•Vipimo vya kuangalia k**a figo zimeshindwa kufanya kazi vizuri k**a;

a)Kipimo cha utendaji kazi wa figo (Renal function tests) ambacho husaidia kuchunguza kiwango cha urea (blood urea nitrogen (BUN) katika damu. Aidha husaidia pia kuchunguza ongezeko la kiwango cha creatinine katika damu.

b)Uchunguzi wa kiwango cha madini mbalimbali katika damu (blood electrolytes)

c)Kupima kiasi cha mkojo kinachotolewa na mgonjwa katika masaa 24

d)Uchunguzi wa mkojo (Urine analysis): Rangi ya mkojo, kiasi cha electrolytes, uwepo wa usaha au damu au casts.

e)Ultrasound ya figo na kibofu cha mkojo

f)Renal biopsy.

Tiba ya Gynecomastia

K**a nilivyosema hapo awali, tatizo hili kwa vijana waliokatika umri mdogo au wa kubaleghe hupotea lenyewe taratibu ndani ya miezi 18. Kwa mzazi unatakiwa usihofu, lakini k**a litaonekana kwa mtoto zaidi ya miaka 17, basi hapa mzazi unatakiwa kuchukua hatua za haraka ambazo ni kumuona daktari ili aweze kukusaidia kwa ufasaha zaidi.

1.Tiba ya madawa

•Tiba ya kutumia vichocheo (Testerone Replacement Therapy) – Kichocheo aina ya testerone hutolewa kwa mgonjwa kwa njia ya mdomoni, kwenye dripu, au kipachiko (patch forms). Hii hutolewa kwa wagonjwa ambao hawawezi

kutoa testerone kutoka kwenye korodani zao kutokana na kupata ajali, ugonjwa au wale ambao hawana korodani kutokana na sababu mbalimbali.

•Dawa aina ya Selective Estrogen Receptor Modulator (SERMs) k**a Tamoxifen, raloxifen, husaidia kupunguza ukubwa (volume) wa mat**i lakini haziondoi tishu zote kwa ujumla. Aina hii ya tiba hutumiwa kwa wale wenye

tatizo sugu la gynecomastia au wale wenye kupata maumivu makali sana. Dawa hizi zina madhara na hivyo ni vizuri kutumia kwa maelekezo ya daktari.

•Dawa aina ya Aromatase Inhibitors k**a anastrozole, hufanya kazi kwa kuzuia kimengenyo aina ya aromatase na hivyo kuzuia utengenezwaji wa kichocheo aina ya estrogen. Tafiti nyingi zilizofanywa zimeshindwa kutoa majibu ya

uhakika juu ya matumizi ya dawa hizi katika kutibu tatizo hili la kukuwa kwa mat**i kwa wanaume.

2.Tiba ya Upasuaji – Kwa wale wenye tatizo hili sugu, upasuaji wa kurekebisha mat**i unaweza kufanyika. Hii humuongezea mwanamume hali ya kujiamini na hivyo kuwa katika hali nzuri kisaikolojia, na huongeza ufanisi wa maisha yake ya kila siku.

3.Kupunguza uzito kwa kufanya mazoezi mara kwa mara na kula mlo wenye virutubisho vyote muhimu.

4.Kutibu chanzo au magonjwa mbalimbali k**a hyperthyroidism, ugonjwa wa figo kushindwa kufanya kazi, saratani mbalimbali na nk.

5.Kuacha kunywa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya k**a bangi/marijuana.

6.Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa baada ya kuona dalili za tatizo hili kwa wale wenye kutumia dawa za kutibu ugonjwa wa Ini, dawa za kurefusha maisha. Kwa wagonjwa wa Ukimwi, ni vizuri kwa daktari kabla ya kumpa

mgonjwa dawa, kumfanyia mgonjwa kipimo cha fasting lipid profile, ili uweze kutambua k**a dawa unazotaka kumpa zitamletea madhara au la. Na

inashauriwa kurudia kipimo hiki kati ya miezi 3 hadi 6 baada ya kuanza dawa hizi za kurefusha maisha au baada ya kumbadilishia mgonjwa dawa. Hata hivyo sio dawa zote za kurefusha maisha zilizo na madhara haya, kwani zipo nyingine zinazopunguza kiwango cha mafuta mwilini na kwenye tishu.

Madhara ya Gynecomastia

1.Uwepo wa tatizo hili kwa muda wa zaidi ya miezi 12 au mwaka mmoja, husababisha mat**i kutengeneza makovu au kwa kitaalamu scarring/fibrosis na hivyo kufanya tiba kwa kutumia dawa kuwa ngumu sana.

