20/05/2023
*Mwanamke Kuota*
*ndevu na vinyweleo vingi*
*mwanamke kuota ndevu*
*mwanamke mwenye* *ndevu*
*0753500112*
Kuwa na vinyweleo kadhaa kwenye kidevu chako k**a mwanamke, inaweza kuwa siyo tatizo. Kuna mabadiliko mengi yanaweza kuchangia ikiwemo kuzeeka, homoni na mazingira fulani. Mwanamke kuota ndevu na vinyweleo vingi inaanza kuwa tatizo pale zinapokuwa nyingi sana.
Kitaalamu tatizo la kuwa na vinyweleo vingi maeneo mmbalimbali ya mwili huitwa hirsutism. Ni hali ya mwanamke kuwa na sifa k**a za mwanaume. Nyele zinaota kupita kiasi kwenye maeneo ya kidevu, kifua, tumboni na mgongoni. Hali hii inaweza kumuathiri sana mwanamke kisaikolojia, akawa mpweke na kuhisi hana thamani.
Fahamu tu kwamba kuna njia nyingi za asili na rahisi ambazo waweza kufatilia ili kupunguza ndevu na vinyweleo bila kuathirika. K**a wewe ni mwanamke na upo kwenye umri wa kuza (mika 18 mpaka 35) na una ndevu nyingi sana, kuna haja ya kumwona daktari. Unaweza kuwa na tatizo kubwa la kiafya linalopelekea hali yako.
*Dalili za kwamba una homoni za kiume zilizozidi*
kuota nywele nyeusi usoni, kifuani, mgondoni, kwenye mikono, mapaja ama sehemu zingine ambazo siyo kawaida kwa wanawake.
chunusi nyingi kupita kiasi
kuota kipara
matiti kuwa madongo sana
misuli kukua na kujaa
kisimi kuwa kirefu sana
sauti nzito
Nini kinapelekea mwanamke kuota ndevu?
Kila mtu ana vinyweleo kwenye ngozi yake na ni jambo la kawaida kabisa. Kazi ya vinyweleo hivi ni kurekebisha joto la mwili kwa kuruhusu jasho kutoka ama mwili utunze maji.
*Wakati wa kubalehe, homoni za* kiume(androgens) huongezeka sana na kupelekea vinyweleo hivi kuwa vikubwa mpaka kuwa nywele kamili ambayo ni ndefu na nyeusi. Hii ni kwa wote mwanamke na mwanaume. Wote wana homoni za k**e na za kiume ndani yao, ila tu mwanamke ana homoni kidogo za kiume na mwanaume ana homoni kidogo za k**e.
Homoni hizi huendelea kubadilika kadiri umri wako unavosogea, unavobadilika uzito, kushika mimba na pia unavokaribia kukoma hedhi. Mabadiliko kidogo tu ya homoni za kiume yanaweza kupekelea uote nywele nyingi mwilini ikiwemo kidevuni. Hapa chini ni baadhi ya changamoto zinazopelekea mabadiliko ya homoni na hatimaye uwe na ndevu nyingi.
Polycystic o***y syndrome(PCOS)
Hii ni moja ya sababu kubwa sana ya kwanini una ndevu k**a mwanaume. Kati ya wanawake wanne wenye ndevu basi watatu ni kutokana na PCOS. PCOS inasababisha hedhi kuvurugika na homoni kuvurugika pia na kupelekea uote ndevu nyingi.
PCOS ni tatizo la mifuko ya mayai kushindwa kutoa mayai yaliyopevuka na yanabadilika kuwa vimbe ndogo ndogo nyingi. Pcos linaweza kuwa tatizo la kurithi.
*Cushing’s syndrome hupelekea mwanamke kuota ndevu*
Hii ni hali ya mwili kuzalisha homoni nyingi ya cortisol. Homoni ya cortisol huzalishwa hasa wakati wa hatari ama ukiwa na msongo wa mawazo ili kuandaa mwili kupambana. Inapozalishwa kila mara inakufanya uanze kuwa na sifa za kiume. Baadhi ya vitu vinavyochangia kuongezeka kwa cortisol ni pamoja na matumizi ya dawa kwa muda mrefu hasa prednisone.
Matatizo ya tezi ya thyroid yanachangia mwanamke kuota ndevu
Pale tezi ya shingoni ya thyroid isipofanya kazi vizuri, inapelekea kupanda ama kushuka kwa uzalishaji wa homoni. Kitendo hiki kinaathiri kazi zingine za mwili. k**a una nywele nyingi nenda hospitali kapime homoni ya TSH, T3 na T4 kuona k**a kuna tatizo.
Matumizi ya dawa huchangia mwanamke kuota ndevu
Dawa nyingi tu zinaweza kuvuruga mipangilio ya mwili na kukufaya uote ndevu na nywele nyingi kupita kiasi. Pale utakapoenda hospotali kujieleza tatizo, daktari atakuuliza kuhusu dawa unazotumia ikiwemo tiba asili.
*Vimbe*
Japo inatokea mara chache, lakini vimbe kwenye tezi mfano tezi ya adrenal ama kwenye mifuko ya mayai(ovaries), inachangia uote nywele nyingi kupita kiasi.
Ushauri na njia asili za kurekebisha ndevu na vinyweleo vingi
Naweza kusema wanawake wenye ndevu na vinyweleo vingi na wanahitaji njia asili za kurekebisha tatizo, wana bahati sana. Kwasababu kuna njia nyingi mno za kurekebisha dalili za tatizo. Jaribu kutumia njia hizi za asili na ufatilie mabadiliko kisha utupe mrejesho.
Msaaada upo
*0753500112*