21/06/2020
*MAUMIVU_YA_TUMBO_LA_HEDHI* *(Dismenorrhea)*
Hujitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni au wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.
Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani. Huanza pale tu yai linapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mrija wakati wa ovulation
*AINA_YA_MAUMIVU*
1: Maumivu yasiyokuwa na sababu zozote kimsingi na kitiba. Hutokea sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Huanza siku moja kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
2: Maumivu yanayojumuisha na sababu nyinginezo za kitiba k**a vile; matatizo ya kizazi, ugonjwa wa nyonga na matatizo katika mirija ya mayai.
Kadhalika imegundilika sababu zinazopelekea kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi
-Umri chini ya miaka 20
-Kuvuja ungo wakati wa miaka 11 au chini
-kutoka damu nyingi wakati wa hedhi
-wanawake ambao hawajawahi kuzaa
magonjwa ambayo husababisha maumivu wakati wa hedhi ni:-
*ENDOMETRIOSIS*, ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kutoka nje ya fuko hilo au hata sehemu nyinginezo
*ADENOMYOSIS,* ni uvimbe au tezi (tumors) ziotazo katika mfuko wa uzazi
*PID* ni ugonjwa wa nyonga au uvimbe katika nyonga
Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi
Pia kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanayoweza kusababisha mtu kupata maumivu ya tumbo la hedhi ni;
Ugonjwa wa nyonga ambao mara nyingi husababishwa na bacteria watokanao na zinaa.
maumivu ya tumbo la hedhi hutegemeana na mtu na mtu. Mwingine anaweza pata dalili zote ma mwingine moja na mwingine baadhi tu au hata dalili moja. Wanawake wengi hujitambua tu bila msaada wa daktari
*MATIBABU*
kwa kawaida hutibika kwa urahisi kwa kutumia dawa za kupunguza maumivu au kwa njia ya tiba lishe kwa kutumia virutubisho ambavyo huweza kukuponesha kabisa na tatizo likaikasha