25/04/2026
Kaa Kijanja Organization inaendelea kuhamasisha uwajibikaji kwa vijana wasanii na wabunifu kutumia sanaa, ubunifu na teknolojia k**a nyenzo za kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mnamo 2025, kupitia mradi wa REST II (Reproductive Equity Strategy in Tanzania), zaidi ya vijana wasanii 40 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania walijengewa uwezo wa kutumia sanaa na ubunifu kuelimisha na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa Afya bora kwa Vijana, Stadi za Maisha na kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Kutana na Saraphina Wilson miongoni mwa vinara wa REST II, anaeleza jinsi maarifa aliyopata yatakavyoboresha sanaa yake na kuchochea mabadiliko chanya katika jamii.