21/07/2023
*SOMA KWA MAKINI UTAMBUE UGONJWA HUU.*
↔PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa
mwanamke na mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa k**a gonorrhea na
chlamydia ila kuna aina ya maambukizi mbali na magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha
maambukizi ya PID.
✅JE! MWANAMKE HUAMBUKIZWAJE PID?
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza
kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na:
🌺K**a una ugonjwa wa zinaa na haijatibiwa
🌺 Kufanya ngono zembe isiyo salama
🌺 Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi nje
🌺 K**a umekuwepo na historia ya PID hapo nyuma
🌺 Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
🌺 Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
🌺 Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango
🌺 Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID
🌺 Kuingiza vitu mbalimbali ukeni (Vaginal Dauche)
✅UTAJUAJE UKO NA (PID)?
↔Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID.
Miongoni mwa dalili hizi ni:
🎯Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa
maeneo ya chini ya kitovu
🎯Kupata maumivu ya mgongo
🎯Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri unaoambatana na harufu mbaya.
🎯Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
🎯Kupata maumivu au kutokwa na damu wakati
wa tendo la ndoa
🎯 Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
🎯 Kupata homa
🎯 Kupata damu innje ya siku zako zako za kawaida kupata damu ya hedhi
🎯Wakati fulani kuhisi kichefuchefu k**a
mwanamke mja mzito na kutapika.
✅JE PID INAWEZA KUTIBIWA?
↔Jibu ni ndio k**a itagunduliwa mapema inaweza kutibiwa na ikaisha, ila ieleweke k**a tayari ilikuwa imeharibu njia za uzazi uharibifu ule haiwezi kurekebishwa. Kila mara ukichelewesha kutibu PID ndivyo itaharibu mfumo wako wote wa uzazi.
✅MATIBABU YA UGONJWA HUU.
↔Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa
ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa huu, lakin ikiwa maambukiz ni ya muda mrefu dawa hizi haziwez kukutibu ukapona kabisa.
✅MADHARA YAKUTOTIBU P.I.D
♨ Maumivu ya mfuko wa uzazi wakudumu
♨ Utapata ugumu wa kushika mimba
♨ Ectopic pregnancy (mtoto kuwa nje ya mfuko wa uzazi)
♨ Kuziba kwa njia ya uzazi
♨ Viuvimbe katika kizazi
♨ Mabadiliko ya homoni
♨ Mimba kuharibika.
✅JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI.
↔Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika
mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na:
💥Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni
kuwacha ngono zembe na kufanya ngono salama
💥 Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa au anatembea na wanawake wengine
💥 Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya
maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI) hususan ugonjwa wa chlamydia ufanyie vipimo kila mwaka mara 1
💥Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua,
mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.
🔵Kuna program ambayo tumekuandalia ya virutubisho lishe kwa wote ambao wanateseka na P.I.D na magonjwa mbalimbali. Endapo utakuwa unahitaji ushauri, tiba ya haraka basi wasiliana nami.255783326598