20/05/2026
Stress inaweza kuathiri uwezo wa kupata mimba kwa njia nyingiβna mara nyingi watu hawajui jinsi inavyoingilia mfumo wa uzazi. Hapa chini kuna maelezo rahisi lakini muhimu:
1. Stress inaharibu homoni za uzazi
Stress husababisha mwili kutoa homoni k**a cortisol.
Homoni hii inapokuwa nyingi:
Inapunguza uzalishaji wa homoni za uzazi (k**a estrogen & progesterone)
Inachanganya mfumo wa ovulation
π Matokeo: Mwanamke anaweza kukosa ovulation bila kujua
2. Inavuruga mzunguko wa hedhi
Stress inaweza kusababisha:
Hedhi kuchelewa au kuja mapema
Kukosa hedhi kabisa (amenorrhea)
π Bila mzunguko sahihi, ni ngumu kujua siku za kupata mimba
3. Inazuia au kuchelewesha ovulation
Kwa wanawake wengi:
Stress kubwa = hakuna yai linalotoka (anovulation)
Au yai linachelewa kutoka
π Hii inapunguza sana nafasi ya kushika mimba
4. Inapunguza hamu ya tendo la ndoa
Stress huathiri pia akili na hisia:
Kupunguza libido (hamu ya tendo la ndoa)
Kuleta uchovu au msongo wa mawazo
π Matokeo: tendo linapungua hasa kwenye siku muhimu za rutuba
5. Inaweza kuathiri hata upandikizaji wa mimba
Baadhi ya tafiti zinaonyesha:
Stress inaweza kufanya mazingira ya mfuko wa uzazi kuwa si rafiki kwa yai lililorutubishwa
π Hivyo hata mimba ikitokea, inaweza kushindwa kushik**ana vizuri