2.Wanaume wenye tatizo hili wapo kwenye hatari zaidi ya mara tano ya kupata saratani ya mat**i ikilinganishwa na wanaume ambao hawana tatizo hili.

3.Kuathirika kisaikolojia (kuona aibu, kutojiamini, kujihisi tofauti na wanaume wenzake). Hali hii inaweza hata kumfanya mtu kuishi maisha ya huzuni au kushindwa kujumuika na watu katika shughuli mbalimbali k**a michezo na nk
WhatsApp
+255623713243

17/05/2024

Saratani ya mat**i ni nini?
K**a jina linavyopendekeza, saratani ambayo hukua kwenye seli za mat**i inaitwa saratani ya mat**i (tumor). Ni moja ya saratani zinazotokea sana kwa wanawake. Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, vituo vya matibabu vya juu vimesaidia katika kutambua mapema na matibabu ya saratani ya mat**i, kwa ujumla kupunguza vifo vinavyohusiana na saratani ya mat**i.
Uvimbe wa mat**i ni uvimbe usio na saratani unaopatikana kwenye mat**i moja au zote mbili. Wao ni wa kawaida na hutokea kwa kawaida kutokana na mabadiliko katika mat**i na kuzeeka na mabadiliko ya homoni.

Je! ni aina gani za saratani ya mat**i?
Madaktari wanasema, saratani ya mat**i hutokea kwa sababu ya mgawanyiko wa seli wa haraka, usio na udhibiti katika seli. Kulingana na tishu zinazoathiri, saratani ya mat**i inaweza kuwa:
Ductal carcinoma: saratani ya mirija ya kutoa maziwa
Lobular carcinoma: saratani ya tishu za tezi
Kansa ya mat**i vamizi: Wakati saratani ya mat**i iliyotajwa hapo juu inapoenea kwa tishu zinazozunguka, huitwa saratani ya ductal vamizi na lobular carcinoma vamizi.
Saratani ya mat**i ya metastatic: Saratani ya mat**i inaweza kuenea kupitia damu au limfu hadi kwa viungo vya mbali, mchakato huu huitwa Metastasis. Saratani ya mat**i ya metastatic inaweza kuenea kwa viungo k**a vile mifupa, mapafu, ini, moyo na ubongo.
Saratani ya mat**i ya kiume: Katika hali nadra, saratani ya mat**i inaweza kugunduliwa kwa wanaume. Saratani ya mat**i ya wanaume kwa kawaida hutokana na dawa fulani au viwango vya homoni isiyo ya kawaida (estrogen) au historia kali ya familia ya saratani ya mat**i.
Aina zingine za saratani ya mat**i ambazo hazijajulikana sana ni pamoja na medulary carcinoma, mucinous carcinoma, papilary carcinoma, inflammatory carcinoma, na phyllode tumors.
Ni nini sababu za saratani ya mat**i?
Sababu za saratani ya mat**i inaweza kuwa:
• Homoni
• Historia ya urithi au familia
• Kuvimba
• Maisha
• Vichocheo vya mazingira
Dalili za saratani ya mat**i ni zipi?
Baadhi ya ishara za kawaida kuonekana na dalili za saratani ya mat**i ni:

• Unene au uvimbe ndani ya mat**i, ambayo huhisi tofauti na tishu za jirani
• Mabadiliko ya sura, saizi au mwonekano wa mat**i
• Kutoboka au kutoboka kwa ngozi ya t**i, na kuifanya ionekane k**a ganda la chungwa
• Chuchu iliyogeuzwa, ambayo hapo awali haikugeuzwa
• Kuwa na rangi nyeusi au kuchubuka na kuchubua ngozi karibu na chuchu au mahali popote kwenye t**i
• Mabadiliko ya rangi ya ngozi ya mat**i k**a uwekundu
Ni wakati gani unapaswa kushauriana na daktari?
Iwapo unaona mojawapo ya dalili zilizo hapo juu au una shaka, tembelea daktari wako mara moja. Daktari wako anaweza kukuelekeza daktari wa oncologist, ikiwa inahitajika.
Nani ana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya mat**i?
Kuwepo kwa baadhi ya mambo kunaweza kuongeza hatari ya saratani ya mat**i. Baadhi ya sababu hizo ni:

