22/04/2024
CHAKULA cha Kuzuia Kuzeeka Haraka..!!!
ILI kudumisha muonekano wa ujana kwa mwili wako unahitaji kuupa mahitaji yake yaliyobadilika. Kuzuia kuzeeka haraka unahitaji chakula chenye calcium ya kutosha kuipa mifupa yako nguvu na kupata chakula chenye collagen kwa wingi ili kuifanya ngozi yako isiwe na makunyanzi mwilini, kiashiria cha uzee.
Mwili una uwezo wa kudhibiti madhara yanayotokana na uwepo wa free radicals kwa kiasi fulani, lakini idadi ikizidi mwili huzidiwa na madhara mengi hutokea, yakiwepo kuzeeka kwa mwili na magonjwa mengi k**a kansa, magonjwa ya moyo, mifupa (arthritis), usahaulifu (Alzheimer’s), ugonjwa wa parkinson’s na kisukari.
Free radicals katika mwili huweza kuongezeka kwa kutumia vitu kutoka nje ya mwili. Sumu kutoka nje zinazozalisha free radicals katika mwili ni pamoja na hewa chafu hasa inayotoka kwenye viwanda, moshi wa sigara, na chakula chenye dawa za kuulia wadudu na utumiaji wa pombe kwa kiwango cha kuzidi kiwango.
Kiwango kidogo cha free radicals kinachozalishwa na mwili wenyewe kinaweza kikadhibitiwa vizuri na kemikali nyingine zinazoitwa antioxidants ambazo nazo pia huzalishwa na mwili.
Free radicals za ziada zinazozalishwa na vitu kutoka nje ya mwili zisipodhibitiwa kikamilifu husababisha madhara mengi pamoja na magonjwa yaliyotajwa hapo juu.
Hivyo basi tunahitaji kupata chakula chenye antioxidants kwa wingi ili kuisaidia miili yetu kupambana na kemikali hizi za ziada. Kuna aina nyingi za antioxidants zikiwemo vitamini C, vitamini E, flavonoids na polyphenols kwa kutaja tu bila kuingia kwa undani zaidi.
Baada ya utangulizi huo, sasa ni wakati wa kupitia chakula ambacho kikitumiwa kitakupa vitu tulivyovitaja hapo juu na kuufanya mwili wako kuwa na mwonekano wa ujana daima.
Vitamini C
Katika utafiti wa Mtafiti Herman uliofanywa kwenye kikundi cha wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40 ulionyesha kwamba wanawake wanaotumia chakula chenye vitamini C zaidi walikuwa na makunyanzi zaidi na ngozi zao hazikuwa kavu ukilinganisha na wale ambao walitumia vitamini hiyo kidogo.
Hii ni kwa sababu vitamini C ni antioxidant yenye nguvu inayozuia uharibifu wa seli na DNA za seli hivyo kulinda uzalishaji wa collagen