Lubonji Wa Lubonji

Lubonji Wa Lubonji L.W.L MUSIC & INTERNATIONAL NEWS

HADITHI YA REBO TCHULOL'HISTOIRE DE REBO TCHULO Amezaliwa mwaka 1997 mjini Kinshasa, Rebo Tshulo, ambae jina lake halisi...
12/04/2026

HADITHI YA REBO TCHULO
L'HISTOIRE DE REBO TCHULO

Amezaliwa mwaka 1997 mjini Kinshasa, Rebo Tshulo, ambae jina lake halisi ni Déborah, ni miongoni mwa Wasanii wa kizazi kipya walioleta upekee mpya katika Muziki wa Congo.
Kalelewa katika mazingira yenye mchanganyiko wa ibada za kidini na harakati za kisanii za jiji, jambo lililomjengea msingi wa kipaji chake tokea utotoni.

Lwanzoni kaanza kufahamika kwa jina la Rebelle (Muasi) na hapo baadae akaja kuibuka na jina la Kisanii la "Rebo", ambalo likaja kuwa alama ya safari yake ya ubunifu.

Umaarufu wake uliongezeka mwishoni mwa miaka ya 2010, hasa baada ya kushirikiana na Ferré Gola mwaka 2019.

Aina yake ya Muziki inayochanganya Afrobeat, Rumba ya kisasa na ladha ya Pop ya mijini ulimfanya kuwa Msanii mwenye mvuto wa kipekee.

Nyimbo zake k**a “Pepele”, “Mboté”, “Contaminée”, “Mukaji Internationale”, pamoja na “Loketo Remix” iliyotamba sana kwenye TikTok mwaka 2023, zilimpa nafasi ya pekee katika Tasnia ya Muziki.

Mwaka 2024, alithibitisha umahiri wake kupitia “Choquer”, uliotazamwa zaidi ya mara milioni tatu.

Katika maisha yake binafsi, Rebo aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Msanii Innoss’B, na pamoja wakabarikiwa kupata mtoto.

Ingawa kwa sasa wametengana, hatua hiyo imebaki kuwa sehemu muhimu ya historia yake, bila kupunguza nguvu ya safari yake ya Kisanii.

Safari yake imeendelea kuimarika kupitia ushirikiano wake na wa Sanii wengine wenye majina yao k**a Innoss’B, Samarino, Awilo Longomba, Yemi Alade na Ferré Gola.

Akiwa amevutiwa na Wanamuziki k**a Fally Ipupa na Barbara Kanam, Rebo ameweza kuunganisha urithi wa Congo na mitindo ya kisasa kwa ustadi wa hali ya juu.

Mwaka 2023, ushiriki wake katika tamasha la kibinadamu Umoja huko Brussels ndo ukawa hatua muhimu katika kupanua upeo wake wa kimataifa.

Mwaka 2025, aliandika historia kwa kuwa Mwanamke wa kwanza wa Congo kusaini mkataba na Def Jam Africa, jambo lililothibitisha nafasi yake k**a Msanii mwenye ushawishi mkubwa na mwakilishi wa kizazi kipya cha Muziki wa Congo.

Version Française :
HISTOIRE DE REBO TCHULO

Née en 1997 à Kinshasa, Rebo Tshulo, dont le nom civil est Déborah, appartient à cette génération d’artistes congolaises qui ont introduit une singularité nouvelle dans le paysage musical de la RDC.

Elle a grandi dans un environnement où se mêlaient la ferveur des pratiques religieuses et l’effervescence artistique de la capitale, un contexte qui a façonné dès l’enfance les fondations de son talent.

À ses débuts, elle se fait connaître sous le nom de Rebelle (Muasi), avant d’adopter plus t**d le nom de scène «Rebo», qui deviendra l’emblème de son identité créative et de son parcours artistique.

Son ascension s’accélère à la fin des années 2010, notamment après sa collaboration avec Ferré Gola en 2019.

Son style musical, qui marie afrobeat, rumba contemporaine et esthétique pop urbaine, lui confère une aura singulière et un charme artistique distinctif.

Des titres tels que «Pepele», «Mboté», «Contaminée», «Mukaji Internationale», ainsi que «Loketo Remix», devenu viral sur TikTok en 2023, lui ouvrent une place privilégiée au sein de l’industrie musicale congolaise.

En 2024, elle confirme son talent avec le titre «Choquer», qui dépasse les trois millions de vues.

Sur le plan personnel, Rebo a vécu une relation amoureuse avec le chanteur Innoss’B, relation dont est né un enfant.

Bien qu’ils soient aujourd’hui séparés, cet épisode demeure une composante importante de son histoire, sans jamais diminuer la force ni l’autonomie de sa trajectoire artistique.

Sa carrière continue de s’enrichir grâce à des collaborations avec des artistes de renom tels qu’Innoss’B, Samarino, Awilo Longomba, Yemi Alade et Ferré Gola.

Inspirée par des figures majeures comme Fally Ipupa et Barbara Kanam, Rebo parvient à unir avec finesse l’héritage musical congolais et les tendances contemporaines, témoignant d’une maîtrise artistique remarquable.

En 2023, sa participation au concert humanitaire Umoja à Bruxelles marque une étape décisive dans l’élargissement de son rayonnement international.

