28/11/2024
SUNGURA NA FISI
*STORIKA KIDOGO*
(nimei copy mahali)
Hapo zamani za kale bwana, kwenye kijiji kilichoitwa 'Mnikome Wachawi' kulikuwa na marafiki wawili, Sungura na Fisi. Walipendana, na wasaidiana kwa hali na mali.
Siku moja walipata mialiko ya shughuli, na shuguli zote mbili zilipangwa kufanyika siku mmoja. Sungura akaamwambia rafiki yake: "Best eh, tujitaidi siku hiyo tuhudhurie shuguli zote mbili." Fisi akamwuliza "Kwanini tusiende kwenye shuguli moja, tamaa ya nini?" Sungura akamjibu "Siku iyo ni siku ya kuufinya mpunga hadi tuvimbiwe, mimi nitaenda kote."
Basi siku ilipofika walikutana nyumbani kwa Sungura wakaanza safari kwenda shuguli ya kwanza. Hapo walikuta shuguli ya ndoa bwana Simba - alikua anamwozesha mwanawe. Walikuta akina mama wanapika vyakula uku wakipiga vigeregere. Sungura akamwambia Fisi; "Kwa kuwa pale ndo kwanza wanaandaa basi twenzetu kwenye shuguli ya pili". Kulikuwa na umbali kidogo. "Twende tukaangalie huko huenda chakula kikawa tayari, tule kisha turudi hapa tena". Lakini Fisi akamwambia "Mimi siendi, hilo sio jambo la busara. Bora tubaki kuliko kua na tamaa." Sungura akakataa wazo la Fisi, akamwacha kisha akatimua mbio kwenda mwaliko wa pili.
Huko, Tembo alikua anafanya arobaini ya mwanawe ambaye alifariki nyuma. Basi Sungura kufika tu, looh masikini akakuta wamemaliza, wanaosha vyombo. " Sungura alichukia, hakutaka kuzubaa aliamua kutimua mbio kurudi kule alikomwacha rafikiye Fisi. Kwa kuwa kulikuwa na kaumbali, ile anakaribia kufika, akamkuta rafiki yake Fisi njiani, anarudi mdogo mdogo nyumbani, Yuko fiti yaani ameshiba. Sungura akashangaa sana, akauliza "Mbona unaondoka vipi?" Fisi akamjibu "Sherehe imeisha, bwana harusi6 kashachukua mkewe. Du, akalia sana. Akarudi nyumbani kwake huku akiwa na njaa na uchovu mkubwa kwa kukimbia umbali mrefu, akiilaumu tamaa yake.