23/07/2024
LEO TUJIFUNZE KUHUSU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER)
DR.YUNUSU .
Saratani ya shingo ya kizazi ni ugonjwa ambao huwakumba wanawake ,na maana yake ni kuzalishwa kwa cells ambazo si za kawaida katika shingo ya kizazi (malignant tumor in the cervix).
Wanawake wengi hupata saratani ya shingo ya kizazi kupitia sababu tofauti tofauti,lakini sababu kubwa ni kuwepo kwa maambukizi kwenye via vya uzazi hususani HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV) ni aina ya maambukizi yanayosababishwa na virus na huenea kutoka kwa mtu moja hadi mwingine kupitia ngono. Takriban wanawake 90% Hupatikana na saratani kupitia chanzo hiki.
Jamii nyingine ya wanawake waliopo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ni wale wanao jihusisha na mapenzi ya utotoni kabla ya miaka 18,
Pia wanawake ambao wapo kwenye hatari pia ni wale ambao hutumia njia za uzazi wa mpango kinyume pamoja na wanaofanya mapenzi na zaidi ya mwanaume moja nk.
mwanamke mwenye satarani ya shingo ya kizazi anaweza kuona dalili zifuatazo.
•kuona matone ya damu hata K**a haupo kwenye hedhi
•kutokwa na hedhi muda mrefu zaid
•kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa
•kutokwa uchafu wa brown,pink,ukeni
•maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
•kuona damu wakati wa monopause.
Saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuenea taratibu na inaweza kuchukua mwaka 1 au zaidi ili kuanza kuonesha dalili,
Mwanamke anaweza kuanza kuona dalili kutokana na mabadiliko ya shingo ya kizazi,na wanawake ambao kinga zao za mwili ziko chini wanaweza kuona dalili mapema zaidi.
Na wanawake wanaofanya huduma za tiba za mionzi au hufanyiwa upasuaji hawawezi kubeba tena ujauzito tena.
Wanawake wenye saratani ya shingo ya kizazi wanashauriwa kutumia zaidi vyakula vifuatavyo,asali,cabbage,broccoli,tangawizi,mchai chai,maziwa,apple,cinnamon,nuts,mayai.
Madhara makubwa hutapata wanawake ambayo hupata tiba ambazo Sio sahihi au ambao hawajapata matibabu,K**a vile
•kutokwa na damu ukeni bila kukata
•kukojoa mara kwa mara
•magonjwa ya figo (kidney failure)
•ugumba
•kupoteza maisha.
Tunakushauri ufike kwenye ofisi zetu ili uweze kupata ushauri wa kitabibu na namna ya kutibu changamoto hii.
Dr.yunusu
0766786266.
Arusha.