UZAZI salama 2022

UZAZI salama  2022 utapata ufumbuzi WA changamoto zote Za Uzazi Kwa binadamu

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Love Mtei, Furaha Yotham, Ruth Shango, Joymary Daniel, Me...
04/12/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Love Mtei, Furaha Yotham, Ruth Shango, Joymary Daniel, Merilian Paschal

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Stella Michael Lutome, Faudhia Said, Pili Ally, Belinda M...
24/11/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Stella Michael Lutome, Faudhia Said, Pili Ally, Belinda Mfoi, Stella Samon, Agatha Fwila, Sally Ally, Fairness Mashimbi

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Aalyan Mushi, Freda Petro, Leontia Peter, Bertha Jotham, ...
13/11/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Aalyan Mushi, Freda Petro, Leontia Peter, Bertha Jotham, Elizabeth Jeremiah, Mariam Mamuor

FAHAMU UTE WA UZAZI (FERTILITY MUCUS)✍️ Kwa kawaida mwanamke yeyote alie kamili yaani (asie na tatizo lolote kwenye mfum...
10/11/2024

FAHAMU UTE WA UZAZI (FERTILITY MUCUS)

✍️ Kwa kawaida mwanamke yeyote alie kamili yaani (asie na tatizo lolote kwenye mfumo wa uzazi) hupevusha mayai. Dalili ya upevushaji wa mayai kwa mwanamke ni kupata ute wa uzazi.

♥️ Ute wa uzazi ndio unafanya kazi kubwa yakusafirisha mbegu za kiume (s***m) kutoka ukeni (vaginal) mpaka kwenye mirija ya uzazi (fallopian tube) ambapo itakutana na yai lililopevuka (o**m) kutoka kwenye o***y ndipo mimba itatungwa.

🫄Yai lililorutubishwa litasafiri kwenye mirija ya uzazi na kufika kwenye mji wa mimba (uterus) ambapo litajishikiza kwenye kuta za uterus na mimba itaendelea kukua hatua kwa hatua.

🧠 Ifahamike kwamba matatizo mengi ya uzazi yanayosababisha mwanamke asishike mimba husababishwa na kasoro katika uzalishwaji mbegu za kiume (s***m) na matatizo katika ute wa uzazi kwa mwanamke.

✍️ Mwanamke anapoukosa ute huu,ansababisha zoezi la mbegu za kiume (s***m) kusafiri mpaka kulifikia yai lililopevuka hata k**a mbegu za kiume ziko sawa na hazina kasoro yoyote! K**a hakuna ute wa uzazi zitafia njiani.

🧠 Tambua kuna tofauti kati ute unaoupata wakati wa tendo la ndoa na ute wa uzazi. Ute anaopata mwanamke wakati wa tendo huu unaweza kuupata wakati wowote ukiandaliwa kwaajili yakukutana na mwenza wako au ukiwa na hisia zakukutana na mwenza wako. Lakini ute wa uzazi unaoupata pale tu yai linapopevuka (o**m).

AINA ZA UTE WA UZAZI
📌 Kuna aina nne (4) za ute wa uzazi ambazo mwanamke anaweza akazipata katika mazingira au nyakati tofauti tofauti. Na kati ya hizo ni aina moja tu ndio inakupa uhakika wa kushika mimba kwa 100% Hebu tuzipitie mojamoja ili tuzijue:

1.UTE MKAVU/UNANATA SANA

✍️ Aina ya ute k**a huu hauruhusu mbegu za kiume kusafiri kuingia kwenye mirija ya uzazi kwasababu ni mkavu na mzito hivyo zoezi la kusafiri linakua gumu mwishowe s***m zinafia njiani.
Ute huu hutokea wakati mwanamke hayupo kwenye joto au yai halijapevuka.

2.UTE WA RANGI YA CREAM(KRIMU)

✍️ Aina hii ya ute hutokea wakati mwanamke anakaribia kuingia kwenye kipindi cha joto na yai linakaribia kupevuka lakini hataweza kushika mimba kwasababu mpaka yai lipevuke s***m zitakua zimekufa.

