17/09/2025
Kwa wale wageni kuwakumbusha tu kabla ya kuwa mwalimu na Daktari wa kiroho nilifuzu pia kuwa Daktari au muuguzi ndio maana wengi wananijua k**a Dr.Mwaka haimaanishi ni jina tu la utani bali ni jina lenye hadhi kubwa sana kwangu hivyo leo tugusie maswala ya Afya ya mwili maana kuna mambo yanaendelea huku mitandaoni ukiskiza unaeza rukwa na akili, utasikia mara hoo mimi ni blood group O, siezi dumu kwa mahusiano, mimi ni blood group O nina hasira za kuua mtu😀😀 Sasa hawa blood group O ni nani haswaa mara Uskie “Mimi nina Group O Siugui Magonjwa Ovyo" JE..? Ukiwa na damu kundi O, Magonjwa hayawezi kukugusa...?
Au ni porojo tu za mtaani..?
Maana naona watu huwa mnatamba na Blood Groop O Kwamba hampati UKIMWI..Kirahisi..!☠️
Kundi la Damu O – La Kipekee au la Kawaida..?
Kabla ya kuchambua magonjwa na kinga ya kundi hili, hebu kwanza tulielewe vizuri....
Je, unajua kwamba kundi la damu O ndilo kundi la damu linalopatikana kwa wingi zaidi duniani..?
↳ Inakadiriwa kuwa karibu 45% ya watu duniani wana kundi la damu O
Hili ni kundi la damu linaloweza kutolewa kwa watu wa makundi yote mengine, lakini wenyewe wanaweza kupokea damu kutoka kwa kundi lao pekee...
Linaitwa *"Universal Donor"* kwa sababu wanaweza kumsaidia mtu yeyote anayehitaji damu...
K**a wewe ni kundi O, basi damu yako inaweza kuokoa maisha ya mtu yeyote bila kujali kundi lake.
*Lakini sasa swali kuu ni hili....*
Je, hii inamaanisha kinga yao ya mwili ni ya kipekee pia...?
Wenye Kundi la Damu O Hawashikwi na Magonjwa?
→Ebu tuweke rekodi sawa..!
Ukweli ni kwamba kuwa na kundi la damu O kunaweza kutoa faida fulani za kiafya, lakini si kwamba hauwezi kuugua !
Magonjwa Yaliyo na Hatari Ndogo kwa Wenye Damu O...
✔ Magonjwa ya Moyo...
Utafiti umeonyesha kuwa watu wenye kundi la damu O wana hatari ndogo ya kupatwa na magonjwa ya moyo k**a shinikizo la damu na mshtuko wa moyo (heart attack) ukilinganisha na makundi mengine ya damu.
Sababu ni kwamba damu yao ina chembe zinazosaidia kuzuia kuganda kwa damu haraka, hivyo kupunguza hatari ya kuziba kwa mishipa ya damu.
✔ Dengue...
Unasikia watu wakishikwa na homa ya dengue hadi hali zao zinakuwa mbaya sana..?
Wanasayansi wanasema kuwa wenye kundi la damu O wako katika hatari ndogo ya kupata madhara makali ya homa hii ikilinganishwa na makundi mengine..!
✔ Blood Clots (Damu Kuganda Kiholela)
Wenye kundi la damu O wana hatari ndogo ya kupata magonjwa yanayosababishwa na damu kuganda ovyo mwilini (deep vein thrombosis na pulmonary embolism).
Hii ni kwa sababu damu yao ina kiwango kidogo cha baadhi ya protini zinazohusika na mchakato wa kuganda kwa damu.
*Ps;* Kwa hiyo, k**a wewe ni O, unaweza kujivunia kuwa na kinga fulani dhidi ya magonjwa haya...! Lakini subiri… Si kila kitu ni kizuri kwa Kundi O
*Magonjwa Yanayowaathiri Zaidi Wenye Damu O..*
Sasa tusonge upande wa pili wa sarafu.
Watu wenye kundi la damu O si malaika wasioguswa na magonjwa..
Kuna hatari wanazokumbana nazo pia....
→Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)..
Utafiti unaonyesha kuwa watu wenye damu ya kundi O wana uwezekano mkubwa wa kupata vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na bakteria aitwaye Helicobacter pylori.
Bakteria huyu anapopata mazingira mazuri tumboni, husababisha vidonda ambavyo huleta maumivu makali na shida za mmeng’enyo wa chakula.
→ Matatizo ya Kupoteza Damu (Bleeding Disorders)...
Kwa sababu damu ya kundi O haishikani haraka, watu hawa wanaweza kuvuja damu kwa muda mrefu zaidi wakipata jeraha au kufanyiwa upasuaji...
Hii ni hatari hasa kwa wanawake wenye hedhi nzito au kwa watu wanaofanyiwa upasuaji mkubwa.
→ Maambukizi ya Bakteria na Virusi...
Ingawa wanapata kinga dhidi ya baadhi ya magonjwa, bado wako kwenye hatari ya kushambuliwa na maambukizi fulani ya bakteria na virusi.
Kwa hiyo, wale wanaosema “Mimi nina group O, magonjwa hayanipati” – Ujaribu tena kutamba na kauli hiyo!
*Lishe ya Wenye Kundi la Damu O Ukweli au Uzushi...?*
↳Kuna dhana kwamba kundi la damu linaweza kuathiri vyakula unavyopaswa kula.
Unakumbuka ile “BloodType Diet” inayosema wenye damu O wanapaswa kula nyama nyingi na kupunguza wanga?
*Ipo hivi...*
Hadi sasa, hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuthibitisha kuwa chakula kinapaswa kutegemea kundi la damu.
Lakini kwa ujumla...
✔ Wenye kundi la damu O wanahimizwa kula lishe yenye protini nyingi k**a nyama, samaki, mayai, na mboga za majani kwa wingi....
❌ Wanga nyingi (mkate, wali, pasta) zinaweza kusababisha kuongeza uzito kwa haraka, hivyo ni vyema kupunguza kiasi.
Hii haimaanishi kuwa watu wa kundi O wasile vyakula vya wanga kabisa – inategemea mtu na mwili wake!
*Je, Huwezi Kuugua Ukiwa na Damu O?*
❌ HAPANA! Kuwa na kundi la damu O hakumaanishi huwezi kupata magonjwa!
Ni kweli kwamba una faida fulani za kiafya, lakini pia kuna magonjwa yanayoweza kuwa hatari zaidi kwako.
→Hakuna kundi la damu lisiloweza kuugua! Kinachoamua Kuwa na Afya bora ni..
✔ Kula chakula bora
✔ Kufanya mazoezi mara kwa mara
✔ Kupata usingizi wa kutosha
✔ Kupunguza msongo wa mawazo
✔ Kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara
Kwa hiyo, kwa wale wanaojiona kuwa “immune” kwa sababu wana kundi O, wajipange upya!...🫵🏾