• Wanawake, haswa wale ambao walipata mtoto wao wa kwanza baada ya miaka 30
• Uzeekaji
• Uzito kupita kiasi/unene kupita kiasi
• Historia ya matibabu ya zamani ya hali ya mat**i au saratani katika moja ya mat**i
• Kesi ya saratani ya mat**i katika familia, k**a vile dada, mama au binti, haswa katika umri mdogo
• Wanawake kwenye tiba ya homoni baada ya kukoma hedhi
• Mfiduo wa muda mrefu kwa mionzi
• Kuanza kwa hedhi mapema (katika umri mdogo) au kuchelewa wakati wa kukoma hedhi (mwisho wa hedhi)
• Unywaji wa pombe kupita kiasi
• Sababu za kijeni: mabadiliko fulani ya jeni yanayoitwa BRCA1 na BRCA2 yamehusishwa na saratani ya mat**i
Je, saratani ya mat**i inaweza kuzuiwa?
Ufahamu wa saratani ya mat**i unaweza kuokoa maisha ya watu wengi. Kuna mambo kadhaa ya maisha ambayo tunaweza kudhibiti ili kupunguza hatari ya saratani ya mat**i. Baadhi ya tahadhari zimeorodheshwa hapa chini:

• Tafuta maoni ya daktari wako kuhusu uchunguzi wa saratani ya mat**i.
• Jifahamishe na muundo wa mat**i yako na ujichunguze mat**i mara kwa mara. Huenda isizuie ugonjwa huo lakini inaweza kusaidia katika kutambua mapema na kudhibiti.
• Kuwa mara kwa mara kwa uchunguzi wa saratani ya mat**i k**a unavyoshauriwa na daktari wako.
• Acha kuvuta sigara na unywaji pombe.
• Shiriki katika mazoezi ya kawaida na kudumisha uzito wenye afya.
• Jadili sababu zako za hatari na oncologist wako. Kulingana na sababu za hatari, oncologist anaweza kushauri dawa za kuzuia au upasuaji, ikiwa inahitajika.
Je, ni hatua gani nne za saratani ya mat**i?
K**a saratani zingine, ugonjwa wa saratani ya mat**i unaendelea kupitia hatua 4. Mapema utambuzi, bora ni mbinu ya matibabu na kasi ni kupona.
Kulingana na eneo la tumor, ushiriki katika node za lymph na kuenea, TNM (tumor, node, metastasis) staging ya tumor hufanyika. Kwa kugundua saratani, daktari wako anapata wazo bora zaidi -
• Tumor iko wapi hasa?
• Je! uvimbe unaenea (pia huitwa metastases ya tumor), ikiwa ni hivyo, huenea kwa nodi za lymph?
• Je, ni ubashiri gani kwa mgonjwa - nafasi za kupona kamili na kuishi?
Saratani ya mat**i inaweza kuhusisha au isihusishe homoni - estrojeni, progesterone, na HER2. Kulingana na hali ya homoni na TNM, daktari hugundua hatua za saratani ya mat**i k**a:
Hatua 0 - Saratani katika hatua hii bado iko kwenye asili ya makosa ya DNA.
Hatua 1 - Hapa, saratani imefungwa kwa eneo ndogo.
Hatua 2 - Katika hatua ya 2, saratani ya mat**i imeanza kukua na kuenea kupitia nodi za lymph.
Matibabu kwa kawaida huhusisha upasuaji na chemotherapy adjuvant (matibabu baada ya upasuaji unaolenga kujaribu kuharibu seli zozote za saratani zilizosalia na au bila tiba ya mionzi).
Hatua 3 - Hatua ya 3A saratani inaashiria kuenea kwa saratani kwenye nodi za limfu, lango la kuingia katika sehemu mbalimbali za mwili. Kupitia hatua ya 3B na 3C, saratani huenea polepole kupitia idadi zaidi ya nodi za limfu na kuvamia tishu zilizo karibu lakini sio viungo vya mbali. Chaguzi za matibabu ni sawa na hatua ya 2.
Hatua 4 - Katika hatua hii, saratani imeenea kwa angalau sehemu moja ya mbali ya mwili - k**a vile ini, mapafu. Hatua ya mwisho ya 4B inaashiria kuenea kwa saratani katika sehemu zaidi ya moja ya mwili.
Kiwango cha kuishi kwa saratani ya mat**i ni nini?
Mara tu mtu anapogunduliwa na saratani, swali la haraka linalokuja akilini ni, "ni nafasi gani za kuishi?"
Kiwango cha kuishi ni makadirio ambayo yanaweza kukuongoza ikiwa unaweza kuishi miaka michache. Asilimia ya viwango vya kuishi vinaonyesha ni watu wangapi wameishi angalau hadi sasa baada ya utambuzi. Kwa mfano, kiwango cha kuishi kwa miaka 5 cha 90% kinaonyesha wagonjwa 9 kati ya 10 wa saratani waliishi kwa angalau miaka 5 baada ya kugunduliwa.