3.UTE MWEPESI/WENYE UNYEVUNYEVU

✍️ Huu unaweza kusafirisha mbegu za kiume mpaka kwenye mirija ya uzazi na hata k**a bado siku 2/3 yai lipevuke ukikutana na mwenza wako bado kuna uwezekano ukashika mimba kwasababu yai likipevuka litakuta na s***m. Kumbuka s***m zinaweza kukaa kwenye mirija masaa 72 yaani siku tatu zikisubiri yai lije. Lakini ute huu unakupa uwezekano wakushika mimba 50/50

4.UTE MWE MWEUPE K**A UTE WA YAI

👍 Huu ndio ute ambao kwa zaidi 95% unatoa uhakika wa mwanamke kushika mimba,maana ni mzuri kwa kusafirisha s***m kwa uhakika.
Hapa mwanamke anakua tayari yuko kwenye kipindi cha joto na yai limepevuka hivyo uwezekano wa kushika mimba ni mkubwa labda kuwe na vizuizi vingine.

🤔NINI SABABU ZA KUKOSA UTE?

📌 Zipo sababu mbalimbali zinazohusiana na kukosa ute wa uzazi. Lakini karibu zote zinaangukia kwenye mabadiliko ya hali yakujiendesha kwenye mfumo wa uzazi.

Mifumo ya mwili wa binadamu imeumbwa kufanya kazi na kujiendesha automatic hivyo inapotokea kufanyiwa mabadiliko yoyote kutoka nje hauathiri utendaji wa mfumo husika.

Tuangalie sababu zinazopelekea kukosa ute wa uzazi;

1.UZAZI WA MANGO

Hii inaweza ikawa ni moja kati sababu kubwa yakukosa ute wa uzazi. Kazi ya njia yoyote ya uzazi wa mpango ni kuvuruga mpangilo wa homon ili usishike mimba.

Ukijaribu kufuatilia asilimia kubwa ya wanawake waliowahi au wanatutumia njia za uzazi wa mpango mpangilio wa hedhi umevurugika,hedhi haieleweke inaanza lini na inaisha lini. Hii inaathiri hata homoni ya estrogen ambayo inahusika sana kwenye uzalishaji wa ute wa uzazi.

2.MAAMBUKIZI KWENYE VIA VYA UZAZI

Mwanamke anapopata maambukizi ya magonjwa kwenye via vya uzazi na akachelewa kupata matibabu au akapata matibabu yasyo sahihi,yanaweza kupelekea kukosa ute wa uzazi.
Magonjwa k**a PID UTI gono,kaswende na magonjwa mengine ya zinaa yanachangia mabadiliko makubwa katika mfumo wa uzazi hivyo kupelekea kukosa ute wa uzazi.

3.KUSAFISHA UKE KUSIKO SAHIHI(VAGINAL DOUNCHIN)

Hapa naomba tuelewane vizuri! Ndani ya uke kuna kemikali zinazalishwa kwaajili ya uke kujisafisha! Ndio maana kuna wakati unatoka ute mweupe k**a maziwa na hauna harufu yoyote,hiyo ni uke unajisafisha ndani wenyewe.

Sisemi kwamba ndio tusijisafuahe!
Kuna katabia mnajisafisha mnaingiza vitu k**a sabuni, napkins zenye kemikali ukeni. Hizi zikikutana na kemikali zilizopo ukeni inaathiri homoni hasa estrogen baade unapata shida za kukosa ute ute ukeni.

📌 Zipo sababu zingine zinazoweza kuchangia kukosa ute wa uzazi k**a;
*Matumizi ya dawa za kupevusha mayai
*Matibabu ya magonjwa ya kawaida
*Uzito mdogo kupita kiasi

Natumaini umejifunza kitu hapa!
K**a una swali au unahitaji ushauri unaweza kunipata kwa Whatsapp 0767 904 560 au nipigie 0677 904 560.