Puis, en 2025, elle inscrit son nom dans l’histoire en devenant la première femme congolaise à signer avec Def Jam Africa, consacrant ainsi son statut d’artiste influente et de représentante emblématique du renouveau musical féminin en RDC.

BABA L.W.L

JB MPIANA NA BINTI YAKE SORAYA AMBAE LEO NI B'DAY YAKE.ANATIMIZA MIAKA 29.ALIZALIWA TAREHE 12/04/1997.BABA L.W.L
12/04/2026

JB MPIANA NA BINTI YAKE SORAYA AMBAE LEO NI B'DAY YAKE.
ANATIMIZA MIAKA 29.
ALIZALIWA TAREHE 12/04/1997.

BABA L.W.L

KOFFI OLOMIDE KATI YA FALLY NA FERRÉ NAWACHAGUA WOTE WAWILI.Koffi Olomide alipoulizwa kwa namna gani Fally Ipupa na Ferr...
12/04/2026

KOFFI OLOMIDE
KATI YA FALLY NA FERRÉ
NAWACHAGUA WOTE WAWILI.

Koffi Olomide alipoulizwa kwa namna gani Fally Ipupa na Ferré Gola walivyojiunga na Quartier Latin International,
Koffi Olomide alijibu kwa mzaha wake wa kifasihi:
«Jina langu ni Koffi, na lina herufi mbili F.
Kwa hiyo kati ya Fally na Ferré, nawachagua wote wawili».

Kujiunga kwa Fally Ipupa
Koffi ameeleza kuwa Fally aliingia Quartier Latin wakati baadhi ya Wanamuziki walikuwa wameondoka ili kuanzisha Group lao la (Academia).

Katika harakati ya kuimarisha upya Group lake, Koffi aliwaomba Jamaa zake kadhalika na wasaidizi wake wamletee vijana wawili wenye muonekano mzuri, wanaojua kuimba na kucheza.
Ndivyo Fally alivyoletwa mbele yake.

Koffi alimwomba aimbe wimbo wa Quartier Latin. Fally akasema wala hazimudu vizuri nyimbo za Quartier Latin, lakini kajitahidi kuimba nyimbo chache alizozijua.

Kisha Koffi akamwambia acheze.
«Alipoanza kucheza, ilikuwa mshangao Mkubwa kabisa.
Tulipigwa na bumbuwazi kuona anavyo cheza kwa umaridadi na ustadi wa hali yajuu kabisa.

Kwa ukweli alicheza kwa hali ya ajabu kabisa.

Kwa sababu ya kipaji chake na makubaliano ya wote waliomwona, Koffi alimwambia papo hapo:
«Unaingia kwenye Group langu».

Kuhusiana na Ferré Gola.
Koffi anakumbuka tukio maalum.
Alikuwa anafanya Show kwenye Mtaa mmoja wa Kinshasa, Show ya kermesse lililokusanya karibu watu elfu kumi.

Kabla ya Show kuanza, kijana mmoja alikuwa akiimba k**a fungua pazia kwa sauti ya kipekee.

Koffi akauliza:
«Huyu kijana anayeimba vizuri hivi ni nani?»

Wakamjibu kuwa ni kijana wa mtaa ambaye huwashangaza Watu kila mara.

Koffi akaomba wamlete. Wakamwendea na kumnong’oneza kuwa Koffi Olomide anahitaji kuzungumza naye.

Kijana akaja.
Koffi akamwambia:
«Unaimba kwa ustadi wa ajabu. Wewe ni nani?»
Akajibu : «Naitwa Ferré».

Koffi akamwambia kuwa anasafiri, lakini akirudi angependelea ajiunge na Quartier Latin.

Koffi alivyorudi, akagundua kuwa Ferré tayari amejiunga na Wenge Musica BCBG 4X4 TOUT TERRAIN.

Aliendelea kumfuatilia hadi alipoondoka Wenge Maison Mère na kuanzisha Les Marquis de Maison Mère.

Baadae, Ferré alimtafuta na kuomba wakutane. Walizungumza kwa kina, na Koffi akakubali masharti yake yote, mradi tu akubali kujiunga na Quartier Latin.
Ndivyo ushirikiano wao ulivyoanza.

Version Française

KOFFI OLOMIDE
ENTRE FALLY ET FERRÉ,
JE LES CHOISIS TOUS LES DEUX.

Lorsqu’on demanda à Koffi Olomide de raconter comment Fally Ipupa et Ferré Gola avaient intégré le Quartier Latin International, il répondit avec une pointe d’esprit :
«Mon prénom est Koffi, et il comporte deux F.
Ainsi, entre Fally et Ferré, je les choisis tous les deux».

L’entrée de Fally Ipupa
Koffi expliqua que Fally avait rejoint le Quartier Latin à une période de recomposition, lorsque certains musiciens avaient quitté l’orchestre pour fonder leur propre groupe (Academia).

Souhaitant revitaliser sa formation, il demanda à ses proches et collaborateurs de lui présenter deux jeunes artistes au port soigné, capables de chanter et de danser.
C’est dans ce contexte que Fally fut conduit devant lui.