Je, saratani ya mat**i hugunduliwaje?
Ikiwa kuna ishara au dalili yoyote, tembelea daktari wako mara moja, ambaye anaweza kukupeleka kwa oncologist, ikiwa inahitajika. The oncologist anaweza kutambua saratani ya mat**i kwa:
• Kuweka historia kamili ya matibabu
• Uchunguzi wa kimwili wa mat**i yote mawili na pia angalia uvimbe au ugumu wa nodi za limfu kwenye kwapa.
• Uchunguzi wa kuelekeza:
• Mammogram: X-ray ya mat**i
• Ultrasound ya mat**i
• Imaging resonance magnetic (MRI) ya mat**i
• Biopsy ya tishu : Kuondolewa kwa tishu za mat**i kwa uchunguzi na mtaalamu wa magonjwa.
• Biopsy ya nodi ya Sentinel: Mara tu saratani ya mat**i imethibitishwa, wagonjwa mara kwa mara hupitia biopsy ya nodi ya sentinel. Hii husaidia kugundua seli za saratani za inlymph nodi ili kudhibitisha metastasis ya saratani ya mat**i kwenye mfumo wa limfu.

wasiliana na MM healthcaretz
0623713243
kwa msaada zaidi karibumi

16/05/2024

Dondoo muhimu kuhusu mtindo bora wa maisha ili kuzuia na kukabiliana na saratani
Saratani na matibabu yake huweza kumfanya mtu kuwa dhaifu. Ni muhimu sana kwa mgonjwa wa saratani kuzingatia ulaji bora na kufuata mtindo bora wa maisha kwa sababu unasaidia sana kupunguza madhara ya ugonjwa kabla, wakati na baada ya tiba. Hata kwa wale waliugua na kupona saratani wanahitaji kudumisha mtindo bora wa maisha ili kupunguza uwezakano wa saratani kurudi tena.
Hivyo ni muhimu kila mmoja kuzingatia ushauri ufuatao:
Tumia vyakula vitokanavyo na mimea Zaidi:
• Kula mboga-mboga na matunda kwa wingi kila siku.
• Kula mboga-mboga za kijani, njano, nyekundu, zamabarau na rangi nyingine zilizopikwa angalau ujazo wa kikombe kimoja katika kila mlo. Tumia pia mboga zisizopikwa, k**a vile saladi, nyanya, matango n.k; hakikisha mboga-mboga zinazoliwa mbichi zinaoshwa vizuri kwa maji safi na salama.
• Kula matunda ya aina mbalimbali angalau tunda moja katika kila mlo. Kumbuka matunda halisi ni bora kuliko juisi .
• Kumbuka mchanganyiko wa mboga-mboga au matunda yenye rangi mbalimbali huongeza ubora wake.
• Hakikisha katika kila mlo unatumia nafaka zisizokobolewa k**a vile unga wa mahindi wa dona, mchele wa blauni (usiong’arishwa), unga wa ngano usiokobolewa/usiong’arishwa au ngano isiyosagwa, pia ulezi, mtama au uwele kwani havikobolewi; na
• Tumia vyakula mbalimbali vya jamii ya kunde k**a vile maharagwe, kunde, njegere kavu, njugu mawe, dengu, choroko na mbaazi.
Punguza matumizi ya nyama nyekundu.
• Kwa wale wanaotumia nyama nyekundu, ni muhimu kuitumia kwa kiasi, isizidi nusu kilo kwa wiki. Nyama nyekundu ni pamoja na ile ya ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe. Ni vyema kutumia nyama nyeupe k**a samaki au kuku.
Epuka matumizi ya nyama zilizosindikwa.
• Nyama zilizosindikwa ni pamoja na zile zilizohifadhiwa kwa kuongezwa chumvi, mafuta, kemikali au kukaushwa kwa moshi. Nyama hizi zimeonekana kuongeza uwezekano wa kupata saratani. Nyama hizo ni paomoja na nyama za makopo, soseji (hotdogs), bekoni (bacon) n.k.
Kuwa na uzito wa mwili wa wastani.
• Uzito wamwili uliozidi kiasi sio tu huchangia kuongeza uwezekano wa kupata saratani, bali pia huongeza hatari ya uvimbe wa saratani kurudi hata pale ambapo ulishatolewa. Unene uliozidi kiasi pia huongeza uwezekano wa kupata maradhi mengine sugu. Ni muhimu kuwa na uzito wa wastani lakini pia usipungue kuliko invyotakiwa. Kwa mtu mzima ni vizuri kuwa na uzito wenye uwiano wa uzito na urefu (BMI) kati ya 21 na 2. (Pata ushauri Zaidi kuhusu BMI kutoka kwa mtaalamu wa afya/lishe).
• Punguza ulaji wa vyakula vinavyochangia ongezeko la uzito wa mwili kwa haraka hasa vile vyenye mafuta mengi au sukari nyingi.
• Mafuta yatumike kwa kiasi kidogo. Mafuta huupatia mwili nishati-lishe na pia husaidia utumikaji mzuri wa baadhi ya virutibishi mwilini, lakini huhitaji kwa kiasi kidogo. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi. Vyakula hivyo ni pamoja na vile vinavyopikwa kwa kudumbukizwa kwenye mafuta au kukaangwa kwa mafuta mengi. Vyakula hivyo ni k**a chips, vitumbua, maandazi, sambusa, chapati nk. Vyakula hivi ni bora kuviepuka au viliwe mara chache na kwa kiasi kidogo sana.
