23/04/2025
Msanii maarufu kutoka Uganda, , ametangaza kuwa sasa hawezi tena kunywa pombe wala kuvuta sigara, sio kwa sababu ya maagizo ya daktari, bali ni uamuzi wa binafsi baada ya kutafakari afya yake kwa kina.
Akizungumza na wanahabari wa burudani alipowasili JKIA nchini Kenya, Chameleone alisema safari yake haikuwa ya kimatibabu pekee, bali pia ya kukutana tena na marafiki wa zamani.
Akiwa Marekani kwa matibabu, alikiri alipoteza kilo 13 na hapo ndipo alipoamua kubadili mtindo wake wa maisha.
“Daktari hajanilazimisha kuacha, ila nimejipima mwenyewe. Nilikuwa natumia pombe kupita kiasi na kuvuta sigara maisha yangu yote. Kwa ajili ya afya yangu, nimeacha yote hayo.”
Chameleone pia alieleza kuwa alikaribia kufa, na anaamini Mungu amempa nafasi ya pili ya kuishi:
“Hii ni round ya pili ya maisha. Round ya kwanza imeisha. Imebaki miaka mitatu tu nifikishe miaka 50, kuna mambo lazima nipunguze.”
Kuhusu muziki, alisema hajarejea kikamilifu, lakini ana hamu kubwa ya kusaidia wasanii wengine:
“Sihitaji tena kuthibitisha chochote. Mimi ni hitmaker, kazi zangu zinajieleza. Sasa ni wakati wa kuinua wengine. Kusaidia mtu kung’aa hakuondoi mwanga wako.”
Chameleone pia alikumbuka jinsi Kenya ilivyokuwa sehemu ya mwanzo wa safari yake ya muziki miaka 25 iliyopita — hata uhusiano wake wa kwanza wa kimapenzi ulianzia hapa. “Hata mpenzi wangu wa kwanza nilikutana naye hapa Kenya. Hapa ndipo kila kitu kilianzia.”
Ametoa mwaliko kwa wasanii wote wenye ndoto kubwa za muziki:
“Niko Kenya kwa muda, k**a unaamini kwenye kazi yako, njoo tufanye kitu pamoja.”
Powered By: