15/02/2022
UVIMBE KWENYE KIZAZI
Kuna magonjwa ndani ya mji wa uzazi ambayo pengine huweza kusababisha harufu licha ya mchanganyiko wa kawaida katika taratibu za utungaji mimba.
Wengi hupatwa na uvimbe au vimbe mbalimbali ambazo huweza kusababisha kutokwa na uchafu, harufu na pia kusababisha kuharibika kwa mimba au kukosa kushika mimba kabisa.
Fibroid
Aina ya fibroid (s ), yaani uvimbe kwenye mji wa mimba.
Dalili:
Dalili zake ni hedhi nzito kupita kiasi, utokwaji wa uchafu ukeni, mimba kuharibika, maumivu chini ya kitovu kwa katikati, kuongezeka kwa tumbo kadiri uvimbe huu unavyoongezeka, n.k.
Ovarian Cyst
Hii ni aina ya uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke. Hutokea kwenye vifuko vya mayai ya uzazi, kwa ndani au kwa nje, na yaweza ikawa kwenye kifuko kimoja cha mayai au vyote viwili.
Dalili
Dalili kubwa ya uvimbe wa aina hii ni kichomi chini ya kitovu na sehemu moja. Kichomi huzidi sana mgonjwa anapocheka kwa nguvu au kuinama au anapobeba vitu vizito.
Dalili nyingine kubwa ni kuwa na tatizo la hedhi inayokoma kwa zaidi ya miezi mitatu, tatizo ambalo kitaalamu huitwa Amenorrhea, maumivu wakati wa kutoa haja ndogo na kutoa haja ndogo mara kwa mara, maumivu ya kiuno kwa nyuma, maumivu wakati wa kujamiiana, maumivu makali wakati wa hedhi, kupoteza hamu ya kula, kuongezeka uzito na unene kwa kiasi.
Mwanamke anapoona dalili zaidi ya moja kati ya hizi awahi kwenda hospitali.
Je huna mtoto? Unapata changamoto ya kupata mtoto? Basi wasiliana nasi kwa ushauri na utatuzi kwa simu namba 0763 031270