Dr.Joh Healthcare

Dr.Joh Healthcare Mfumo maarifa wa TEHAMA unaotoa habari, elimu na ushauri wa Afya kutoka kwa madaktari kulingana na sera, miongozo na viwango vya utoaji huduma za Afya.

Tupate kidogo elimu ya lishe kwa mama anaenyonyesha
06/02/2025

Tupate kidogo elimu ya lishe kwa mama anaenyonyesha

Lishe bora kwa mama anayenyonyesha ni muhimu sana kwa afya yake na ukuaji mzuri wa mtoto wake. Mama anayenyonyesha anahitaji virutubishi vya kutosha ili kuzalisha maziwa yenye lishe bora kwa mtoto na kudumisha afya yake mwenyewe.

https://imalilo.com/lishe-2/
03/02/2025

https://imalilo.com/lishe-2/

Lishe bora kwa mama anayenyonyesha ni muhimu sana kwa afya yake na ukuaji mzuri wa mtoto wake. Mama anayenyonyesha anahitaji virutubishi vya kutosha ili kuzalisha maziwa yenye lishe bora kwa mtoto na kudumisha afya yake mwenyewe.

https://imalilo.com/unga-wa-rosella-beetroot/
03/02/2025

https://imalilo.com/unga-wa-rosella-beetroot/

Unga wa Rosella (Hibiscus) na Beetroot ni mchanganyiko wenye nguvu wa mimea asilia unaotoa lishe bora kwa mwili wako. Unga huu unatokana na maua ya Rosella yaliyokaushwa na kusagwa pamoja na mizizi ya Beetroot, bila kemikali wala vihifadhi bandia. Rosella inajulikana kwa kuwa na vitamini C nyingi, i...

07/01/2025

DAWA ZA UZAZI WA MPANGO ZINAATHIRI VIPI MZUNGUKO WA HEDHI
Kwanza kabisa tuangalie udhibiti wa hormone katika mzunguko wa hedhi, yaani hormone zipi zinahusika na mzunguko wa hedhi na zinafanya vipi kazi.Kama inavyoonekana katika mchoro huu.

Katika ubongo kuna tezi ya hipothalmas inayozalisha hormone ya Gonadotropini hii hormone inachochea tezi ya pituitari ambayo nayo ipo kwenye ubongo kuzalisha hormone zifatazo

1.hormone chochezi ya mayai (FSH) ambayo huchochea kukua na kupevuka kwa mayai na kuchochea mfuko wa mayai (ovari) kuzalisha hormone za uzazi estrogen na progesterone.

2.Hormone ya lutea ambayo huchochea kuachiliwa kwa yai kutoka kwenye mfuko wa mayai (Ovulation).

Baadae estrogen na progesterone ambazo zinakazi kubwa katika mzunguko zinapokuwa zimezalishwa kwa kiasi cha kutosha zinafanya sasa tezi ya hipothalmus isizalishe tena Hormone ya gonadotropin na kuzuia mzunguko mzima.

Pindi unapokaribia hedhi estrogen na progesterone zinashuka kiwango ili kuruhusu Hipothalmus izalishe tena gonadotropin ili mzunguko uanze tena

JE DAWA ZA UZAZI WA MPANGO K**A MAJIRA ,P2 NA NYINGINEZO ZINAATHIRI VIPI MZUNGUKO?

Kwanza kabisa ile dhana kwamba zinaacha sumu si kweli,
Unapomeza mfano vidonge ndani ya masaa 24 hadi 36 zinakuwa zimeshatolewa kabisa mwilini kupitia ini.

Sasa kwa nini mtu anaweza kukosa hedhi baada ya kuacha kutumia hizi dawa.

Dawa hizi zinakuwa na kemikali ambazo zinafanana na hormone ya progesterone na nyingine zina dawa inayofanana na estrogen.

Zinapoingia mwilini zinafanya kazi k**a hormone hizo na kuziba vijishikizo (receptors) za hormone hizo, mwili huhisi kuwa kuna kiwango kikubwa cha hormone ya estrogen na progesterone matokeo yake hipothalmus inakuwa inactive na kuacha kuzalisha hormone ya gonadotropin na kuathiri uzalishwaji wa mayai na hedhi. Hadi mtu hapati ujauzito. Kwa hiyo znafanya kazi kwa kuvuruga huo mpangilio wa hormone.

Unapoacha kutumia tezi ya hipothalmus kurudia hali yake ya kawaida kuanza kuzalisha gonadotropin inatofautiana kati ya mtu na mtu wengine muda mfupi na wengine muda mrefu kwani mwili umekua tegemezi kwa hizo hormone zilizomo kwenye dawa kuliko zile unazozalisha wenyewe.

HIVO BASI DAWA HIZI HAZIACHI SUMU BALI ZINAVURUGA JINSI MFUMO WA HORMONE UNAVORATIBU MZUNGUKO WA HEDHI

SABABU ZA MAMA MJAMZITO KUTOKWA NA JASHO SANA.DR.JOHANESWanawake wengi katika kipindi cha ujauzito hutokwa sana na jasho...
07/01/2025

SABABU ZA MAMA MJAMZITO KUTOKWA NA JASHO SANA.
DR.JOHANES

Wanawake wengi katika kipindi cha ujauzito hutokwa sana na jasho hasa wakati wa usiku.

Je nini husababisha?

Mabadiliko ya viwango vya vichochezi vya mwili (homornes); kipindi cha ujauzito huambatana na mabadiliko ya viwango vya vichochezi, mabadiliko haya huuweka mwili katika hali ya kuweza kubeba ujauzito kwa kipindi cha miezi yote 9.

Kichochezi aina ya projesteroni huongezeka na kuwa katika kiwango kikubwa katika damu wakati wa ujauzito, mabadiliko haya hupelekea mishipa mingi ya damu iliyo karibu na ngozi kutanuka hivyo kuruhusu damu kupita kwa wingi hivyo kuongeza kiasi cha maji yanayopotea kwa njia ya jasho.

Kutokwa na jasho husaidia kuupoza mwili hivyo hii hutokea ili kuuweka mwili katika hali ya msawazo wa joto.

Kufanya kazi nzito: Mama mjamzito kwa kawaida huchoka haraka hata baada ya shughuli ndogo. Hivyo iwapo mama mjamzito anafanya shughuli nzito huweza kupelekea kuongezeka kwa kiwango cha jasho kinachotolewa.

Maambukizi ya magonjwa: Wakati mwingine kutokwa na jasho sana hasa wakati wa usiku huweza kuwa ni dalili ya mwanzo ya homa (fever) ambayo huashiria kuwepo kwa maambukizi ya magonjwa. Hivyo ni vyema k**a ukiona hali ya kutokwa na jasho si ya kawaida, basi wahi kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.

Je nifanye nini kupunguza kutokwa na jasho sana?

Pendelea kukaa maeneo ya wazi ambako kuna mzunguko mkubwa wa hewa safi.
Pia epuka kuvaa nguo nyingi au zinazobana mwili bali pendelea kuvaa nguo nyepesi kwani huruhusu mzunguko wa hewa.
Pendelea kufanya mazoezi mepesi
Ni vyema kuoga kabla ya kulala
Kwa sababu kutokwa na jasho kwa wingi husababisha mwili kupoteza maji sana hivyo basi ni vyema kunywa maji ya kutosha kila siku.

Address

Bukoba
Bukoba
255

Telephone

+255762167811

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr.Joh Healthcare posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Dr.Joh Healthcare:

Share

Category