Hello watu wa nguvu! Natumaini tuko vizuri kabisa. Napenda kuwapa habari njema kabisa kua kesho tutakua na darasa zuri k...
09/11/2024

Hello watu wa nguvu! Natumaini tuko vizuri kabisa. Napenda kuwapa habari njema kabisa kua kesho tutakua na darasa zuri kabisa kuhusu UTE WA UZAZI!

Tutajifunza mengi kuhusu mada hii. Jitahidi kupitia somo hili,yawezekana unahangaika kutafuta mimba lakini vitu unatakowa kushughulikia then mambo yaende sawa.

Usisahau kualika wengine kufollow page hii UZAZI salama 2022 ili nao wapate kitu kitakacho wasaidia mahali fulani!!!

Nawatakia wakati mwema!
USIPANGE KUKOSA!!!!

28/10/2024

Hellow familia ya UZAZI salama 2022!!

Natumaini tuko poa kabisa na bado Mungu anaendelea kututunza sana!

Tumepotezana muda mrefu kidogo hatupata muda wakujiogezea maarifa na ufahamu kidogo juu ya afya ya uzazi!

Nimerudi tena na sasa tutakua na madarsa ya back to back kuhusu afya ya uzazi na tutajifunza mengi!

Mungu akipenda wiki hii tutaanza kupost na kushare na Wana familia wa page hii ili tuendelee kujifunza!

Mwisho nikuaombe kukaribisha rafiki,ndugu au jamaa kufollow na kulike page hii ili tuongeze Wana familia!!!!!

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Frida Mario, Ney Cris, Tabia Mbwili, Neema Juma
23/10/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Frida Mario, Ney Cris, Tabia Mbwili, Neema Juma

*USIHANGAIKE  KUTAFUTA  MIMBA K**A MZUNGUKO WAKO WA HEDHI HAUPO SAWA * SOMA MAKALA HII FUPI                        👇👇👇👇👇...
15/07/2023