Koffi lui demanda d’interpréter un titre du Quartier Latin.
Fally reconnut qu’il ne maîtrisait pas encore pleinement le répertoire, mais il chanta néanmoins quelques morceaux qu’il connaissait.
Puis Koffi l’invita à danser.

«Lorsqu’il s’est mis à danser, ce fut un véritable choc.
Nous sommes restés stupéfaits devant tant d’élégance, de précision et de virtuosité.
À vrai dire, sa prestation relevait de l’extraordinaire».

Séduit par son talent et constatant l’unanimité autour de lui, Koffi lui déclara immédiatement :
«Tu entres dans mon groupe».

La découverte de Ferré Gola
À propos de Ferré, Koffi évoque un souvenir marquant.
Il donnait un concert dans un quartier populaire de Kinshasa, une grande kermesse rassemblant près de dix mille personnes.

En lever de rideau, un jeune homme chantait avec un timbre singulier et saisissant.

Koffi demanda :
«Qui est ce jeune qui chante avec une telle maîtrise?»
On lui répondit qu’il s’agissait d’un garçon du quartier, habitué à émerveiller le public.

Koffi demanda qu’on le lui amène.
On alla lui murmurer que Koffi Olomide souhaitait lui parler.
Le jeune homme s’avança.
Koffi lui dit :
«Tu chantes avec une virtuosité remarquable. Qui es‑tu ?»
Il répondit : «Je m’appelle Ferré».

Koffi l’informa qu’il devait voyager, mais qu’à son retour, il souhaiterait l’intégrer au Quartier Latin.

À son retour, il découvrit que Ferré avait déjà rejoint Wenge Musica BCBG 4x4 Tout Terrain.

Il continua néanmoins à suivre son parcours, jusqu’à ce que Ferré quitte Wenge Maison Mère pour fonder Les Marquis de Maison Mère.

Plus t**d, Ferré reprit contact avec lui et sollicita une rencontre.

Ils eurent un long entretien, au terme duquel Koffi accepta toutes ses conditions, à la seule exigence qu’il rejoigne le Quartier Latin.
Ainsi débuta leur collaboration.

BABA L.W.L

HADITHI YA FALLY IPUPA NA MKEWE NANA KETCHUP BAFANA HERI YA SIKU YA KUZALIWA YA NANA Nana_Ketchup.bafana FanHOMMAGE À NA...
10/04/2026

HADITHI YA FALLY IPUPA NA MKEWE NANA KETCHUP BAFANA
HERI YA SIKU YA KUZALIWA YA NANA Nana_Ketchup.bafana Fan
HOMMAGE À NANA KETCHUP :
CELLE QUI A CRU EN FALLY AVANT LE MONDE
JOYEUX ANNIVERSAIRE

1. Hadithi ya Fally Ipupa na Nana Ketchup ni miongoni mwa simulizi nzuri zaidi za uaminifu, uvumilivu na ustahimilivu katika Sanaa ya Congo.
Safari yao ya pamoja ilianza kwenye miaka ya 1998, muda mrefu kabla ya Fally kuwa Nyota wa Kimataifa, na inaonyesha upendo uliojengwa katika unyenyekevu na kuaminiana.

2. Wakati huo, Fally alikuwa kijana mwenye ndoto nyingi lakini asiye na uwezo.
Nana Ketchup ndie aliyekuwa kati ya Watu wamwanzoni kabisa kutambua kipaji chake cha kipekee na hatima yake ya juu. Alimsaidia bila kuchoka kiakili, kifedha na kihisia hata kabla dunia haijamtambua.

3. Kabla ulimwengu haujamjua “Dicap la Merveille”, Nana Ketchup alimlea kwa uangalifu wa pekee: alimsaidia kuvaa, kumwandalia chakula, kumtia moyo katika mazoezi yake na kuamini mustakabali wake bila kuyumba.
Kwake yeye, Fally hakuwa tu Msanii, bali Mwanaume mwenye thamani.

4. Mnamo 1 Septemba 2002, walibarikiwa kumpata Mtoto wao wa kwanza, Marcosins Ipupa, ishara ya upendo wao wa ujana.
Baadae walipata watoto wengine: Vincizo, Jaden, Malka Monickel na Fannalya, kila mmoja akiwa sura mpya ya safari yao.

5. Miaka ilivyopita na kazi ya Fally ikawa ya kimataifa, Nana Ketchup alibaki kuwa nguzo thabiti.
Hakuwahi kutafuta umaarufu; alichagua kuwa nyuma ya pazia ili kuimarisha familia na kumsaidia mume wake kimya kimya.

6. Uaminifu wake usioyumba ulimgusa sana Fally, ambae mara nyingi amesisitiza kuwa Nana Ketchup ndiye Mtu wa kwanza kumwamini, kumpenda bila masharti na kusimama naye katika nyakati ngumu zaidi.

7. Hadithi yao inatukumbusha kuwa nyuma ya mafanikio makubwa, mara nyingi kuna nguvu tulivu, moyo wenye subira na roho yenye ustahimilivu.
Nana Ketchup ndiye mfano wa nguvu hiyo, Mwanamke aliyevumilia na kusimama imara licha ya changamoto.

