Afya ya uzazi

Afya ya uzazi Afya ya uzazi kwa wanawake na wanaume

SOMA KWA MAKINI UTAMBUE UGONJWA HUU.  UGONJWA WA PID.  (Pelvic Inflammatory Disease) au Maambukizi Katika Mfumo wa via v...
11/07/2021

SOMA KWA MAKINI UTAMBUE UGONJWA HUU. UGONJWA WA PID. (Pelvic Inflammatory Disease) au Maambukizi Katika Mfumo wa via vya uzazi. (PID) NI NINI? PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mara nyingi husababishwa na magonjwa ya zinaa k**a gonorrhea na chlamydia ila kuna aina ya maambukizi mbali na magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha maambukizi ya PID. JE! MWANAMKE HUAMBUKIZWAJE PID? Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na: - K**a una ugonjwa wa zinaa na haijatibiwa - Kufanya ngono zembe isiyo salama (yani kulala na wanaume tafauti tafauti) - Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi nnje - K**a umekuwepo na historia ya PID hapo nyuma - Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period) - Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage) - Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango - Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID - Kutumia (Vaginal Dauche) UTAJUAJE UKO NA (PID)? Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni: - Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu - Kupata maumivu ya mgongo - Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya. - Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa - Kupata maumivu au kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa - Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi - Kupata homa - Kupata damu innje ya siku zako zako za- kawaida kupata damu ya hedhi - Wakati fulani kuhisi kichefuchefu k**a mwanamke mja mzito na kutapika. VIPIMO VYA PID. Hakuna vipimo maalum kudhibitisha mwanamke ameathirika ila Dactari hujua mwanamke ameathirika baada ya kuchukua historia ya muhusika na kufanya vipimo vingine k**a: - Kuchunguza mkojo ili kufahamu k**a mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba - Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo. - Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na uambukizi huo au k**a kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha. JE PID INAWEZA KUTIBIWA? Jibu ni ndio k**a itagunduliwa mapema inaweza kutibiwa na ikaisha, ila ieleweke k**a tayari ilikuwa imeharibu njia za uzazi uharibifu ule haiwezi kurekebishwa. Kila mara ukichelewesha kutibu PID ndivyo itaharibu mfumo wako wote wa uzazi. MATIBABU YA UGONJWA HUU. Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa huu, lakin ikiwa maambukiz ni ya muda mrefu dawa hizi haziwez kukutibu ukapona kabisa. MADHARA YAKUTO-FWATA MATIBABU - Maumivu ya mfuko wa uzazi wakudumu - Utapata ugumu wa kushika mimba - Ectopic pregnancy (mtoto kuwa innje ya mfuko wa uzazi) - Kuziba kwa njia ya uzazi - Viuvimbe katika kizazi -mabadiliko ya homoni - mimba kuharibika. JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI. Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na: - Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni kuwacha ngono zembe na kufanya ngono salama - Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa au anatembea na wanawake wengine - Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI) hususan ugonjwa wa chlamydia ufanyie vipimo kila mwaka mara 1 - Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema. KWA USHAURI ZAID NA MATIBABU MBADALA PIGA SIMU.
📲0672575505
📲0765525748

Afya ya uzazi kwa wanawake na wanaume

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya ya uzazi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya ya uzazi:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram