21/06/2023
Hello everyone, kila siku ni mpya. Alishaifanya Mungu, maisha yetu yanategemea nini umekusudia ndani ya moyo wako. Ikiwa wewe ni mwanandoa unapaswa kujua au kukumbuka kwamba changamoto lazima zitakuwepo katika mahusiano. Kwahiyo ni jinsi gani umejiweka kukabiliana na hizo changamoto zitakapo tokea. Na tunapaswa kukumbuka kila mtu anamapungufu yake, namaanisha Mumeo anamapungufu yake na mkeo anamapungufu yake pia. Sasa wewe lazima uwe tayari kukabiliana na hayo yatakapo tokea. Na sio kuachana na mwenzi wako, suluisha na muendele mbele. Usijidanganye kila mwanaume unaemuona anamapungufu yake, na wewe kijana au baba usijidanganye kuwa wapo wasio sumbua, hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe kweli, sasa huyo ulie nae ndio utamuweza, ukipewa mwingine kaka utaona dunia ndogo. Wewe ng'ang'ana na huyo wako unamuweza. Napia agizo la Mungu wetu ni mume mmoja na mke mmoja mpaka kifo. Usiwaze kumuacha mumeo, usiwaze kumuacha mkeo. Nawapenda wote karibuni