isamilo_specialized_clinic

  • Home
  • isamilo_specialized_clinic

isamilo_specialized_clinic Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from isamilo_specialized_clinic, Medical and health, .

“Leo ni Siku ya Hemophilia Duniani – muda muafaka kwa jamii kujifunza ABC za Hemophilia:Hemophilia si ugonjwa wa kuambuk...
17/04/2025

“Leo ni Siku ya Hemophilia Duniani – muda muafaka kwa jamii kujifunza ABC za Hemophilia:

Hemophilia si ugonjwa wa kuambukiza – ni hali ya kurithi inayosababisha damu kushindwa kuganda haraka.
Wagonjwa wa hemophilia hupata damu kuvuja kwa muda mrefu, hata kwa jeraha dogo au ndani ya mwili bila kuonekana.

Utambuzi wa mapema na matibabu ya kudumu huokoa maisha na kuboresha ubora wa maisha.

Tuelimishe, tuwasaidie, tuwajali.
Isamilo Specialized Clinics inasimama na jamii kwenye kutoa elimu na huduma bora.

Je, unafahamu kuhusu Bawasiri (Hemorrhoids)?Bawasiri ni uvimbe wa mishipa ya damu kwenye eneo la haja kubwa unaoweza kus...
14/04/2025

Je, unafahamu kuhusu Bawasiri (Hemorrhoids)?
Bawasiri ni uvimbe wa mishipa ya damu kwenye eneo la haja kubwa unaoweza kusababisha maumivu, muwasho, na kutokwa na damu kidogo hasa wakati wa haja kubwa.

Sababu kuu:
• Kukosa choo mara kwa mara (constipation)
• Kunywa maji kidogo
• Lishe duni isiyo na nyuzinyuzi
• kunyanyua vitu vizito
• Kukaa muda mrefu bila kusimama

Dalili za Bawasiri:
• Maumivu au muwasho sehemu ya haja kubwa
• Kutokwa na damu kidogo kwenye kinyesi
• Uvimbe au uvimbe unaoshuka wakati wa haja kubwa
• Kuhisi k**a haja haijakamilika

Daraja za Bawasiri na Matibabu:
• Daraja la 1: Mishipa imevimba lakini haishuki – Matibabu: lishe bora, maji mengi, na dawa.
• Daraja la 2: Hushuka wakati wa haja kubwa lakini hurudi yenyewe – Matibabu: lishe, dawa maalum, tiba ya ndani (suppositories).
• Daraja la 3: Hushuka na hurudi kwa mkono – Matibabu: tiba kali zaidi au upasuaji mdogo.
• Daraja la 4: Imetoka kabisa na haiwezi kurudi – Matibabu: upasuaji.

Njia za Kujikinga:
• Kunywa maji ya kutosha kila siku
• Kula mboga mboga na matunda kwa wingi
• Epuka kukaa au kusimama muda mrefu
• Fanya mazoezi mara kwa mara
• Nenda haja kubwa unapojisikia – usicheleweshe

Je, unapata dalili hizi? Usisite kutafuta msaada wa kitaalamu.
Wasiliana nasi leo:
+255 755 413 099

Siku ya Afya Duniani“Mwanzo wenye afya, mustakabali wenye matumaini”Isamilo Specialized Clinics tunasimama imara kwa afy...
07/04/2025

Siku ya Afya Duniani
“Mwanzo wenye afya, mustakabali wenye matumaini”

Isamilo Specialized Clinics tunasimama imara kwa afya ya mama na mtoto!

Tunatoa huduma za Daktari Bingwa kwa akina na watoto kila siku saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku.

Karibu ujipatie huduma bora kwa ajili ya kizazi chenye afya na matumaini

🌙✨ Embracing the spirit of Eid with joy and blessings! From Isamilo Specialized Clinics, we wish you a prosperous and he...
30/03/2025

🌙✨ Embracing the spirit of Eid with joy and blessings! From Isamilo Specialized Clinics, we wish you a prosperous and healthy Eid Mubarak. 🕌💛

🌟 Isamilo Specialized Clinics - Huduma Bora kwa Afya Yako! 🌟👉 Tunakuhudumia kwa upendo na weledi katika idara zifuatazo:...
28/03/2025

🌟 Isamilo Specialized Clinics - Huduma Bora kwa Afya Yako! 🌟

👉 Tunakuhudumia kwa upendo na weledi katika idara zifuatazo:
✅ Kina Mama (Obstetrics & Gynecology)
✅ Watoto (Paediatrics)
✅ Magonjwa ya Ndani (Internal Medicine)
✅ Upasuaji (Surgery)
✅ Macho (Ophthalmology)

⏰ Tuko Wazi:
Jumatatu - Jumamosi
Saa 2:00 Asubuhi - Saa 1:00 Usiku

👩‍⚕️👨‍⚕️ “Afya Yako, Kipaumbele Chetu!”
Njoo ujipatie huduma bora na za kisasa kwa familia yako!

04/02/2024

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when isamilo_specialized_clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to isamilo_specialized_clinic:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share