8. Wawili hawa wamekuwa mfano wa upendo wa kudumu, heshima ya pande mbili na uthabiti katika tasnia yenye misukosuko mingi. Safari yao inaonyesha kuwa mafanikio ni matokeo ya kazi ya pamoja, msaada wa dhati na maono ya pamoja.

9. Kwa leo hii, Fally Ipupa akiwa mmoja wa Wasanii wakubwa zaidi barani Afrika, bado hamwachi kumkumbuka Mwanamke aliyesimama naye tokea mwanzoni.
Hadithi yao ni ushahidi kuwa subira hulipa na upendo wa dhati hushinda majaribu ya muda.

10. Katika siku hii maalum, tunampongeza Nana Ketchup Bafana, mwanamke wa ujasiri, uaminifu na moyo mkuu.
Heri ya siku ya kuzaliwa kwa yeye ambaye upendo na uwepo wake umechangia kumjenga Msanii anayeheshimiwa duniani kwa leo hii. Mwenyezi Mungu amzidishie furaha, afya na baraka tele.

HOMMAGE À NANA KETCHUP :
CELLE QUI A CRU EN FALLY AVANT LE MONDE
JOYEUX ANNIVERSAIRE

1. L’histoire de Fally Ipupa et de son épouse Nana_Ketchup.bafana compte parmi les plus belles pages de fidélité, de patience et de résilience que la musique congolaise ait connues.
Leur parcours commun débute en 1998, bien avant que Fally ne devienne une icône internationale, et témoigne d’un amour construit dans la simplicité, l’humilité et la confiance mutuelle.

2. À cette époque, Fally n’était qu’un jeune homme animé de rêves immenses mais dépourvu de moyens.
Nana Ketchup fut l’une des toutes premières personnes à reconnaître l’exceptionnalité de son talent et la grandeur de sa destinée. Elle l’a soutenu sans relâche moralement, financièrement et émotionnellement bien avant que le monde ne découvre son nom.

3. Avant que la planète ne connaisse «Dicap la Merveille», Nana Ketchup veillait sur lui avec une attention rare : elle l’aidait à s’habiller, lui préparait ses repas, l’encourageait dans ses répétitions et croyait en son avenir avec une conviction inébranlable.
Pour elle, Fally n’était pas seulement un Artiste en devenir, mais un Homme de valeur.

4. Le 1er septembre 2002, ils accueillirent leur premier enfant, Marcosins Ipupa, symbole vivant de leur amour de jeunesse.
Par la suite, leur famille s’est agrandie avec Vincizo, Jaden, Malka Monickel et Fannalya, chacun représentant un nouveau chapitre de leur histoire et de leur complicité.

5. Au fil des années, alors que la carrière de Fally prenait une dimension internationale, Nana Ketchup demeura une présence stable et essentielle.
Elle n’a jamais recherché la lumière ; elle a choisi de rester dans l’ombre pour préserver leur foyer, soutenir son mari et maintenir l’équilibre familial avec une discrétion admirable.

6. Cette loyauté sans faille a profondément marqué Fally, qui rappelle souvent que Nana Ketchup fut la première à croire en lui, à l’aimer sans condition et à rester à ses côtés dans les moments les plus difficiles.
Elle est pour lui un repère, une force et une source de gratitude infinie.

7. Leur histoire nous enseigne que derrière chaque grande réussite se cache souvent une force silencieuse, un cœur patient et une âme persévérante.
Nana Ketchup incarne cette force : une Femme qui a su tenir bon, affronter les défis et demeurer constante malgré les épreuves.

8. Ensemble, ils sont devenus un symbole d’amour durable, de respect mutuel et de stabilité dans un milieu souvent marqué par l’instabilité.
Leur parcours démontre que la réussite est le fruit d’un travail commun, d’un soutien sincère et d’une vision partagée.

9. Aujourd’hui, alors que Fally Ipupa est reconnu comme l’un des plus grands Artistes du continent africain, il n’oublie jamais celle qui l’a accompagné depuis ses débuts.
Leur histoire est la preuve que la patience finit toujours par porter ses fruits et que l’amour véritable triomphe du temps et des épreuves.

10. En ce jour si particulier, nous rendons hommage à Nana Ketchup Bafana, femme de courage, de loyauté et de cœur.
Joyeux anniversaire à celle dont l’amour, la présence et la force ont contribué à façonner l’homme et l’artiste admiré dans le monde entier. Que Dieu lui accorde davantage de joie, de santé et de bénédictions.

BABA L.W.L

WANAMUZIKI WAWILI WA FERRE GOLA, CHARLY SOLO NA LIMOUSINE FERRARI, WATOWEKA BAADA YA SHOW YA ACCOR ARENA (BERCY) JIJINI ...
10/04/2026

WANAMUZIKI WAWILI WA FERRE GOLA, CHARLY SOLO NA LIMOUSINE FERRARI, WATOWEKA BAADA YA SHOW YA ACCOR ARENA (BERCY) JIJINI PARIS TAREHE 04/04/2024 :
ISHARA YA MGOGORO WA KIMFUMO KATIKA MUZIKI WA CONGO

1. Tukio la kutoweka kwa Charly Solo na Limousine Ferrari baada ya show ya kihistoria ya Ferre Gola katika ukumbi wa Accor Arena jijini Paris tarehe 04/04/2024 si jambo geni kwenye Tasnia ya Muziki wa Congo.
Wanamuziki hawa hawakurudi Kinshasa, na kitendo chao kinaendelea kuibua swali lile lile: kwa nini Wanamuziki wengi wa Congo hutumia ziara za nje k**a fursa ya kutoweka kabisa?