*USIHANGAIKE KUTAFUTA MIMBA K**A MZUNGUKO WAKO WA HEDHI HAUPO SAWA *

SOMA MAKALA HII FUPI 👇👇👇👇👇👇👇

Mzunguko wa kawaida kwa mwanamke huchukua siku 28 ukianzia kuhesabau siku ya kwanza kupata hedhi katika mwezi husika mpaka siku ya kwanza kupata hedhi kwa mwezi unaofuata, lakini mizunguko inatofautiana kwa kila mwanamke. Pale ambapo mzunguko wako wa hedhi unachukua zaidi ya siku 35 hapo tunasema hedhi imevurugika.

``````NINI KISABABISHI CHA HEDHI KUVURUGIKA````

❤️Mchango wa homoni kuvurugika:

Homoni au vichocheo vikuu zinazoratibu mpangilio wa hedhi yako ni estrogen na progesterone, inaweza kuchukua miaka mingi kwa homoni hizi kuwa na uwiano sahihi. Vihatarishi ambavyo vinapelekea kuvurugika kwa homoni na hatimaye hedhi kuvurugika ni pamoja na

⏩Matumizi ya uzazi wa mpango wa kisasa k**a sindano, vidonge na njiti

⏩Uzito mkubwa kupita kiasi, kitambi au Kupungua uzito kupita kiasi

⏩Msongo wa mawazo
Changamoto za kushindwa kula vizuri na hivo kukosa virutibishi muhimu

⏩Mazoezi makali mfano riadha

⏩Kuugua maambukizi kwenye kizazi(PID) kwa muda mrefu: endapo maambukizi haya yasipotibiwa mapema yanaweza kuathiri mirija ya uzazi pamoja na kizazi kwa ujumla na hivo kuvuruga mpangilio wa hedhi.

⏩Uvimbe kwenye mayai(polycstic ovarian syndrome);mfuko wa mayai kwa mwanamake huitwa o***y na mifuko hii huwa miwili kushoto na kulia. Kila mwezi mwanamke hutoa yai moja kwenye kikonyo chake katika upande mmoja ili liweze kurutubishwa, inapotokea mayai kugoma kutoka kwenye mfuko ndipo uanageuka kuwa vimbe zenye maji (cyst) zikiwa nyingi huitwa polycyst. Changmoto hii ndio chanzo kikuu cha mwanamke kuvurugikiwa hedhi.

⏩Saratani kwenye kizazi inaweza kusababisha mwanamke kupata hedhi nzito sana ama hedhi katikati ya mzunguko wake

⏩Matatizo ya tezi ya shingoni (thyroid gland), tezi hii ndio inayoratibu utolewaji wa homoni za estrogen na progesterone, tezi ikipata hitilafu inapelekea kuvurugika kwa homoni na hivo hedhi pia kuvurugika.
Kuvimba kwa kiazi(endometriosis): hali hii hutokea pale seli za ndani ya ya mfuko wa mimba zinapota na kutoka nje ya mfuko wa mimba, hali hii hisababisha maumivu makali wakati wa hedhi lakini pia yaweza kusababisha mabaki ya hedhi kwenye kizazi.

🥦CHANGAMOTO hii imefanya watu wengi wanahangaika kupata mimba, na k**a hutaweka mfumo wako wa hedhi sawa, basi huwezi pata mimba kamwe...

🌎Sasa Nini cha kufanya ili mzunguko wako u kae sawa.??

🏃‍♀️Wahi mapema kwenye CLINIC ZETU zilizopo mikoa mbalimbali Tanzania

🩺Ushauri wa kitaalamu

💊Matibabu ya uhakika ya tatizo lako.

📲KWA MAWASILIANO
📞PIGA 0626504560Message Uzazi Salama 2022

Au bonyeza link hapo chini👇 kuwasiliana na daktari wa.me/message/TCDVG6L62YHXJ1

Wanawake tibuni  PID,fangasi na magonjwa mengine ya ngono kabla hujapata madhara ya uvimbe kwenye kizazi!  Kuna hatari k...
02/11/2022

Wanawake tibuni PID,fangasi na magonjwa mengine ya ngono kabla hujapata madhara ya uvimbe kwenye kizazi! Kuna hatari kubwa kutoa mimba na husafishi kizazi, uwezekano wa kupata uvimbe kwenye kizazi ni mkubwa. Matumizi ya dawa za kukata hedhi huchangia pia kwa kiasi kikubwa uvimbe kwenye kizazi maana unapoizuia period damu hubaki kwenye kizazi na kutengeneza tissues ambazo baadae zinakua uvimbe mdogomdogo na kadri siku zinaenda, huwa uvimbe mkubwa! JALI AFYA YA UZAZI K**A UNATAMANI SIKU MOJA KUNYONYESHA!

Unafahamu ugonjwa wa uvimbe kwenye kizazi au FIBROIDS na madhara yake?  Ogopa Sana mgonjwa yasyoonekana kwa macho maana ...
25/07/2022

Unafahamu ugonjwa wa uvimbe kwenye kizazi au FIBROIDS na madhara yake? Ogopa Sana mgonjwa yasyoonekana kwa macho maana hutafuna taratibu ndani kwa ndani,inapofikia hatua yakuonekana kwa nje unakua umeshaathiri ndani kwa kiwango kikubwa Sana! Pichani hapo chini ni hatua tofautitofauti za uvimbe kwenye kizazi! Unaanza kakiwa kadogo Sana lakini kadri siku zinaenda nao unaongezeka! Madhara yakuchelewa kutibu ni kufanyiwa upasuaji,wakati mwingine unaweza ukaondolewa kizazi kabisa na usizae tena! Pica ya pili ni uvimbe pamoja na kizazi vimetolewa mamaake mtu huyu hawezi tena kuzaa! KARIBU KWA MSAADA ZAIDI!

Address

Arusha

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 16:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UZAZI salama 2022 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to UZAZI salama 2022:

Share