07/07/2025
UJUMBE KWA WAFUGAJI
Wengi huanza ufugaji wakiwa na hamasa, lakini huacha njiani kwa sababu hawakuwa na maarifa, uvumilivu, na mpango wa kujifunza zaidi kila mzunguko.
🧠 Mambo 5 ya Kukumbuka Milele:
Elimu huokoa pesa nyingi kuliko dawa.
Ukijua namna ya kuzuia – hutumii fedha nyingi kutibu.
Faida haiwi bahati – ni matokeo ya nidhamu ya kila siku.
Wafugaji wanaofuatilia lishe, chanjo, kumbukumbu na soko hushinda hata bila mtaji mkubwa.
Kila kuku ana gharama – hata usipomwangalia.
Kutochanja au kutokadiria chakula si kuokoa, ni kupoteza kimya kimya.
Usiige kila mtu – fuata mwelekeo wa maarifa uliyonayo.
Kila mfugaji ana mazingira, mtaji, na soko tofauti. Wewe jifunze, jaribu, rekebisha.
Usikate tamaa baada ya hasara ya kwanza.
Hasara ni ada ya kujifunza. K**a ulishapoteza mara moja, tafuta sababu – usirudie kosa lilelile.
📚 USHAURI WA MWISHO:
✅ Soma vitabu vyetu vya ufugaji mara kwa mara – hata mara moja kwa mwezi
✅ Jiunge na vikundi sahihi – si kila group la WhatsApp lina maarifa
✅ Tumia sehemu ya faida yako kuwekeza katika elimu (kozi, semina, mentorship)
✅ Weka malengo ya mzunguko unaofuata: "Nataka kuku wangu waingie sokoni wakiwa na kg 2.2 wiki ya 7."
✅ Kuwa mvumilivu – Kila changamoto ni darasa.
“Usiwe mfugaji wa bahati nasibu. Kuwa mfugaji wa maarifa.”
“Jifunze kwanza, fuata taratibu, faida itafuata.