2. Kuzamia kwa wanamuziki wa Congo wakati wa ziara za Ulaya ni jambo lililodumu kwa zaidi ya miaka ishirini.
Mwaka 2004, wakati wa ziara ya Wenge Musica Maison Mère nchini Uingereza, Wanamuziki kadhaa wakiwemo : Ferré Gola,JDT Mulopwe, Bill Clinton Kalonji, walamua kujiondoa na kuanzisha Group lao (Les Marquis de Maison-Mère), wakifuatiwa na Serge Mabiala, Japonais Maladi, Mimiche Bass na wengine.

3. Mwaka 2021, Group (Villanova) la Fabregas lilipoteza wanamuziki 17 wakiwemo : Christelle, Philo Mbuyi, Brassard, Zoulou, Joël Synthé, Blanchard Basse, Impact, Phraseologie, Kenete na Mbonda, na Madansa wawili waliotoweka nchini Ufaransa.
Tukio hili lilionyesha kwa mara nyingine tena udhaifu wa mifumo ya usimamizi wa Muziki Nchini Congo na kuendeleza mtiririko wa matukio ya aina hii.

4. Tokea miaka ya 1990, Group k**a Zaïko Langa Langa, Quartier Latin, Wenge BCBG, Viva La Musica na mengine yamewahi kupoteza Wanamuziki waliotumia ziara za nje k**a njia ya kuzamia. Matukio haya yameathiri vibaya Taswira ya Muziki wa Congo kimataifa na kuibua mjadala mpana kuhusu sababu zake.

5. Sababu kuu zinazochangia hali k**a hii ni pamoja na umaskini, kutokuwa na utulivu wa kifedha, kutolipwa mishahara ya uhakika, kukosa mikataba rasmi ya kazi, kumtegemea Leader wa Group kwa kila jambo na kukosa ulinzi wa kijamii.
Kwa wengi, ziara ya nje huwa k**a njia pekee ya kukimbia maisha magumu.

6. Ndoto ya Ulaya k**a “Eldorado” pia inachochea kutoweka kwa Wanamuziki.
Ulaya huonekana k**a mahali pa uhuru wa Kisanii, usalama wa kijamii na fursa za kiuchumi, hata k**a mara nyingi Taswira hii imepambwa kupita kiasi.
Wengine hukimbia kutokana na migogoro ya ndani, upendeleo, fitina na usaliti unaopandikizwa na Watu wa karibu na viongozi wa Group.

7. Shinikizo la familia na jamii pia ni sababu muhimu, kwani katika fikra za watu wengi hasa barani Afrika, mafanikio yanahusishwa na kuhama nchi.
Wengine husukumwa moja kwa moja na familia zao kutotaka kurudi.
Zaidi ya hapo, kukosekana kwa sheria na mifumo ya kuwalinda Wasanii kunafanya mazingira ya kazi kuwa magumu na yasiyo na usalama.

8. Madhara ya hali hii ni makubwa sio tuu kwa viongozi wa Goup,bali pia kwa Wasanii na kwa Taswira ya Taifa.
Viongozi hupoteza uaminifu kwa mapromota, hupata shida yakupewa tena visa na mipango ya muziki huvurugika.
Muziki wa Congo hupata sifa mbaya ya ukosefu wa nidhamu na Wasanii kutokuaminika Ulaya, jambo linalochelewesha maendeleo ya sekta.

9. Kwa wanamuziki wanaobaki Ulaya, wengi hukutana na changamoto ya kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi, kukosa makazi, kufanya vibarua visivyo vya Muziki, upweke, msongo wa mawazo na ndoto zao za Muziki kufifia.
Suluhisho linahitaji Viongozi wa Group kuwajibika, kuweka mikataba rasmi, kulipa kwa wakati, kupambana na fitina na kuwathamini Wanamuziki.

10. Serikali ya Congo inapaswa kutunga na kutekeleza sheria za kuwalinda Wasanii, kuanzisha bima ya kijamii, kuunda mfuko wa kusaidia Sanaa na kuimarisha diplomasia ya kitamaduni.
Matukio k**a haya ya Charly Solo, Limousine Ferrari, Wanamuziki 17 wa Fabregas mwaka 2021 na lile la Wenge Maison Mère mwaka 2004 si bahati mbaya bali ni dalili za mfumo uliodhoofika.
Bila mageuzi ya kina, Wanamuziki wataendelea kuzamia na muziki wa Congo utaendelea kupoteza hadhi yake.

Version Française

1. Le 4 avril 2024, à l’issue du concert triomphal de Ferre Gola à l’Accor Arena de Paris, un phénomène devenu presque banal dans la Musique Congolaise s’est reproduit : les musiciens Charly Solo et Limousine Ferrari ont choisi de ne pas regagner Kinshasa.
Leur disparition, loin d’être un incident isolé, s’inscrit dans une longue tradition de fuites lors des tournées européennes, où de nombreux artistes transforment ces déplacements en opportunités de départ définitif.
Cette répétition interroge profondément la structure même du secteur musical congolais.

