26/11/2021
SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA UJAUZITO 🤰
- #0766786266 / #0655203943.
——————————————————————
Ili mwanamke apate mimba, sehemu zote za mwili wake zinazohusika na uzazi zinatakiwa zifanye kazi inavyotakiwa na katika hatua zote. Hatua katika utengenezaji wa mimba ni k**a zifuatazo:
✍️1. Moja kati ya ovari mbili za mwanamke kuachia yai lililokomaa
✍️2. Yai hii kusafirishwa na mrija wa uzazi (fallopian tube)
✍️3. Mbegu za mwanamme kusafiri hadi kwenye cervix, kupitia tumbo la uzazi (uterus) hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai na kulipevusha.
✍️4. Yai lililopevushwa kusafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi (uterus).
✍️5. Yai kunata kwenye ukuta wa uterus na kukua.
Ugumba kwa mwanamke unaweza kutokana na dosari katika hatua yoyote katika hizo tulizozitaja na mara niyingine kutokana na dosari katika hatua zaidi ya moja.
Pamoja na kuwa kuna sababu nyingi za mwanamke kutopata mimba, lakini sababu kuu tatu ndizo zinazohusika zaidi k**a tutakavyozielezea hapa chini.
🤱 tatizo la kukosa mtoto
✍️Kushindwa Kuzalisha Mayai (Anovulation)
Hili ndilo tatizo ambalo linachangia ugumba kwa wanawake kwa asilimia 30 lakini kwa bahati nzuri asilimia 70 ya wanawake wenye tatizo hili hupata tiba na kufanikiwa kupata watoto. Mwanamke mwenye tatizo hili hutoa mayai mara chache au hatoi mayai kabisa. Chanzo cha tatizo huwa ni moja ya yafuatayo:
✍️1. Matatizo Ya Homoni
Matatizo ya homoni ndiyo yenye mchango mkubwa zaidi kwenye kumfanya mwanamke ashindwe kuzalisha mayai. Uzalishwaji wa mayai hutegemea mchanganyiko wa homoni utakaofanya kazi kwa kuhusiana bila kuvurugwa katika utendaji wake wa kazi.
Kuna matatizo ya aina tatu yanayoweza kuvuruga mpangilio huo.
•Kuzalisha Mayai Yasiyokomaa:
Matatizo Ya Hypothalamus: Hypothalamus ni sehemu ya ubongo inayohusika na kutoa ishara kwa tezi ya pituitary (pituitary gland) ambayo nayo huamsha homoni za ovari zinazoruhusu yai kukomaa. Hypothalamus isipofanya kazi yake, mayai hushindwa kufika ukomavu. Asilimia 20 ya dosari za ukomavu wa mayai husababishwa na matatizo ya hypothalamus.
Matatizo Ya Pituitary Gland: Tumeona hapo juu kuwa tezi ya pituitary inahusika katika kukomaza mayai. Endapo pituitary itatoa homoni kwa kiwango kidogo au kikubwa kupita kiasi, ovari zitashindwa kuzalisha na kutoa mayai ipaswavyo. Hali hii hutokea pale tezi hii inapoharibiwa kwa ajali, kunapotokea uvimbe ndani yake au kunapokosekana ulingano wa kikemikali ndani ya tezi hiyo.
✍️2. Makovu Kwenye Ovari
Uharibifu kwenye ovari unaweza kusababisha ovari hizi kushindwa kuzalisha mayai. Operesheni za mara kwa mara hujenga makovu kwenye ovari hizo na kuzifanya zishindwe kuzalisha mayai. Maambukizi ya magonjwa huweza pia kusababisha ovari kushindwa kuzalisha na kutoa mayai.
✍️3. Kukoma Hedhi Mapema
Kukoma hedhi mapema ni tatizo ambalo halijaeleweka vizuri kisayansi. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao za kawaida kwenye umri usiotegemewa. Dhana moja ni kuwa hifadhi yao ya mayai imekwisha au nyingine ni kuwa inatokana na wanawake hawa kuwa wenye historia ya kuwa wanariadha waliokuwa na miili yenye uzito mdogo na waliofanya mazoezi ya nguvu kwa muda mrefu. Kuna uwezekano kuwa kukoma hedhi mapema ni suala la urithi.
✍️4. Matatizo Ya Follicle
Kuna tatizo lisilo na maelezo ya kisayansi “unruptured follicle syndrome” ambapo mwanamke hutengeneza mfuko wa kawaida wa yai wenye yai ndani yake kila mwezi lakini mfuko huo hugoma kupasuka na kuachia yai. Hivyo kwamba, yai hubaki ndani ya ovari na utolewaji wa yai nje ya ovari
Magonjwa katika mirija ya uzazi huathiri asilimia 25 ya wanafamilia ambapo tatizo laweza kuwa dogo la kunata kwa yai au kubwa la mirija kuzibwa kabisa. Tiba kwa matatizo ya mirija ya uzazi mara nyingi ni upasuaji. Matatizo yanayopelekea kuziba kwa mirija ya uzazi ni k**a yafuatayo:
✍️1. Maambukizi Ya Wadudu
Maambukizi ya virusi na bacteria yanayoenezwa kwa ngono husababisha makovu na uharibifu, kwa mfano, maambukizi ya Hydrosalpinx yanayosababisha mirija ya uzazi kuziba pande zote na kujaa maji .
2. Upasuaji
Hii ni sababu kubwa ya magonjwa na uharibifu wa mirija ya uzazi. Upasuaji wa kwenye maeneo ya kinena na tumbo huweza kusababisha uharibifu utakaozuia upitaji wa yai.
3. Mimba Ndani Ya Mirija Ya Uzazi (Ectopic Pregnancy)
Mimba zinazotunga ndani ya mirija ya kizazi huweza kuleta uharibifu kwenye mirija hiyo hata k**a tahadhali ya juu itachukuliwa kuziondoa.
4. Matatizo Ya Kuzaliwa Nayo
Mara chache huweza kutokea kuwa mwanamke akazaliwa akiwa na dosari katika mirija yake ya uzazi.
💊kwa wewe ambaye umeteseka muda mrefu kutafuta mtoto bila mafanikio ni wakati wako sasa kuitwa mama,tumakuletea suluhisho lako wahi sasa
Tupigie simu kwa namba zinazoonekana hapo juu.