• Epuka matumizi ya vinywaji, asusa au vyakula vyenye sukari nyingi k**a soda, juisi bandia (vinywaji hivi ni mchanganyiko wa maji, rangi, sukari na ladha bandia), chokoleti, keki, ice-cream nk.
• K**a unaongezeka uzito kuliko kawaida, epuka ulaji wa asusa (vitafunwa) zenye nishati-lishe nyingi kati ya mlo na mlo na badala yake ongeza vyakula vyenye makapi-mlo kwa wingi k**a matunda, mboga-mboga na nafaka zisizokobolewa/zisizong’arishwa.
Punguza matumizi ya chumvi.
• Kwa wastani mwanadamu anahitaji gramu 6 za chumvi kwa siku (sawa na kijiko cha chai kilichojazwa kwa usawa wa bapa au mfuto). Lakini tukumbuke vyakula vingi tayari vina chumvi kwa asili. Ni bora kuongeza ladha kwenye chakulakwa kutumia viungo mbalimbali badala ya chumvi.
• Epuka vyakula vilivyosindikwa kwa kuongeza chumvi na vyakula vilivyoongezwa chumvi nyingi.
• Usiongeze chumvi kwenye chakula wakati wa kula.
Epuka vyakula vilivyoota fangasi au ukungu.
• Vyakula vya aina ya nafaka, jamii ya kunde, karanga au korosho huota ukungu iwapo havikuhifadhiwa vizuri. Ukungu huu husababishwa na fangasi ambazo hutoa sumu iitwayo sumu kuvu “aflatoxin”. Sumu hii ina hatarisha afya na pia huweza kuongeza uwezekano wa kupata baadhi ya saratani.
Epuka utumiaji wa tumbaku au sigara.
• Utumiaji wa tumbaku ikiwa ni pamoja na uvutaji sigara umeonekana kusababisha baadhi ya saratani, hasa zile za mapafu.
• Uvutaji wa sigara pia huingilia na kudhoofisha mfumo wa kinga hivyo kuongeza uwezakano wa kupata baadhi ya saratani.
Epuka matumizi ya pombe.
• Pombe imeonekana kuongeza uwezekano wa kupata aina nyingi za saratani hasa zile za mdomo, koo, mat**i na tumbo. Hivyo kutokana na uhusiano wake na saratani, inashauriwa kuepuka pombe sio tu katika kuzuia bali pia kupunguza uwezekano wa hali ya afya ya mtu mwenye saratani kuwa mbaya Zaidi.
• Pombe huweza kuingilia umeng’enyaji wa chakula na ufyonzaji wa virutubishi mwilini, na pia huingilia uhifadhi wa baadhi ya vitamini na madini mwilini.
Fanya mazoezi ya mwili.
• Kufanya mazoezi ya mwili kila siku kumeonekana kuzuia saratani za aina nyingi. Kutofanya mazoezi ya mwili kumeonekana kuongeza uwezekano wa kupata saratani na pia kuchangia ongezeko la uzito wa mwili. Mazoezi ni paomoja na kutembea, kufanya kazi za nyumbani k**a vile bustani, kufua, kufanya usafi n.k.
• Fanya mazoezi kila siku kuufanya mwili kuwa mkak**avu pamoja na kusaidia chakula kuyeyushwa na kufanya kazi vizuri.
• Anza kwa kufanya mazoezi ya mwili ya wastani k**a vile kutembea harakaharaka angalau dakika 30 kila siku na mwili ukishazoea, ongeza hadi kufikia dakika 60 kila siku. K**a unafanya mazoezi ya nguvu sana, basi iwe angalau dakika 30 kila siku.
• Punguza sana mtindo wa maisha ambao unakufanya uketi bila mazoezi k**a vile kuangalia televisheni kwa muda mrefu au kufanya kazi ukiwa umeketi kwa muda mrefu.
• Kwenye jengo la gorofa tumia ngazi badala ya lifti.
Epuka kutumia virutubishi vya nyongeza (supplements) kwa nia ya kuzuia saratani.
• Virutubishi vya nyongeza havizuii saratani na kuna aina nyingine ya virutubishi vinapotumika k**a nyongeza huchangia kuongeza uwezekano wa kupata saratani. Ni vyema kupata mahitaji yako ya virutubishi kutokana na kula vyakula vya mchanganyiko. Muone daktari kwa ushauri kabla ya kutumia virutubishi vya nyongeza au unapodhani una upungufu wa virutubishi.
Mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama.
• Unyonyeshaji wa maziwa ya mama umeonekana kupunguza uwezekano wa kupata saratani kwa mama na mto. Inashauriwa mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama pekee bila kitu kingine chochote (hata maji) katika miezi sita ya mwanzo. Baada ya miezi sita aendelee kunyonyeshwa na kupewa chakula cha nyongeza hadi atimize miaka miwili au Zaidi.
Mambo mengine yanayoweza kumsaidia mgonjwa wa saratani ni:
• Kunywa maji ya kutosha ili kumaliza kiu.
• Kunywa angalau glasi nane kwa siku
• Maji ya madadu na togwa pia ni vinywaji vizuri iwapo vinapatikana.
• Inapowezekana tumia maziwa ya mgando (mtindi). Maziwa ya mgando huyeyushwa kwa urahisi pia husaidia ufyonzwaji wa virutubishi tumboni kutoka kwene vyakula vingine.
• K**a inawezekana, tumia mafuta ya zeituni kidogo k**a sehemu ya mlo.
• Ongeza matumizi ya viungo mbalimbali k**a vile vitunguu saumu, majani mbalimbali ya viungo, binzari halisi, n.k.