2. Ce phénomène n’est pas nouveau.
Depuis plus de deux décennies, il marque l’histoire de la musique congolaise moderne.
En 2004, lors d’une tournée de Wenge Musica Maison Mère à Londres, plusieurs musiciens dont : Ferré Gola, JDT Mulopwe, Bill Clinton Kalonji refusèrent de rentrer au pays et fondèrent leur propre formation, (Les Marquis de Maison-Mère), bientôt rejoints par Serge Mabiala, Japonais Maladi, Mimiche Bass et d’autres.
Cet épisode spectaculaire demeure l’un des tournants majeurs de la scène musicale congolaise.

3. En 2021, un événement tout aussi marquant survint lorsque le groupe (Villanova) de Fabregas perdit dix-sept musiciens, dont les artistes Christelle, Philo Mbuyi, Brassard, Zoulou, Joël Synthé, Blanchard Basse, Impact, Phraseologie, Kenete na Mbonda, ainsi que d’autres membres du staff, tous disparus en France.
Cette fuite massive révéla une fois de plus les failles profondes du système de gestion artistique en République démocratique du Congo.

4. Depuis les années 1990, des musiciens issus de Zaïko Langa Langa, Quartier Latin, Wenge BCBG, Viva La Musica et d’autres formations prestigieuses ont eux aussi profité de leurs tournées pour s’établir en Europe.
Ces départs répétés ont progressivement altéré la réputation internationale de la Musique Congolaise, souvent perçue comme indisciplinée ou instable par les promoteurs étrangers.

5. Les causes de ces départs sont multiples :
La précarité économique constitue l’un des facteurs les plus déterminants : la majorité des Musiciens évoluent sans contrat formel, sans rémunération stable, sans protection sociale et dans une dépendance totale vis‑à‑vis du leader de leur groupe.
Dans un tel contexte, chaque voyage à l’étranger apparaît comme une échappatoire à une réalité professionnelle instable et parfois humiliante.

6. À cette précarité s’ajoute l’illusion persistante de l’Europe perçue comme un «Eldorado» artistique, social et économique.
Pour beaucoup, l’Occident représente un espace de liberté, de sécurité et d’opportunités, même si cette vision est souvent idéalisée.
La simple perspective d’une vie meilleure suffit à nourrir le désir de ne pas revenir, surtout lorsque les conditions de travail au pays semblent sans issue.

7. Les tensions internes au sein des orchestres jouent également un rôle majeur.
Outre les rivalités classiques, un phénomène plus insidieux fragilise les artistes : l’influence toxique de certains proches des leaders, qui, par jalousie ou intérêt personnel, inventent des histoires, sèment la discorde et montent certains Musiciens contre leur chef.
Ces manipulations entraînent l’isolement injustifié de certains Artistes, la destruction volontaire de carrières prometteuses et l’instauration d’un climat de travail marqué par la peur et la suspicion.

8. À cela s’ajoute la pression sociale et familiale.
Dans l’imaginaire collectif congolais et plus largement africain, la réussite est souvent associée à l’émigration.
Certains Musiciens sont explicitement encouragés, voire poussés, par leur entourage à ne pas revenir au pays.
Cette pression psychologique renforce l’idée que la fuite constitue une voie légitime vers une vie meilleure.

9. L’absence d’un cadre juridique solide aggrave encore la situation.
Le secteur culturel congolais souffre d’un manque criant de législation protectrice, de l’inexistence d’une sécurité sociale dédiée aux Artistes, de l’absence de politiques culturelles ambitieuses et de normes professionnelles claires.
Dans un tel vide institutionnel, les musiciens se retrouvent livrés à eux‑mêmes, sans filet de sécurité.

10. Les conséquences de ces départs sont lourdes : perte de crédibilité pour les leaders, méfiance accrue des promoteurs européens, difficultés d’obtention de visas, désorganisation artistique et effondrement des carrières individuelles.

Pour rompre ce cycle, des réformes profondes s’imposent : contrats clairs, rémunérations régulières, protection juridique, diplomatie culturelle renforcée et lutte contre les manipulations internes.

La disparition de Charly Solo, de Limousine Ferrari, des dix-sept Musiciens de Villanova ou encore la scission de Londres ne relève pas du hasard : elle révèle un système culturel fragilisé qui doit impérativement être réformé pour que la musique congolaise retrouve la discipline, la dignité et le prestige qui ont fait d’elle l’une des plus grandes richesses culturelles du continent africain.

BABA L.W.L

HADITHI YA CINDY LE CŒUR MAMACYLA VOIX QUI DEVINT REINE :HISTOIRE DE CINDY LE CŒUR01) Alizaliwa tarehe 11 Novemba 1983, ...
09/04/2026

HADITHI YA CINDY LE CŒUR MAMACY
LA VOIX QUI DEVINT REINE :
HISTOIRE DE CINDY LE CŒUR

01) Alizaliwa tarehe 11 Novemba 1983, Candy Nkunku anafahamika na kuheshimiwa katika jukwaa la muziki wa Congo na ulimwengu mzima kwa jina la Cindy Le Cœur Mamacy,ni miongoni mwa Wasanii wachache ambao wito wao wa kisanaa unaonekana kuandikwa moja kwa moja katika misingi ya utoto wao.

