05/08/2024
*TAFAKARI NENO HILI 👇*
FAHAMU KWAMBA TAARIFA MBAYA HUZAA MAOMBI MABAYA.👇
Nabii Habakuki anainuka k**a nabii kwenye taifa takatifu la
Mungu, Israeli, kipindi ambapo kuna vurugu, madhira na
sintofahamu katikati ya taifa lake. Kuna hali ya kutokosa
utulivu kwenye mifumo ya uongozi na usimamizi ambayo
inapelekea kuwa na hali mbaya ya maisha ya kijamii.
👉🏾Jambo hili linainua hasira na huzuni kwenye moyo wa
Habakuki, nabii. Kiasi kwamba anamwendea Mungu kwa
kilio chenye uchungu na laumu ndani yake:
“Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia
kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.”
Habakuki 1:2
➡️Hapa Habakuki anaenda kwenye maombi ya kulia kidini tu.
Anaenda kutimiza wajibu tu. Kwasababu tayari ameshatoa
hitimisho la mashaka yake juu ya usikivu wa Mungu na
uhusika wake wa kutatua yanayoendelea kwenye nchi:
“… wewe usitake kusikia? ….. ila hutaki kuokoa.”
👉🏾Umewahi kwenda kwenye maombi wakati ukijitazama ndani
ya kilindi cha moyo wako una hali k**a ya Habakuki?
Umewahi kumtilia Mungu mashaka kwamba hatatenda? Au
haoni?
Hali hii huwatokea watu wanapoenda kwenye maombi hali
wakilitazama tatizo, wakilichambua na kulielewa sana kiasi.👇
kwamba wanao ushahidi wote ya kwamba Mungu amechagua
kukaa kimya mambo yajiendee au amewakasirikia watu, na
hivyo hatahusika kwa chochote.
➡️Ni vizuri ukajua ya kwamba BWANA hutazama nia ya moyo –
huona sirini. Huwezi kuigiza mbele yake. Hivyo basi, k**a
una mashaka juu yake, usijaribu kuigiza kwamba uko sawa.
Itakupelekea kuwa mtu wa laumu badala ya kuomba.
👉🏾Habakuki anazungumza juu ya “habari ya KULALAMIKA
kwangu...”’ Si maombi tena!
Ukitazama kwa jicho la kujifunza utagundua ya kwamba
Habakuki anaendelea na malalamiko japokuwa yuko kwenye
maombi ni kwasababu ya kutotosheka na mpango wa Mungu. 👇
Namna ambavyo alikuwa anatekeleza swala la kuondosha
uovu kwenye taifa lake takatifu.