13/11/2022
Tunaomba radhi kwa unaetazama video hii. Si rafiki sana lakini wakati mwingine inabidi uhalisia ujulikane. Hili jipu ambalo limeshamiri chini ya mdomo, chanzo chake ni jino lililotoboka kinywani likaachwa (neglected). Sababu kuu mbili za watu wengi kuacha meno yaliyotoboka kinywani ni;
1. Elimu mtaani.com, hii ni ile watu wasio na elimu yoyote kuhusu magonjwa ya kinywa kukupa taarifa potoshi. Unaambiwa uking'oa jino lililotoba mdudu anarukia meno mengine, usipong'oa utabaki salama.
Ukweli ni kwamba unavoacha jino lililotoboka bila kuliziba linaambukiza meno mengine kwa kasi zaidi na kukufanya mhanga wa magonjwa ya meno siku za mbele. Kinachofanya meno yatoboke na kuuuma sio mdudu anaeruka k**a panzi, ni matokeo yako ya muda mrefu ya kupotezea kufuata ushauri wa wataalamu sahihi wa kinywa.
2. Kutumia dawa bila kujua zinakusaidia vipi. Hapa Kuna makundi mawili, moja ni wale ambao kwa kuwa alishawahi kuumwa akaenda hospitali akaandikiwa dawa, akishakariri hizo dawa tayari anaishia kuwa daktari mtaani sasa, akisikia tu rafiki anaumwa jino ndio anakuwa mjuaji, katumie hii na hii, ingekuwa rahisi hivyo kusingekuwa na vyuo vya kusotea udaktari wa kinywa na meno. Pili kuna wale wanaoamini tiba asili, unaambiwa jino haling'olewi tumia dawa litaacha kuuma, kitaalamu tunasema, jino likishatoboka ndio ugonjwa wenyewe, achana ma maumivuu maana hizo ni "complications" za ugonjwa.
Tumeelezea tu kwa ufupi japo yapo mengi ila hayo ndio yamezoeleka kuleta matatizo kwa wateja wetu wengi.
Ukiacha jino lililotoboka bila huduma yoyote ya kitaalamu kuna mambo mengi yanaweza kutokea baadae. Mojawapo ni majipu ambayo yanaweza hata kukatisha uhai. Baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa magonjwa sugu ya kinywani yana uhusiano na magonjwa magonjwa mengine ya mwili k**a vile magonjwa ya moyo.
KUWA MAKINI, WAKATI WOTE ZINGATIA USHAURI WA WATAALAMU HUSIKA.