02) Akiwa mtoto wa nne wa marehemu Mzee Nkunku Seba na Mama Antoinette Nzumba, alilelewa katika mazingira yaliyosheheni upendo, utulivu na kuthamini Sanaa.
Tokea bado akiwa mdogo, sauti yake safi na ilio nyororo ilijaza nyumba yao, akiimba kwa ustadi wa kushangaza nyimbo za wakongwe k**a Céline Dion na Whitney Houston.
Wazazi wake, wakiwa na fahari isiyofichika, walitambua mapema kuwa walibarikiwa na mtoto mwenye kipaji cha kipekee, kana kwamba hatima yake ilikuwa tayari imechorwa.

03) Mwaka 2000, akiongozwa na azma ya ndani isiyotetereka, alijiunga na Chuo cha Taifa cha Sanaa (I.N.A.S.), ambako nidhamu yake, umakini wake na kipawa chake cha asili vilimfanya atambulike kwa haraka.
Mwaka 2001, chuo kilianzisha Group la muziki (WASSA), na Cindy akawa mmoja wa waimbaji Kinara.

04) Mwaka uliofuata, 2002, alichaguliwa kuiwakilisha vijana wa Congo katika kongamano kubwa la Afrika mjini Brussels, ambako aliimba wimbo wa kuhamasisha jamii kuwalinda watoto wa mitaani akikumbushia wajibu wa maadili ambayo familia zinapaswa kuubeba.

05) Baada ya kuondoka WASSA, alishirikiana na mhubiri Jean René Balekita, na baadae na Muinjilisti Kool Matope ambae walifaanikiwa kutoa wimbo “Yesu Nalingi Yo” Yesu Nakupenda sana, uliopanua upeo wa safari yake ya Kisanaa.

06) Mwaka 2007, alijiunga na Group mashuhuri Quartier Latin International chini ya uongozi wa gwiji Koffi Olomide.
Ndani ya Studio Ndiaye, wakati wa kurekodi wimbo “Lili Kaniki”, Koffi aligundua upekee wa sauti yake, uwezo wa kipekee wa kuunganisha nguvu, ustadi na hisia.
Hapo ndipo ushirikiano wao wa muda mrefu, wenye tija na heshima ya pande zote, ulipozaliwa.

07) Mwaka 2008, umaarufu wake uliongezeka zaidi kupitia Album “Bord Ezanga Kombo”, hasa katika wimbo “IKEA”, ambapo sauti yake iling’aa kwa uzuri wa kimalkia.

08) Mwaka 2009, alipewa tuzo la Mwimbaji Bora wa K**e nchini DRC, kisha akang’ara katika Show “Cindy chante Koffi” lililofanyika kwenye Ukumbi wa Grand Hôtel de Kinshasa, kabla ya kutikisa jukwaa la hadithi la Zénith Jijini Paris.

09) Mwaka 2013, alitoa Solo Album yake ya kwanza “Molounge”, yenye nyimbo sita zilizoandikwa na Koffi Olomide.

10) Mwaka 2018, tetesi za kuondoka kwake Quartier Latin zilizagaa, lakini hazikuwa na msingi wowote, ushirikiano wao uliendelea bila kuyumba.

11) Mwaka 2019, alitoa wimbo “Égérie”, uliothibitisha nafasi yake k**a Msanii wa uhakika asiyeweza kupuuzwa.

12) Misiba Iliyoigusa Nafsi Yake
Safari ya Cindy, licha ya mafanikio yake makubwa, haikukosa maumivu.
Alimpoteza Baba yake Mzazi, Mzee Nkunku Seba, tarehe 25 Julai 2022, Mwaka mmoja baadae, tarehe 28 Julai 2023, akampoteza Mama yake mpendwa, Mama Antoinette Nzumba.
Vifo hivi viwili vilivyotokea kwa karibu vilimpa maumivu makubwa, lakini pia viliongeza kina cha hisia katika Sanaa yake.

13) Ufafanuzi Kuhusu Ujauzito na Uzazi Wake
Kinyume na uvumi uliosambaa kwa miaka mingi, Cindy Le Cœur hana mtoto.
Amefafanua kwa uwazi kwamba mtoto aliyeonekana katika baadhi ya picha si mwanawe wa kumzaa, bali ni mpwa wake, ambaye alimlea tokea akiwa mchanga.
Kwa maneno yake mwenyewe, alisema:

“Si mwanangu wa kumzaa. Ni mmoja wa wapwa zangu niliyemlea akiwa mdogo sana.”

Kauli hii ilifuta kabisa uvumi uliokuwa umeenea kuhusu uzazi wake.

14) Ndoa na Koffi Olomide
Baada ya miaka mingi ya kufanya kazi pamoja, ya kuheshimiana kwa kina na ya kujenga uhusiano wa karibu uliozidi mipaka ya muziki, Cindy Le Cœur na Koffi Olomide walifunga ndoa rasmi tarehe 28 Februari 2026, Jijini Kinshasa, mbele ya afisa wa Serekali kwenye Manispaa ya Gombe.
Ndoa hii, iliyosubiriwa kwa hamu na mashabiki wao, imekuwa k**a muhuri wa hadithi yao hadithi ya muziki, ya heshima, ya safari ya pamoja, na sasa, ya maisha ya ndoa.