DEPARTMENT OF NUTRITION AND DIETETICS.
MBUZINI DISTRICT HOSPITAL.
O623713243/0747359668

16/05/2024

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NI NINI?
Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko katika shingo ya kizazi. Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea.

Saratani inayoongoza ni ya Mlango wa Shingo ya Kizazi kwa wasatani kwenye kila wagonjwa wa 100 wa Saratani, wanawake 25 wana Saratani hiyo, nyingine ni Saratani ya Mat**i lakini pia Saratani ya Koo ambapo takwimu zinaonesha kuwa katila kila wanawake 1,000 wanawake Sita wana Saratani hiyo.

NINI KINACHOSABISHA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI?
Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99% ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujamiana

BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA HATARI ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
• Kushiriki tendo ndoa katika umri mdogo au chini ya miaka 18.
• Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti.
• Utumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system).
• Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa k**a Ukimwi.
• Uzazi wa mara kwa mara

BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
• Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni
• Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa.
• Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area).
• Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
• Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia.
• Mkojo wenye matone ya Naipenda Yanga, Shabiki Wa Damu

JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA?
Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema. PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST);Pap-Smear ni kipimo ambacho hutumika kuchunguza mabadiliko ya chembe zilizoko katika mlango wa kizazi ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo na hivyo kuwahi kuyakabili mapema.
UMRI WA KUPATA PAP TEST
Test hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65 na chini ya umri wa miaka 21 endapo ameingia katika tendo la ndoa kwa kipindi kisichopungua miaka 3.
KUPUNGUZA HATARI ZASARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
• Pap tests.
Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3,hii itategemea ushauri wa daktari,umri,hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo wako wa maisha.
• Pata HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari) .
• Kuwa na mpenzi mmoja.
Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.
• Tumia kinga (condoms). Hii husaidia kupunguza maambukizi ya maradhi ya zinaa

Address

Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JointGuard posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to JointGuard:

Share