HISTOIRE DE CINDY LE CŒUR MAMACY

01) Née le 11 novembre 1983, Candy Nkunku connue et célébrée sur les scènes musicales du Congo et du monde sous le nom de Cindy Le Cœur Mamacy appartient à cette catégorie rare d’artistes dont la vocation semble inscrite dès les premiers instants de l’enfance. Son destin artistique apparaît comme une évidence, presque comme une écriture intérieure qui ne demandait qu’à éclore.

02) Quatrième enfant du regretté Papa Nkunku Seba et de Maman Antoinette Nzumba, elle grandit dans un environnement empreint d’amour, de sérénité et d’un profond respect pour les arts.
Dès son plus jeune âge, sa voix pure et soyeuse résonne dans la maison familiale, interprétant avec une maîtrise étonnante les grandes divas telles que Céline Dion et Whitney Houston.
Ses parents, fiers et émerveillés, comprennent très tôt qu’ils ont donné naissance à un talent exceptionnel, comme si son destin avait été tracé d’avance.

03) En 2000, guidée par une détermination intérieure inébranlable, elle intègre l’Institut National des Arts (I.N.A.S.), où sa discipline, sa rigueur et son talent naturel lui valent une reconnaissance rapide.
En 2001, l’institution crée le groupe musical WASSA, dont Cindy devient l’une des voix principales.

04) L’année suivante, en 2002, elle est choisie pour représenter la jeunesse congolaise lors d’un grand colloque africain à Bruxelles, où elle interprète un hymne appelant la société à protéger les enfants des rues, rappelant ainsi la responsabilité morale que les familles doivent assumer.

05) Après avoir quitté le groupe WASSA, elle collabore avec le prédicateur Jean René Balekita, puis avec l’évangéliste Kool Matope, avec qui elle enregistre le titre «Yesu Nalingi Yo» (Jésus, je t’aime tant), une œuvre qui élargit considérablement l’horizon de sa carrière artistique.

06) En 2007, elle rejoint le prestigieux Quartier Latin International, sous la direction du maître incontesté Koffi Olomide.
C’est au Studio Ndiaye, lors de l’enregistrement du titre «Lili Kaniki», que Koffi découvre l’exceptionnelle singularité de sa voix : une capacité rare à unir puissance, finesse et émotion.
De cette rencontre naît une collaboration durable, féconde et marquée par un profond respect mutuel.

07) En 2008, sa notoriété s’accroît encore grâce à l’album «Bord Ezanga Kombo», notamment avec le titre «IKEA», où sa voix brille d’un éclat véritablement royal.

08) En 2009, elle reçoit le prix de la Meilleure Chanteuse de la RDC, puis triomphe lors du spectacle «Cindy chante Koffi» au Grand Hôtel de Kinshasa, avant de conquérir la scène mythique du Zénith à Paris.

09) En 2013, elle publie son premier album solo, «Molounge», composé de six titres écrits par Koffi Olomide.

10) En 2018, des rumeurs annoncent son départ du Quartier Latin, mais celles‑ci s’avèrent infondées : leur collaboration se poursuit sans la moindre rupture.

11) En 2019, elle dévoile le titre «Égérie», confirmant sa stature d’artiste incontournable, solide et indiscutable.

12) Les deuils qui ont marqué sa vie
Malgré une carrière éclatante, la vie de Cindy n’a pas été épargnée par la douleur.
Elle perd son père, Papa Nkunku Seba, le 25 juillet 2022, puis, un an plus t**d, le 28 juillet 2023, sa mère bien‑aimée, Maman Antoinette Nzumba.
Ces deux disparitions rapprochées la frappent profondément, mais elles nourrissent également la dimension émotionnelle et spirituelle de son art.

13) Clarification concernant sa maternité
Contrairement aux rumeurs persistantes, Cindy Le Cœur n’a pas d’enfant.
Elle a elle‑même clarifié la situation : l’enfant apparaissant sur certaines photographies n’est pas son fils biologique, mais l’un de ses neveux, qu’elle a élevé dès son plus jeune âge.
Elle l’a déclaré avec calme et transparence :

«Ce n’est pas mon fils biologique.
C’est l’un de mes neveux que j’ai élevé lorsqu’il était encore très jeune».
Cette mise au point a définitivement dissipé les spéculations entourant sa maternité.

14) Le mariage avec Koffi Olomide
Après de longues années de collaboration artistique, de respect profond et d’un lien personnel devenu indéniable, Cindy Le Cœur et Koffi Olomide se sont unis officiellement le 28 février 2026, à Kinshasa, devant l’officier de l’état civil de la commune de la Gombe.
Cette union, attendue avec ferveur par leurs admirateurs, scelle une histoire faite de musique, de loyauté, de chemin parcouru ensemble, et désormais, d’une vie conjugale partagée.

BABA L.W.L

Adresse

Avenue D'ORADOUR SUR GLANE
Bonneuil-sur-Marne
94380

Téléphone

33668312952

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Lubonji Wa Lubonji publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Contacter La Pratique

Envoyer un message à Lubonji Wa Lubonji:

Partager

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram